Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

Kama hujawahi pitia situation ambayo ukoo mzima unashindwa kuchanga laki tano hadi mgonjwa anapatiwa mitishamba kama betting, akipona inshallah, asipopona sawaa..

Au mgonjwa anaenda kubeba tofali ili alishe familia

Bhasi hauujui umaskini maana kuna watu baadhi niliowaona katika hizo situations . Aseee umaskini ni nusu kifo
 
Mimi kuna siku mgeni kaja kunitembelea, sina hata mia mbovu, ndani nina mchele na nje kuna matembele, nikaandaa mboga kwa ajili ya kupika na kubandika wali, basi bwana mgeni amefika tunasubiri msosi uive mara gesi ikaisha ndio kwanza maji yanaanza kukaukia , matembele yako kwenye maji, mgeni kaja na njaa anategemea kula kwangu alikotoka hakula, yani nilibaki sina cha kufanya, nikatafutiza kasoda kalibaki kwenye friji ndo nikampa akanywa.. akaondoka na njaa yake. Umasikini mbaya sana.
Una Mchele, kabustani ka matembele, jiko la geso, Huku kwetu wewe ni bilionea ndugu.
 
Back
Top Bottom