Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

smartware

New Member
Joined
Sep 19, 2024
Posts
1
Reaction score
20
Mimi kuna siku mgeni kaja kunitembelea, sina hata mia mbovu, ndani nina mchele na nje kuna matembele, nikaandaa mboga kwa ajili ya kupika na kubandika wali, basi bwana mgeni amefika tunasubiri msosi uive mara gesi ikaisha ndio kwanza maji yanaanza kukaukia , matembele yako kwenye maji, mgeni kaja na njaa anategemea kula kwangu alikotoka hakula, yani nilibaki sina cha kufanya, nikatafutiza kasoda kalibaki kwenye friji ndo nikampa akanywa.. akaondoka na njaa yake. Umasikini mbaya sana.
 
Unajiita masikini unafrji ndani Michele na pia unatumia gesi ndani na bustani ya matembele mkuu

Hujakutana na choka mbaya bongo sio poa
Huyu analeta utani , mimi nikiwa na gunia mbili za mkaa najiona kama Bill Gates

1000012625.jpg
 
Kuna kipindi na mimi nilifulia, wamekuja wageni sina kitu, ila nilikuwa nimefuga vikuku na mayai yalikuwepo, nikamwambia wife sina kitu fanya maarifa, akasema nifanye maarifa gani sasa, nikamwambia apige ugali na mayai, wakala wakaondoka, nashangaa siku nakutana na mmoja wao anasema bro umetapatia mpaka mayai yanaliwa ndani😂😂😂😂 nikabak nashangaa kumbe nimeyapatia
 
Back
Top Bottom