Ni goli gani halitoki kwenye kumbukumbu zako??

Ni goli gani halitoki kwenye kumbukumbu zako??

Cr7 final na Chel 2008 Uefa mshikaji aliganda hewani sekunde kadhaa kabla ya kupiga kichwa
 
Unapoangalia mpira kuna matukio mengi yanatokea ila nadhan tukio linalosisimua zaid ni goli linapoingia, kuna magoli yanafungwa kimaajabu au kiustadi mkubwa hadi yanakuachia kumbukumbu isiyofutika..

Kwangu goli ambalo haliji kufutika ni goli la Didier Drogba aliwapiga Liverpool, hatari sana ile.. nyuma alikuwepo Carragher basi jamaa aligeuka moja kwa moja na shuti moja kali sana golini..Pepe Reina alibaki anazishangaa tu jinsi nyavu zinavyotikisika..

Tupe goli ambalo lipo kwenye kumbukumbu zako..
goli la mkono la NAPE NAUYE 2015 lililopigwa na Lubuva akipokea pasi safi kabisa toka kwa J.Makamba bila refa kuona kama alinawa mpira
 
Kuna goli alitufunga Jackson Mayanja kwenye fainali ya challenge kati ya Tanzania bara ( Kakakuona ) na Uganda . Alitandika mkwaju wa maana toka upande wa kushoto mwa uwanja kama mita 25 ukagonga besala ya juu ukagonga mstari na kuzama . Tukapoteza kombe . Nafikiri ilikuwa 1993 kama siyo 1992 pale Kirumba Mwanza .
 
Kuna goli alitufunga Jackson Mayanja kwenye fainali ya challenge kati ya Tanzania bara ( Kakakuona ) na Uganda . Alitandika mkwaju wa maana toka upande wa kushoto mwa uwanja kama mita 25 ukagonga besala ya juu ukagonga mstari na kuzama . Tukapoteza kombe . Nafikiri ilikuwa 1993 kama siyo 1992 pale Kirumba Mwanza .
Nakumbuka vizuri golini alikuwepo Josef Katuba ( R . I . P )
 
goli la papa bouba diop 2002,

senegal vs france


ilikuwa senegal ya uhakika aisee, ufaransa alikuwa bingwa mtetezi,, ila alilala moja bila
 
Mustafa Hadji, Kombe la Dunia.....
Ulipigwa mpira akautuliza kwa kifua akiwa karuka juu, kabla hajatua chini, akafyatua Kombora kimo cha Ng'ombe likaingia moja kwa moja kimiani.
 
Wengine tunayakumbuka tu ' Magoli ' ya ' hat-trick ' tunayowafunga Wake na Mademu zetu kila inapoitwa Siku mpya.
Kwa I'd za jf ni kawaida sana na kila siku watu wanahesabu ubingwa
Ila kwa maisha halisi ya mtanzania ni kizungumkuti
 
Goli la David Bergikamp dhidi ya New Castle united... Siwezi kuja kulisahau
 
Goli la pili la Cristiano Ronaldo, match kat ya PSG vs Madrid UCL hatua ya 16 mwaka 2017..dah Ronaldo ni nyoka kafunga hadi goli la goti aiseeeee
 
Dennia bergkamp vs newcastle
Dennis bergkamp vs argentina

Zidane vs bayern leverkusen
Drogba vs liverpool
Thierry henry vs man u
Roberto carlos vs france

Na mengine kede kede..
 
Back
Top Bottom