brigedia mafia
JF-Expert Member
- Jul 21, 2016
- 2,260
- 2,279
Yah kuna malaika wanaitwa Raqiib na Atiid.Malaika hawa kazi yao ni kunakili yale mema na mabaya ya watu.Kwenda motoni au uzimani ni chaguo lako wala Mungu hakulazimishi. Kwa upendo wake ametupa uhuru wa ama kutenda mabaya ama mema.. ila kila tutendalo lina malipo yake..
Si kila mtenda dhambi atachomwa milele kwa kuwa dhambi zinatofautiana hivyo basi mwenyezi Mungu mtukufu atawaadhibu waja wake kulingana na makosa yao.Ila wapo wataochomwa moto milele ambao ni wale ambao wanaabudu viumbe vingine mbali na yeye,kwa mfano wale wanaoabudu sanamu, miti,ng'ombe n.kNadhan hoja ya msingi hapa si swala la kuchomwa....bali lile swala la kuchomwa milele....hapo kwenye umilele ndo panaleta utata hasa....! Mfano umefanya dhambi miaka 80 yaan uhai wako wote...vip uje uchomwe milele na milele daima?! Na daima?! Si swala lenye haki kwakweli!
Hata kipindi cha nabii Mussa kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona Mungu kama wewe unavyotaka.Tatzo mungu mwenyewe kajificha sijui anaogopa nn kujitokeza,,!'
Hapana sio kweli.Jannah au pepo kwa kiswahili ni sehemu yenye bustani yenye matunda aina mbalimballi na penye mito inayopitisha maji mazuri na matamu kuliko asali na meupe kuliko maziwa na yana harufu nzuri kuliko miski.Ukifikiria tu hio pepo ilivyo enyewe nikama inasound as boring place, mko kwenye park mnamuimbia bwanatu, tena mnakaa hapo milele, kweli mtu hatachoka apo
Hapana sio kweli,Mungu ana njia nyingi tu za mawasiliano kama vile kupitia revealition (ufunuo) ambayo hii wamejaaliwa mitume na wale wacha Mungu haswa.Mm naamini mwenyezimungu hana kurugenzi ya mawasiliano kama zilivyo ikulu zetu.
Kurugengi ya mawasiliano ya mwenyezimungu ni vitabu vyake tu.
Na wala mwenyezimungu hana msemaji wake hapa duniani kama tulivyo na Haji manara na wengine.
Mwenyezimungu anamiongozo tu ya jinsi gani anataka tuitumie ktk ulimwengu huu miongozo hiyo ni vitabu vyake alivyo tuteremshia yaani Quraan Taurati Injili nk.
Kwaharaka tu jibu lake ni kuwa atafaidika kwa kutimiza ahadi alizo tuahidi waja wema atawapa malipo mema na waovu atawalipa uwovu ikiwemo huo moto.
Mwenyezimungu atuepushe na ghadhabu zake na moto kesho akhera AMEEN;
Siku zote ukitaka kumjua Mungu usitumie akili ya kawaida ya kibinadamu pamoja na sayansi tunayosoma mashuleni kwa kuwa utaishia kuwa mpagani.Nashindwa kabisa kupata majibu ya maswali yangu kwa maana. Cha mwisho ninachojibiwa ni kua ninakufuru.. Eeeh Mungu kam kweli upo hebu nipe muongozo kwa mambo yanayonitatiza
Hamna atakayechomwaSalaaam..
Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.
Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.
Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..
SWALI:
je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??
Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..
Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??
Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..
Nawasilisha..karibuni
Hapana umemnukuu vibaya mwenyezi Mungu.Ujue zamani Mungu alikuwa anateremsha adhabu papo kwa hapo binadamu anapotenda matendo yasiyompendeza yeye(Mungu).Mwenyezi mungu alishasema hawezi kuiangamiza tena dunia kwa moto wala maji(gharika) sasa sijui hii ya moto umeipata wapi
Umeongea mengi tena vizuri kabisa,kwa maelezo yako ni kwamba moto wa milele haupo au sio??Soka Malaki 4 Biblia inasema waovu wataangamia na kuwa majivu na kisha dunia itaumbwa upya na watakatifu wataishi humo bila dhambi. Faida aipatayo Mungu ni kuteketeza dhambi, kwa kuwa shetani na wafuasi wake wameng'ang'ania dhambi licha ya wokovu wa bure kupitia kwa Yesu Kristo. Moto wa milele hautawaka siku zote ila huitwa wa milele kwa sababu utateketeza waovu pamoja na shetani na malaika zake watoweke milele. Kama una swali zaidi niulize kuhusu moto wa milele.
UMEJIBBU VIZURI SANA. SINA CHA KUONGEZA WALA KUPUNGUZA.NAKUBALIANA NA JIBULAKO 100%Anaejua ni Mwenyezi Mungu mwenyewe hiyo faida anayoipata kwa hiyo ni ngumu kwangu Mimi Kama mwanadamu kujua faida anazopata isipokuwa mi ninachojua ni kutii amri zake!!!!!
Unaweza mtafuta mwenyewe ukamuuliza labda atakuwa na majibu.