Ni fedheha gani ulipitia kisa umasikini?

πŸ‘‰Nakumbuka jirani alinionea huruma akaniita nikale nae
πŸ‘‰nishawahi kunywa U fresh ya mia na andazi la shilingi mia nikanywa maji mengi nikala
πŸ‘‰kunasiku nilinunua mchuzi wa pweza kama mboga nikaondoka nao geto nikapiga ugali usiku ikaisha
 
Maisha yetu ya mjini mgeni ukimlisha kuku alafu wakienyeji utaonekana umeyapatia😁
 
Aisee Kuna watu wanapitia magumu sana mkuu

Mungu atusaidie tuvuke hizi changamoto
 
Mtu kupakataa kwao na kuwaambia washkaji zake eti amekuja kwa mganga leo nendeni tutaonana siku nyingine. Na mtu pale ni kwao kabisa.
Usikatae kwenu hata Kama Kuna dirisha moja Kama police post.
 
Mbona sioni wadada wakitoa confession zao za kupigwa na umaskini humu πŸ€”
 
Huo haukuwa umasikini.Hukuwa mtu wa kujiongeza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…