Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

myself scenario

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2015
Posts
347
Reaction score
213
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..

Nawasilisha..karibuni
 
Anaejua ni Mwenyezi Mungu mwenyewe hiyo faida anayoipata kwa hiyo ni ngumu kwangu Mimi Kama mwanadamu kujua faida anazopata isipokuwa mi ninachojua ni kutii amri zake!!!!!
Unaweza mtafuta mwenyewe ukamuuliza labda atakuwa na majibu.
 
Ukijibiwa
Utapata faida gani?

Ulipoambiwa usizini, kwanini ulizini? Na ulipozini ulipata faida gani? Zaidi ya kujutia na kujilamu!
Ulipoambiwa usiseme uongo,usitamani mwanamke/mume asiye wako,usiibe,usiue,usiseme uongo,waheshimu baba na mama,n.k ulipovunja yote hayo/au moja kati ya hayo ulipata faida gani?
 
Mungu mwenyewe hapendi wanadamu waangamie bali wafikirie toba. Jehanam iliweka kwa ajilu ya Ibilisi na Malaika wake. Binadamu kwa ukaidi wetu na jeuri zetu tunaikataa nuru na kuenenda katika giza. Kwa hiyo si suala la kuuliza faida apatayo Mungu wakati tumeshapewa option sahihi kuepuja moto wa milele
 
Ukijibiwa
Utapata faida gani?

Ulipoambiwa usizini, kwanini ulizini? Na ulipozini ulipata faida gani? Zaidi ya kujutia na kujilamu!
Ulipoambiwa usiseme uongo,usitamani mwanamke/mume asiye wako,usiibe,usiue,usiseme uongo,waheshimu baba na mama,n.k ulipovunja yote hayo/au moja kati ya hayo ulipata faida gani?

Kwanini unakimbilia mahubiri badala ya kustick kwenye swali? Ama umeamua kuongeza maswali yako kufanya mtihani uwe na maswali mengi zaidi?
 
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..

Nawasilisha..karibuni
Mungu hayupo! Ni mastory ya watu tu wajanja ! Nakuuliza swali: Kama Mungu aliwaumba Adamu na Eva, walikuwa weupe, sasa weusi , wachina, wazungu walitoka wapi? Aliwaumba siku moja, ilikuwaje wakaa kama walivyo sasa hivi! Kwa nini Mungu aliumba bacteria, virus etc wa kumuumiza mwanadamu? Aliwaumba lini na tunaambiwa aliumba vitu vya kumsaidia mwanadamu! Maswali ni mengi ukiyatafakari unaambiwa UNAKUFURU ili usidaisi
 
Back
Top Bottom