Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Kupitia huu uzi na wachangiaji wa mada wanavyodadavu wengine tunajifunza jinsi ya kujihami na wezi. Kwa mfano, mimi nimejifunza mbinu ya kuacha maji wazi ili kujihami na wezi wanaotumia Kloroform wengine tulikuwa hatuijui.
Exactly! Hii ndiyo nguvu ya akili kubwa & positive minded people. Siyo wale ambao wanaangalia negatives tu eti oh wezi watapata mbinu....
 
Za bei chee kama kiasi gani?
 
Hii ya kutolea mafuta pikipiki/gari usiku alikuwa ananikumbusha sana mzee ila sikujua maana yake hadi siku majambazi walipotutembelea usiku wakata nyaya ili wawashe kitu waondoke ikagoma wese hamna na ndo ikawa salimika ya huo mchuma ilikuwa 1997
Yaani Ni kwikwi babuu
 
Nilikuwa nawaza kwa sauti hii mbinu ya maji...
Lakini nikawa najiuliza kuwa litaulizwa swali uhusiano uliopo baina ya hiyo dawa na maji, kwa nini maji yakiwepo haiwezi kufanya kazi!!

Cloroform ni solube kwy maji kwa iyo inapoteza ile concentration yake eventually haiwezi kukuletea madhara yake ya usingizi,kutosikia,nk! Huwa ina harufu flan nzuri ivi na ni nyepesi sana kuivuta km hewa! Inatokana na mchanganyiko wa chlorine na methane!nchi za wenzetu huinunui kienyeji mpk uwe na vibali kutoka kwy malaka husika za dawa na chakula etc
 
Sio mwanamke tu mkuu hata kidume wanaweza legeza marinda.ukiona wamesepa na zagazaga na wewe wamekuacha salama unscathed ni jambo la kushukuru mungu.
aisee inabd uwashukulu maana unakuwa kama umekufaa
 
hawakupika supu mkuu wakashushia na viroba?
 
JF GREAT THINKER

MODS PELEKA HII JUKWA LA INTELLIGENCE ALAFU IWE STICKY.
 
upo sawa kabsaa mkuu sio kila mtu anaibiwa kijinga
 
Siyo siri nawachukia sana wezi, mwaka jana walivunja mlango wakaingia mpaka chumbani kwangu nilipokuwa nimelala na kubeba kila kitu, wakabeba na chupa ilikuwa na chai na maandazi wakasepa nayo
Mnanivunja mbavu jama
 
Ukiibiwa njoo PM nikuunganishe na wataalaam, vifaa vyako utavipata bila shaka.
 
Naona hii ya beseni la maji iko passed
Mkuu kuwa makini na kitu wenye kizungu wanachoita ''myth''. Ni kitu kibaya sana. Mimi nimepitia maelelezo yooote hapa lakini kila nikijaribu kuunganisha kwa kutumia sayansi naona nyota nyota. Kwa mfano chukulia mwizi amekuja na hiyo dawa wanayosema inakufanya ulale. Akaipulizia dirishani. Wewe umeweka maji kwenye karai chini ya dirisha lako. Sasa jiulize: Yale maji yana nguvu ya uvutano ya kuvuta ile dawa ielekee kwenye karai lenye maji na isielekee puani kwako? Katika hali ya kawaida itakimbilia puani kwenye nguvu ya kuvuta au kwenye beseni? Huoni hapa kuna maswali mengi kuliko majibu? Hii ya maji kwenye karai ni hadithi ya kusadikika na mimi sitaiamini kwa namna yoyote. Wengine wamefikia hatua ya kusema wanakuja na chloroform hivyo ukiweka maji yanai-netralize! Kweli mtu aliyesoma chemistry hili linaingia akilini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…