Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

👉Nakumbuka jirani alinionea huruma akaniita nikale nae
👉nishawahi kunywa U fresh ya mia na andazi la shilingi mia nikanywa maji mengi nikala
👉kunasiku nilinunua mchuzi wa pweza kama mboga nikaondoka nao geto nikapiga ugali usiku ikaisha
 
Kuna kipindi na mimi nilifulia, wamekuja wageni sina kitu, ila nilikuwa nimefuga vikuku na mayai yalikuwepo, nikamwambia wife sina kitu fanya maarifa, akasema nifanye maarifa gani sasa, nikamwambia apige ugali na mayai, wakala wakaondoka, nashangaa siku nakutana na mmoja wao anasema bro umetapatia mpaka mayai yanaliwa ndani😂😂😂😂 nikabak nashangaa kumbe nimeyapatia
Maisha yetu ya mjini mgeni ukimlisha kuku alafu wakienyeji utaonekana umeyapatia😁
 
Kama hujawahi pitia situation ambayo ukoo mzima unashindwa kuchanga laki tano hadi mgonjwa anapatiwa mitishamba kama betting, akipona inshallah, asipopona sawaa..

Au mgonjwa anaenda kubeba tofali ili alishe familia

Bhasi hauujui umaskini maana kuna watu baadhi niliowaona katika hizo situations . Aseee umaskini ni nusu kifo
Aisee Kuna watu wanapitia magumu sana mkuu

Mungu atusaidie tuvuke hizi changamoto
 
Mtu kupakataa kwao na kuwaambia washkaji zake eti amekuja kwa mganga leo nendeni tutaonana siku nyingine. Na mtu pale ni kwao kabisa.
Usikatae kwenu hata Kama Kuna dirisha moja Kama police post.
 
Mbona sioni wadada wakitoa confession zao za kupigwa na umaskini humu 🤔
 
Mimi kuna siku mgeni kaja kunitembelea, sina hata mia mbovu, ndani nina mchele na nje kuna matembele, nikaandaa mboga kwa ajili ya kupika na kubandika wali, basi bwana mgeni amefika tunasubiri msosi uive mara gesi ikaisha ndio kwanza maji yanaanza kukaukia , matembele yako kwenye maji, mgeni kaja na njaa anategemea kula kwangu alikotoka hakula, yani nilibaki sina cha kufanya, nikatafutiza kasoda kalibaki kwenye friji ndo nikampa akanywa.. akaondoka na njaa yake. Umasikini mbaya sana.
Huo haukuwa umasikini.Hukuwa mtu wa kujiongeza tu.
 
Back
Top Bottom