Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Kwenda motoni au uzimani ni chaguo lako wala Mungu hakulazimishi. Kwa upendo wake ametupa uhuru wa ama kutenda mabaya ama mema.. ila kila tutendalo lina malipo yake..
Yah kuna malaika wanaitwa Raqiib na Atiid.Malaika hawa kazi yao ni kunakili yale mema na mabaya ya watu.
 
Hivi kuna mtu aliewah kwenda akarudii akasema kuna moto huko ,au stori tu
 
Nadhan hoja ya msingi hapa si swala la kuchomwa....bali lile swala la kuchomwa milele....hapo kwenye umilele ndo panaleta utata hasa....! Mfano umefanya dhambi miaka 80 yaan uhai wako wote...vip uje uchomwe milele na milele daima?! Na daima?! Si swala lenye haki kwakweli!
Si kila mtenda dhambi atachomwa milele kwa kuwa dhambi zinatofautiana hivyo basi mwenyezi Mungu mtukufu atawaadhibu waja wake kulingana na makosa yao.Ila wapo wataochomwa moto milele ambao ni wale ambao wanaabudu viumbe vingine mbali na yeye,kwa mfano wale wanaoabudu sanamu, miti,ng'ombe n.k

Pia kundi jingine ambao watachomwa moto wa milele ni wachawi
 
Tatzo mungu mwenyewe kajificha sijui anaogopa nn kujitokeza,,!'
Hata kipindi cha nabii Mussa kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona Mungu kama wewe unavyotaka.
Mungu akaona haina shida ngoja ajitokeze,kimbembe kikaja wakati anakuja wale watu wakaanza kulia na kuomba msamaha kwa kuwa mwenyezi Mungu alikuwa anashuka na nuru ya ajabu kiasi kwamba wale watu walishindwa kustahimili

Kwa hiyo kwa kutumia mfano huu tunajifunza ya kuwa sisi viumbe vyake hatuna uwezo wa kumuona yeye Mungu kwa kuwa hatuna nguvu za kiroho za kutosha kuweza kuonana nae

Ila kipindi cha Qiyama wale watu ambao watapata bahati ya kuingia peponi ndio pekee ambao watamuona Mungu ila kwa wale wataokwenda motoni hawatamuona Mungu kamwe

Si hivyo tu bali hata kwa hawa wataopata bahati ya kuonana nae hawataweza kumkumbuka hata kidogo.
Hapa namaanisha kwamba hawa watamuona mara kwa mara Mungu pale watakapotaka kumuona wataomba kidogo then Mungu atajitokeza wakisharidhika Mungu anarudi kwenye makazi yake sema image yake haiwezi kukaa vichwani mwao mara kwa mara
 
Alaf ngoja nisahihishe na hapa kidogo,jamani wana jamii forum kuanzia leo na kuendelea kaa ukijua kwamba hakuna kiumbe kinachoitwa *SHETANI*

Shetani linatokana na kitenzi ushetani ikimaanisha tendo au matendo yasiyo mpendeza Mungu.Hivyo basi yule kiumbe hai yeyote iwe binadamu au jini anayefanya matendo yasiyo mpendeza Mungu ndio anapachikwa jina la ,'Shetani'

Ila kuna kiumbe kinaitwa Ibilisi huyu ndiye kiumbe ambae ni adui namba moja wa mwenyezi Mungu na alimuahidi Mungu kuwa hata ingia jehhanaamu peke yake bali hatahakikisha kuwa atawarubuni na viumbe wengine.
 
Ukifikiria tu hio pepo ilivyo enyewe nikama inasound as boring place, mko kwenye park mnamuimbia bwanatu, tena mnakaa hapo milele, kweli mtu hatachoka apo
Hapana sio kweli.Jannah au pepo kwa kiswahili ni sehemu yenye bustani yenye matunda aina mbalimballi na penye mito inayopitisha maji mazuri na matamu kuliko asali na meupe kuliko maziwa na yana harufu nzuri kuliko miski.
Hakuishia hapo tu bali Mungu aliendelea kusema kuwa peponi kuna majumba mazuri tu ya kifahari na starehe mbalimbali pia zipo ambazo jicho la binadamu halijapata kuona.Vilevile peponi kuna wanawake wazuri sana wameandaliwa wanaitwa hur'lain

Mungu akuishia hapo bali aliendelea kusema kuwa peponi hakuna mambo ya kwenda haja ndogo wala kubwa.
 
