Ni fedheha kuwa na watunga sheria wanaolalamikia ubovu wa sheria

Ni fedheha kuwa na watunga sheria wanaolalamikia ubovu wa sheria

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Kinachoendelea Dodoma sicho kinachopaswa kufanywa na wabunge watokanao na wananchi.

Wabunge wengi waliopewa nafasi yakusimama bungeni wamejikuta wanasifia, wamelalamika na kuomba.

Wengi wa wabunge hasa jinsia ya like wamejikita zaidi kusifia zaidi yakueleza wananchi wamewatuma nini.

Wabunge wanaume n baadhi ya wanawake wamejikita KULALAMIKA kuhusu sheria zinazosimamia kodi na vyombo vinavyosimamia sheria hizo.

Baadhi ya wabunge wakati wa hitimisho wamejikita kuomba kuliko kushauri nini kifanyike kuboresha.

Sehemu kubwa inayonitatiza ni pale unapoona wabunge wakilalamika kuhusu sheria. Mbunge wa Geita amekuwepo Bungeni Toka kipindi kilichopita na ameshiriki kutunga sheria za kodi, wakati sheria hizo ziznatungwa hakupinga bali aliunga mkono.

Shabiby yupo Bungeni muda mrefu, hakuna siku hoja imewahi fikishwa bungeni akaipinga kila Jambo kwake ni ndiyoooooo. Leo hii aina hii ya wabunge wanawezaja kutuaminisha sheria na mipango ya nchi nimibovu?

Ni mtizamo wa shemeji/wifi wa Mtwara.
 
Back
Top Bottom