Ni dhahiri maendeleo ya vitu hayaleti maendeleo ya watu. Fanyeni tathimini upya

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,480
Reaction score
7,443
Wana Jf, ni wazi kuwa serikali inapofanya maendeleo ya vitu hasa kujenga miundo mbinu, viwanda, na kuboresha sekta zote za kiuchumi lazima zilete matokeo chanya kwenye maisha ya watu.

Lakini serikali ikijigamba kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu ambavyo havileti matokeo chanya kwa maisha ya watu basi ni kama kutwanga maji kwenye kinu na kujenga chuki.

Hebu fikiri, kwa haya maendeleo ya hizi Megastructures mnazojisifia kuwa mmezijenga ndani ya miaka minne, mbona wananchi wanazidi kuwachukia ninyi na serikali yenu?

My take; Jitathimini wapi mmekosea.
 
Duniani kote mtu huwa ndio kiini na kipaumbele cha mipango ya serikali. Na mambo yanayogusa mtu kwa maisha yake ya kila siku ni Elimu, Afya, Chakula. Mtu anaweza kukaa mwaka mzima hajapita kwenye hizo barabara za juu wala kupanda ndege. Lakini mambo ya afya, elimu na chakula ni ya wakati wote. Kwenye maeneo hayo ndiko vipaumbele vya serikali viwekwe. Kwa mfano mtu wa kawaida wa Kule Nkasi, Rukwa hiyo Flyover ya ubungo inamsaidiaje? Hiyo stendi ya Jiwe ya Mbezi iliyokula mabilioni ya fedha ina faida gani za moja kwa moja kwake?

Serkali yoyote isiyowekeza kwenye mambo yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja huwaacha wananchi hao kwenye giza nene wasijue seriakli yao inafanya nini. Ni kama wanasimuliwa tu kinachofanyika ila wa hawaoni maana hakiwagusi wao kwenye maisha yao ya kila siku.

Hivi kwa mfano ajenda ya awamu hii ya kuua upinzani ina faida gani kwa mwananchi wa kawaida? Mamilioni ya fedha yanatumika kuwarubuni akina Mdee na COVID-19 wenzake na wanaendelea kulipwa mamilioni ya fedha bure tu. Kuna faida gani?

Unashindwa kuwaongezea watumishi wa umma mshahara ambao ni haki yao lakini unakuwa na mamilioni ya fedha ya kuwalipa wabunge 19 ambao hawana chama wanachokiwakilisha kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.

Kwa nini kila kitu tutangulize siasa mbele? Kwa maslahi ya nani?
 
Hivi kwa mfano ajenda ya awamu hii ya kuua upinzani ina faida gani kwa mwananchi wa kawaida? Mamilioni ya fedha yanatumika kuwarubuni akina Mdee na COVID-19 wenzake na wanaendelea kulipwa mamilioni ya fedha bure tu. Kuna faida gani?

Unashindwa kuwaongezea watumishi wa umma mshahara ambao ni haki yao lakini unakuwa na mamilioni ya fedha ya kuwalipa wabunge 19 ambao hawana chama wanachokiwakilisha kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.
Jiwe alidhani kwa kuuwa upinzani angelianza kuabudiwa.
 
Hakuna nchi hapa Africa yenye miundo mbinu mizuri kama SA lakini kila siku kuna service protests,Ethiopia vile vile na sisi tunajidanganya hatuna barabara bora ILA tuna vipande vya barabara bora mfano daraja la Nyerere,igawa to sao hill(why matuta kwenye freeway?)
 
Wana Jf, ni wazi kuwa serikali inapofanya maendeleo ya vitu hasa kujenga miundo mbinu, viwanda, na kuboresha sekta zote za kiuchumi lazima zilete matokeo chanya kwenye maisha ya watu.

Lakini serikali ikijigamba kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu ambavyo havileti matokeo chanya kwa maisha ya watu basi ni kama kutwanga maji kwenye kinu na kujenga chuki.

Hebu fikiri, kwa haya maendeleo ya hizi Megastructures mnazojisifia kuwa mmezijenga ndani ya miaka minne, mbona wananchi wanazidi kuwachukia ninyi na serikali yenu?

My take; Jitathimini wapi mmekosea.
Uko sahihi ndugu. Itanichukua miaka mia kuniaminisha kwamba lile daraja pale COCO BEACH sio uharibifu wa pesa zetu walipa kodi. Kulikuwa na haja gani na uharaka gani wa kulijenga? Litamfaidisha nani hasa? Bora ile pesa ingejenga vyumba vya madarasa Dar ambako baadhi ya shule za umma watoto wanakaa chini na wengine wanasomea chini ya mikorosho.
 
Wana Jf, ni wazi kuwa serikali inapofanya maendeleo ya vitu hasa kujenga miundo mbinu, viwanda, na kuboresha sekta zote za kiuchumi lazima zilete matokeo chanya kwenye maisha ya watu.

Lakini serikali ikijigamba kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu ambavyo havileti matokeo chanya kwa maisha ya watu basi ni kama kutwanga maji kwenye kinu na kujenga chuki.

Hebu fikiri, kwa haya maendeleo ya hizi Megastructures mnazojisifia kuwa mmezijenga ndani ya miaka minne, mbona wananchi wanazidi kuwachukia ninyi na serikali yenu?

My take; Jitathimini wapi mmekosea.
Hiyo ni miradi ya kupigia 20% wakubwa wala hakuna la maana hapo
 
Hakuna nchi hapa Africa yenye miundo mbinu mizuri kama SA lakini kila siku kuna service protests,Ethiopia vile vile na sisi tunajidanganya hatuna barabara bora ILA tuna vipande vya barabara bora mfano daraja la Nyerere,igawa to sao hill(why matuta kwenye freeway?)
Watu wengi humu ni wajinga na mazuzu,hivi mkulima aliyepo nindo shinyanga vijijini,ananufaikaje na dengu zake pamoja na choroko kama hakuna barabara ya kuzisafirisha?!, mgonjwa aliyeko migori anafikaje dodoma kujifungua km hakuna barabara?!, kweli ujinga ni mzigo,
 
Back
Top Bottom