Mm naamini mwenyezimungu hana kurugenzi ya mawasiliano kama zilivyo ikulu zetu.
Kurugengi ya mawasiliano ya mwenyezimungu ni vitabu vyake tu.
Na wala mwenyezimungu hana msemaji wake hapa duniani kama tulivyo na Haji manara na wengine.
Mwenyezimungu anamiongozo tu ya jinsi gani anataka tuitumie ktk ulimwengu huu miongozo hiyo ni vitabu vyake alivyo tuteremshia yaani Quraan Taurati Injili nk.
Kwaharaka tu jibu lake ni kuwa atafaidika kwa kutimiza ahadi alizo tuahidi waja wema atawapa malipo mema na waovu atawalipa uwovu ikiwemo huo moto.
Mwenyezimungu atuepushe na ghadhabu zake na moto kesho akhera AMEEN;
Hapana sio kweli,Mungu ana njia nyingi tu za mawasiliano kama vile kupitia revealition (ufunuo) ambayo hii wamejaaliwa mitume na wale wacha Mungu haswa.

Alaf sio kweli kwamba Mungu hana wasemaji.Mungu anaowasemaji wengi kama vile malaika,mitume,masheikh na ,mapadri.
 
Nashindwa kabisa kupata majibu ya maswali yangu kwa maana. Cha mwisho ninachojibiwa ni kua ninakufuru.. Eeeh Mungu kam kweli upo hebu nipe muongozo kwa mambo yanayonitatiza
Siku zote ukitaka kumjua Mungu usitumie akili ya kawaida ya kibinadamu pamoja na sayansi tunayosoma mashuleni kwa kuwa utaishia kuwa mpagani.

Siku zote sayansi ipo kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kuleta ukinzani juu ya maswaala ya dini na imani kwa ujumla.
Alaf sio kila kitu knowledge yake inapatikana katika vitabu vya mashuleni mfano Yesu aliweza kupaa na kwenda kwa Mungu,uwezo huu hauwezi ukaupata kwa kusoma vitabu vya sayansi kama vile fizikia,kwa kuwa ukisoma vitabu hivi vitakuambia ili kitu kipae lazima kani ya msukumo iwe kubwa kuliko kani ya mvutano.

Au mfano mwingine ni kuhusu hawa wachawi ambao wanaweza kuyeyuka na kupaa na ungo.Sayansi hii pia haipatikani kwa kuingia darasani bali ni imani tu basi

Kwa kumalizia ni hivi wewe kuwa na imani juu ya muumba wako na jirudi kwake ili upate kusamehewa.Kwa kuwa Mungu mwenyewe kashasema hata uwe na dhambi mithili ya damu ukimuomba msamaha atazitakasa dhambi zako na kuwa nyeupe mithili ya theruji.
 
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..


Nawasilisha..karibuni
Hamna atakayechomwa
 
Mwenyezi mungu alishasema hawezi kuiangamiza tena dunia kwa moto wala maji(gharika) sasa sijui hii ya moto umeipata wapi
 
Adhabu ya moto aliitoa Sodoma na Gomora na gharika au maji kizazi cha Nuhu na harudii adhabu chagua nyingine
 
Mimi nadhani Mungu alipatwa na maghazabu makubwa baada ya shetani kwenda kinyume, alikasirika sana. Kwahiyo kuhusu hukumu ya milele itakuwa hasira yake ndo itaishia hapo.
 
Mwenyezi mungu alishasema hawezi kuiangamiza tena dunia kwa moto wala maji(gharika) sasa sijui hii ya moto umeipata wapi
Hapana umemnukuu vibaya mwenyezi Mungu.Ujue zamani Mungu alikuwa anateremsha adhabu papo kwa hapo binadamu anapotenda matendo yasiyompendeza yeye(Mungu).
Lakini baadaye Mungu akaamua kubadilisha adhabu za papo kwa hapo na kuamua kuwaweka viporo wale wanaoomkosea ili awape adhabu siku ya hukumu itakapo wadia.
 
Soka Malaki 4 Biblia inasema waovu wataangamia na kuwa majivu na kisha dunia itaumbwa upya na watakatifu wataishi humo bila dhambi. Faida aipatayo Mungu ni kuteketeza dhambi, kwa kuwa shetani na wafuasi wake wameng'ang'ania dhambi licha ya wokovu wa bure kupitia kwa Yesu Kristo. Moto wa milele hautawaka siku zote ila huitwa wa milele kwa sababu utateketeza waovu pamoja na shetani na malaika zake watoweke milele. Kama una swali zaidi niulize kuhusu moto wa milele.
Umeongea mengi tena vizuri kabisa,kwa maelezo yako ni kwamba moto wa milele haupo au sio??
 
Anaejua ni Mwenyezi Mungu mwenyewe hiyo faida anayoipata kwa hiyo ni ngumu kwangu Mimi Kama mwanadamu kujua faida anazopata isipokuwa mi ninachojua ni kutii amri zake!!!!!
Unaweza mtafuta mwenyewe ukamuuliza labda atakuwa na majibu.
UMEJIBBU VIZURI SANA. SINA CHA KUONGEZA WALA KUPUNGUZA.NAKUBALIANA NA JIBULAKO 100%
 
Back
Top Bottom