mwanaMtata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2014
- 2,393
- 1,433
Nikosoe kama nitakosea...Salaaam..
Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.
Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.
Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..
SWALI:
je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??
Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..
Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??
Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..
Nawasilisha..karibuni
Kuna mfano niliwahi kupewa nikiwa mdogo naomba nikupe na wewe.
"Kuna Mtu alikua anahoji na kutafakari sana utemdaji kazi wa MUNGU. Alitaman sana kujua chanzo mipango na mengi kuhusu MUNGU. Siku moja akiwa pembeni ya ufuko wa bahari aliona katoto kadogo kamechimba shimo kando ya bahari, na kanafanya kazi ya kwenda kuchota maji baharini kuyaleta kujaza kwenye shimo lake. Alishindwa kuvumilia na kumuuliza yule mtoto unafanya nini?
Mtoto akajibu "nataka kuhamisha maji ya bahari niyajaze hapa kwenye shimo langu"
Alimcheka sana yule mtoto na kumuona mpumbavu kisha akaondoka na kitudi alipokua amekaa. Alipofika akageuka hakumuona yule mtoto"
[emoji120] moral of the story ni kwamba, ubongo wa mwanadamu ni kale ka shimo na UMUNGU ni ile bahari. Haviwezi kutoshana.
Stay humble and your GOD will have mercy on your soul at the end of time