Ni godoro gani zuri na imara kati ya QFL Dodoma na Tanform Arusha?

Vita supreme 5x6
Inchi 6?
Inchi 8?
Inchi 10?
Naomba kujua gharama wakuu
 
Magodoro standard ni Tanform tu.
Unless kama unatafuta taste mahsusi ndio unaweza kuangalia kushoto au kuliko
 
Niunge...
 
Godoro ni Vita supreme aisee hutajutia, bei imechangamka kidogo ila ni imara sana. Me nimenunua 2019 ila mpaka sasa ni kama jipya hakuna mahali lilipobonyea au kutengezeza wimbi hivi, limenyooka vile vile
Mkuu ulinunua la inch ngapi na bei gani supreme na je no laini ukilalia mkuu
 
Nambari 1 ni tanfoam
Aisee hili godoro lipewe heshima yake

Sio story hili godoro ninalo na nalitumia
 
Mkuu ulinunua la inch ngapi na bei gani supreme na je no laini ukilalia mkuu
Godoro lilikuwa na ukubwa wa futi tano kwa sita na kimo cha nchi kumi na mbili, bei sikumbuki vizuri ila ilikuwa inacheza kwenye 350k mpaka 400k. Godoro ni zuri sana kwa kweli sijuitii hela yangu kabisa, nikilinganisha na magodoro niliyowahi kulalia huko nyuma hili ni ze best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…