Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Tukisema kwamba kuna sehemu ambapo Mungu yupo na kuna sehemu ambapo Mungu hayupo maana yake ni kwamba huo Dunia haija tengenezwa na Mungu. Dunia sio creation ya Mungu. Yaani yako vitu vilivyo tengenezwa na Mungu na vitu ambavyo havijatengenezwa na Mungu. Bali ni Shetani. Yaani kuna Dunia mmoja ya Mungu na pia kuna Dunia ya pili ya Shetani aliye tengeneza Shetani. Na kwamba Binadamu anaishi kwenye Dunia Mbili.
Hiyo haiwezekani kwa sababu Dunia nzima mmoja imetengenezwa na Mungu. Haziko Dunia mbili. Pamoja na hiyo lakini hakuna sehemu ambapo Mungu haupo. Maana yake ni kwamba hata kwenye mwili Mungu yupo. Kwenye kila tende ya mwili Mungu yupo. Kwenye hewa, maji, moto, nafasi tupu, ardhi, kweye kila kitu Mungu yupo. Hata kwenye mawazo, akili Mungu yupo.
Pamoja na hayo Mungu amejipanga mawasiliano yote kwenye taratibu tunaloliona kisayansi. Nikiingiza mkono kwenye moto nitaungua. Kadhalika kila kitendo kinakuwaga na tokeo / matokeo yake. Na sio kwamba matokeo lazima yatoke baada ya kufa. Matokeo yako kila sekunde.
Kitu cha maana kwa kweli ni kwamba God made Man in his own image. Tujue kwamba Mungu upo mwilini pia. Na kitu cha maana zaidi ni kwamba Whole world is image of God.
Kwa hiyo nikijua kwamba kwenye kila kitendochangu Mungu Upo, na nikijua pia kwamba Mungu ni mwenye busara, pendano, uzuri na uwezo wa hali ya juu wa mwisho vitendo vyangu vyote vitakuwa hivyo. Na matokeo pia ya vitendo vyangu yatafanana kwa sababu matokeo pia yakuwaga kisayansi. Ila nikifanya mambo ya chuki ya kuumiza wengene; kisayansi matokeo yatafanana na si lazima kwamba matokeo yatasubiriwa siku ya mwisho.
Asanteni.
 
Hujui faida za kuzini?
 
Inafika mahali mtu unaweza kufikia hitimisho kuwa hivi vitabu kuran na biblia ni watu walijifungia mahali kwa mitazamo yao na matakwa yenye malengo yao binafsi wakaviandika. Kmsingi mimi naamini mungu au shetani mm ndiye ninaemuumba kupitia mawazo au matendo yangu mazuri au mabaya na mambo yanaishia hapa hapa ktk haya maisha. Hivi kuna mtu anaishi ana maradhi anateseka ajabu, mwingine pa kulala, kula ni tabu kubwa eti halafu tena akachomwe,wakat wengine wanakula na kusaza, huyo mungu si atakuwa katili sana.
 
Kwa nini sheria ikawepo? Ni kwa sababu kuna kuzini na mungu alijua hilo.na yeye ndiyo muumba wa vyote,mwenye nguvu zote ,aliumba mema na mabaya ata lusifa alimuumba yeye.KWAHIYO yote tuyafanyayo ni matakwa na mitego ya MUNGU na si kumpakazia lisifa.
 
Halafu huyo shetani bhana mi namkubali kitu kimoja tu ukitaka hela anakupa hapo hapo siyo eti unapiga magoti na kulia miaka na miaka ata usijue km utapewa. Ila nikibahatika kukutana nae ningemwomba alegeze au apunguze mashart. Hapo ndipo nae anazinguaga.
 
Kamuulize yeye!

Mungu hawezi kuchoma moto na wala hapeleki watu motoni bali wao kwa kumkataa watajichoma moto wenyewe.

Ndiyo maana Mungu siku zote ni wa rehema na ana saburi/subira pia.
 
hutofautiani na ngombe au mbuzi!maana wao hawana akili!ww kama unazo akili basi wapo waliokua kabla yako nawao pia walikua na watangulizi wao!ushaambiwa hiyo ni moto ukigusa unaungua!sasa unabisha haya jaribu kuishika utapata majibu yake!na hapo ndo kasoro yako ya kua huna akili!samahani kama nitakua nimetumia neno kali ila sijaona neno sahihi ya kukuelezea!umri wako wenyewe hautazidi sitini (60)karne kibao zimekupita!halafu unakuja kuwabishia waliokua kabla yako!nyie ndo wale minaljinnati wannaas.
 
Ukitaka huo moto usitupate tuwe wacha mungu
Ukifanya jema Moja ×700
Ukifanya ovu Moja ×1
Ukiwa Na nia ya kufanya jema unaandikiwa jema
Ukiwa Na nia ya kufanya ovu huandikiwi chochote
Kutokana Na hizo hisabu binadamu moto wa jehannam anautaka mwenyewe
Mimi ni mwalimu nimewapa mtihani watoto afu nkawapa majibu ya ukweli Na ya uongo pia nkawaambia Na kuweka wazi kuwa haya ni ya uongo Na haya ni ya ukweli..atakaefeli ntamuadhibu.
Hapo atakaeadhibiwa kataka mwenyewe.
 
Hakuna moto ila wote tunaenda mbinguni ila huko kuna mahakama za kutoa haki . Mbingu ni moja ila kuna vyumba vya watu mbalimbali kulingana na maisha ya duniani . Ishi bila hofu mbingu ni ya wote ,vunja mifupa bado meno ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…