Ni changamoto na mafanikio yapi ulipitia wakati ukifanya internship/ kujitolea?

Mtu Kwao

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
394
Reaction score
720
Habari Wana jamvi,

Katika dunia ya Sasa hasa nchini kwetu swala la ajira limekuwa ni kilio kikubwa sana.

Siku hizi kupata ajira ni kama bahati au connection yani kupata ajira kwa ujuzi wako imekuwa nadra sana.

Wapo waliomaliza chuo nakupa kazi moja kwa moja wapo walio subiri kwa zaid ya miaka mi 5 huku wakijitolea lakini pia wapo ambao mpaka Sasa hawajaweza kupata ajira au ata intern kikubwa nikutokukata tamaa tu.

Nikija kwenye dhumuni la uzi huu je ulipitia changamoto zipi wakati ukifanya intern.

Wengi tunajua intern nyingi watu huwa hulipwa lakini kwangu ilikuwa tofauti kabisa.

Binafsi nakumbuka baada ya kumaliza chuo nilituma maombi ya kazi na intern sehemu mbalimbali lakini nilibahatika kupata intern kwenye kampun fulan binafsi.

Dah pale ofisini nilikuwa silipwi chochote na wale jamaa niliowakuta nikama walijua Mimi ndo mkombozi wao wa kufanya kazi. Kazi zote nilikuwa nafanya Mimi ilifika kipindi nikawa natoka home na mandazi kwenye begi ule muda wa kula wenzangu wakienda kunywa chai na Mimi natoka nje kwenda kula mandazi yangu na maji[emoji1] kilichokuwa kikiniuma mtaani watu walikuwa wanajua nafanya kazi kwenye kitengo fulan huko serikalin maana nilikuwa najitahidi walau kupendeza lakini napo ilifika hatua nikachoka nguo zikaanza kuchakaa sabuni nakosa asee kwangu nilipitia wakati mgumu Sana.

Lakini nachoshukuru kupitia intern hiyo niliweza kujiongezea ujuzi zaidi na uzoefu lakini kubwa kupitia hapo ndo palinifungulia njia ya kupata kazi nzuri ambayo ndo nipo mpaka sasa.

Je wewe ulipitia changamoto gani wakati wa intern/kujitolea na je unakipi Cha kuwaambia ndugu zetu ambao bado wapo huko au wanakaribia kwenda huko.

Karibu..

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Watu walioajiriwa wanaowaona ma intern na PT student maboya wanadharau sana vibaya mno ila nashukuru kupitia dharau zao nilipata uzoefu na Wizara ya ajira ikaniona na kunipa kitengo😎
 
Ujijitolea sehemu kwa mda mrefu unadharauliwa unaonekana kilaza hupati kazi ila ukiaga unataka kuondoka wanakudanganya tupo kwenye process za kukupa mkataba kwa hyo ukijitolea sana kwenye sehemu moja unajishusha thamani.
 
Na hili ndo tatizo kubwa Sana mkuu

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa nashinda na njaa siku nzima kuanzia asubuhi mpaka narudi nyumbani saa kumi na mbili wale majamaa ikifika muda wa chakula wanaondoka mmoja mmoja kwenda kula.

Nilikaa pale ofisini kwa miezi mitatu.
 
Nilijitolea 2 months nikiwa napata tabu San kuhus Nauli na mamb ya msosi lkn nilikuw natafut chansi nionane na mkurugenz Tu maan kuanzia Meneja, HR , Mhasib mkuu adi Supervisor wote nilikuw naon Kam hawaon umuhim Wang lkn Mkurugenz niliongea DKK 5 Tu alinielew saw na akaniandikia Barua niwe nachukua kila mwsh WA wiki 65k Kw Cashier Kam posho ya kujikimu angalau kidg mamb yalikuw sawq.
 
Back
Top Bottom