Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Nikosoe kama nitakosea...
Kuna mfano niliwahi kupewa nikiwa mdogo naomba nikupe na wewe.
"Kuna Mtu alikua anahoji na kutafakari sana utemdaji kazi wa MUNGU. Alitaman sana kujua chanzo mipango na mengi kuhusu MUNGU. Siku moja akiwa pembeni ya ufuko wa bahari aliona katoto kadogo kamechimba shimo kando ya bahari, na kanafanya kazi ya kwenda kuchota maji baharini kuyaleta kujaza kwenye shimo lake. Alishindwa kuvumilia na kumuuliza yule mtoto unafanya nini?
Mtoto akajibu "nataka kuhamisha maji ya bahari niyajaze hapa kwenye shimo langu"
Alimcheka sana yule mtoto na kumuona mpumbavu kisha akaondoka na kitudi alipokua amekaa. Alipofika akageuka hakumuona yule mtoto"


[emoji120] moral of the story ni kwamba, ubongo wa mwanadamu ni kale ka shimo na UMUNGU ni ile bahari. Haviwezi kutoshana.
Stay humble and your GOD will have mercy on your soul at the end of time
 
Kama unaweza wasiliana naye ajupe jibu.ukisoma maandiko inaonekana kama atawaacha wasio wake bila msaada.kwakuwa patakuwa hakuna kufa tena watakaobaki nje watajijua wenyewe.sidhan kama ni moto as moto ila kuachwa na Mungu si jambo zuri kabisa
 
Hakuna cha moto wala nini, hayo ni mafundisho ya kipagani.
 
Vitakuwa vilianza sawa.
Sijakuwelewa, unamaanisha viumbe vilikuwepo kipindi universe inaanza na wakaanza pamoja? Kwa kuwa hauamini uwepo wa mungu hii nadharia yako inajipinga hata theory ya evolution. Oxygen iliibukia miaka 2bilion iliyopita sasa mwanadamu na viumbe vingine kipindi universe inaanza walitumia hewa gani kuadapt mazingira? Mkuu au we unaamini katika ubudha?.
 
we
Ni faida gani ataipata kupeleka watu wema peponi!!?

Labda tuanzie hapo mkuu..
kwa mfano kama wewe ni mkulima baada ya mavuno,mazao ukiyaweka ghalani na makapi kuyatupa na kuyachoma moto unapata faida gani
 
Yupi sasa kati ya Allah, Yesu, Yehova, Buddha, Haile ssalasi[emoji32]
 
Mungu hamchomi Mtu ,moto ndio unachoma , moto umewekwa kwa ajili ya shetani wewe unayekwenda jehanum ni kiherehere chako tu , acha dhambi nenda mbinguni hutaki utaenda jehanum tu Na huko huchomwi nu Mungu ni wewe mwenyewe umejipeleka kwa kutotiii Amri za Mungu ,
 
sasa mtoa mada nawe jiulize kuna faida gani anayoipata hakimu baada ya kumfunga mwalifu? hayo yote yamewekwa ili Neno litimie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…