MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Mechi ya Simba na timu moja ya Liberia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha miaka ya tisini. Dua Said anaingia kipindi cha pili dakika za lala salama watu wakiwa wameanza kutoka wakijua ngoma droo. Dua akachukua mpira na kukimbia nao hadi kwenye kona ya bendera na kumsubiri beki. Beki kusogea Dua Said akawa anamtisha kama anataka kumpiga chenga then ghafla akaubetua mpira kwa kisigino ukapanda hadi kwenye mabega na kumkwepa beki huku akitoka mbio na alimkwepa beki mpira ukiwa kwenye bega then ukadondoka akaingia nao kwenye kumi na nane kwa speed kali. Akiwa ameingia kwenye kumi na nane akapiga shuti kali likatinga nyavuni moja kwa moja! Sisahau jinsi tulivyoshangilia lile goli! Tukiwa karibia na geti la kutoka nje ya uwanja!