Ni hadaa na kujidanganya kwamba mahitaji muhimu sana ya wananchi wa Tanzania ni sheria za uchaguzi kubadilishwa

dah! gentleman,
una mambo mengi moyoni, pole aise 🐒
 
Au twende na hoja ya babu yetu mpya wa CCM kwamba - "wananchi wana njaa hawawezi kula katiba mpya".
ni muhimu sana kuzingatia mahitaji muhimu ya kila siku ya wananchi kuliko kumbwelambwela tu na kutapeli wananchi kwamba vyeo na madaraka ndio vipaumbele 🐒
 
Wajinga wakubwa nyie mmebanwa safari hii, mifumo ya hovyo ndiyo inatuletea watu majizi na majangili ya mali za umma, tuambie Rais alitoa wapi milioni 700 za kuwapa taifa star kwenye budget ipi?
relax na ufunguke taratibu gentleman,
ati unasemaje kuhusu hoja mahususi mezani?

kumbuka uchaguzi mkuu ni Oct mwaka huu 🐒
 
Acheni hizi mambo...sheria ziwe za haki..zisiwe za kupendelea chama kimoja....usijiamini mambo hubadilika
ili ziwe za haki ni Lazima wazo na fikra zako zikubaliwe right? Tukizingatie matakwa ya wananchi, si ndio?

Lazima kujiamini kwasababu taifa lipo mikononi salama mwa Dr Samia Suluhu Hassan, hakunaga kuogopa opgopa hapa 🐒
 
Ahaaa. Siyo sana siyo mimi peke yangu afadhali hata mimi sitilii maanani sana hali halisi kwani najua siwezi kubadilisha kitu.
kukata tamaa ni dhambi, na ni kitu mbaya sana,

pole pole mambo yanaweza kueleweka na kubadilika kabisa gentleman,

ni ngumu but keep it up 🐒
 
kukata tamaa ni dhambi, na ni kitu mbaya sana,

pole pole mambo yanaweza kueleweka na kubadilika kabisa gentleman,

ni ngumu but keep it up 🐒
Upo sahihi waoga Mungu amewachanganya na wazinzi na wachawi, tatizo ni moja watanzania bado hawajachoka na mateso waliyo nayo, usidhani mababu zetu walikuwa wapo tayari kupambana na wadharimu wakoloni ni kwasababu walifika kwenye pointi kuwa nisipopambana nitakumbwa na madhila nanikipambana aidha nitajinasua na haya madhila au nitakufa. Watanzania wote wakifikia hatua hiyo basi nchi itachangamka. Kwasababu kwa sasa nchi bado mbichi inalasilimali nyingi kwahiyo uwezo wanchi kuendelea kukopa bado mkubwa. Ila hizi lasilimali zikiisha tutaanza kulana si kwa sisi
 
Danganya wajinga wenzio.
Uongozi bora una nafasi kubwa sana katika suala zima la maendeleo.
Bila uongozi bora na imara suala la maendeleo ni ndoto.
Nchi haiwezi kuendelea kwa kuwa na viongozi wajinga, wababaishaji na wasio na maono.
Viongozi bora hutokana na michakato bora ya uchaguzi, ya wazi na huru.
 
Chawa kama huyo hawezi kukuelewa. Anawaza kwa kutumia tumbo hivyo hawezi kuwa na akili kamwe.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba
Tanzania inahitaji katiba mpya, kwa manufaa mapana ya Taifa letu.
Ila si kwa manufaa ya watu wachache.
Kuwepo kwa katiba mpya kuna watu wanaweza wakapata hasara lakini kama kuna manufaa ya Taifa hatuna budi kuunda katiba mpya sasa na haraka sana.
 
makini mfuasi wa kibaka was siasa, ndo bas tena ushatapeliwa 🤣
 
matapeli na vibaka wa siasa wanaweza kuwahadaa wachache miongoni mwenu kwamba hilo ndilo kipaumbele cha waTanzania kitu ambacho si kweli,

katiba ya Tanzania haitabadulishwa leo kesho ama keshokutwa, kipaumbele cha wananchi ni kupatiwa huduma bara za uhakika za maji, afya, elimu, kilimo n.k.

Poleni kuhangaishwa na matapeli katika siasa.
Kumbuka uchaguzi ni Oct mwaka huu 🐒
 
Chawa kama huyo hawezi kukuelewa. Anawaza kwa kutumia tumbo hivyo hawezi kuwa na akili kamwe.
aah pwagu na pwaguzi mnapeana moyo sio dah, mnapotoshana kindez kweli 🤣
 

Hivi wewe Blaahblaah unaongelea uchaguzi au uteuzi?

 
Ni mwendawazimu pekee atakayepinga HITAJI LA SHERIA MPYA za Uchaguzi na KATIBA MPYA.
Hizo changamoto ulizozitaja za maji, afya, elimu , umeme n.k hazitaisha kama tukiendelea na mfumo huu. Kwa sababu ya sheria mbovu za uchaguzi, tunapata wawakilishi wa wananchi, wanaoona umuhimu wa wapiga kura Uchaguzi unapokaribia na wakishinda huwa wanageuka mbogo dhidi ya Wananchi. Lakini pia, sheria tulizonazo kwa sasa, zinamfanya kiongozi wa kuchaguliwa, awe chawa wa kiongozi mkuu, kwani yeye ndiye mwenye hatima yake ya kisiasa.
Tunahitaji sheria mpya, sheria ambazo zitasimamia maamuzi ya wananchi waliowengi na si maamuzi ya kiongozi wa juu. Tukiweza hapo, tutapata viongozi Waadilifu, wenye hofu, wanaotambua nafasi ya Wapiga kura katika uongozi wao. Tukiwa na viongozi wa aina hiyo, hayo mengine uliyoyataja, ndipo yatatujia.

UKIACHA UBINAFSI, UKAWAZA KWA FAIDA YA WALIO WENGI, UTAKUBALIANA NA HAO WANAOHIMIZA MABADILIKO YA SHERIA. By the way, hata CCM, itatusaidia kuongoza vizuri.
 
Huna akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…