Ni hadaa na kujidanganya kwamba mahitaji muhimu sana ya wananchi wa Tanzania ni sheria za uchaguzi kubadilishwa

Ni hadaa na kujidanganya kwamba mahitaji muhimu sana ya wananchi wa Tanzania ni sheria za uchaguzi kubadilishwa

Kumekuepo na hadaa za wanasiasa matapeli kuhubiri mabadiliko ya sheria za uchaguzi nnje kabisa ya wakati wa mabadiliko ya sheria na katiba, kana kwamba hayo ndiyo mahitaji muhimu zaidi kwa wananchi wa Tanzania kuliko maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara, miundombinu, usafirishaji n.k

Lakini pia,
matapeli hao wa kisiasa nchini wanaendelea kuhadaa wananchi zaidi kwamba hitaji la waTanzania ni vyeo na mamlaka. Kwamba wananchi wanahitaji sana matapeli hao wa kisiasa wapate vyeo, kuliko mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Na ndio maana,
agenda kubwa za wanasiasa hao waliofilisika hoja zimekua ni kujadili umri wa makamu mwenyekiti wa CCM bara, na na ubaguzi dhidi ya ukanda anakotoka rais Dr. Samia Suluhu Hassan na jinsia yake, kana kwamba ukiwa kiongozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka upande wa Zanzibari Bara, ni kosa na ni anasa kubwa mno, huku wakijua wazi kabisa kua hakuna mtu anaweza kupata uongozi wa kitaifa Tanzania bila waZanzibari.

Ni vizuri kama wanasiasa kuibua hoja zenye mashiko kwa wakati sahihi na muafaka, kuliko kubwekabweka na kuwahadaa wananchi kwa vimisemo vitakavyowaathiri wenyewe na kuwakosesha fursa na haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi ambao wanawataka kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Kumbuka,
hata mtua aimbe, alie, acheke, acheze au abwekebweke namna gani, uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania upo pale pale, ni Oct.2025 :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
Kabla ya kuja na polojo, ungeeleza kwanza katiba ni nini, madhara na faida ya katiba kabla ya kuijadili kama tunaiitaji au hatuiitaji
 
Kabla ya kuja na polojo, ungeeleza kwanza katiba ni nini, madhara na faida ya katiba kabla ya kuijadili kama tunaiitaji au hatuiitaji
Gentleman,
andika tu uzi mahususi kwa mtindo huo huo wa swali na bila shaka wadau mbalimbali wa heshima humu jukwaani watakuelimisha juu ya hilo la katiba ni nini, na kwakweli utaongeza uelewa na ufahamu wako na wa wengine juu ya jambo hilo kwa kiasi kikubwa sana.

Na kwa wakati muafaka mwingine,
andika pia uzi mwingine kuhusu hayo mengine ambayo kwakweli ni muhimu na ni mambo ya maana sana kujadiliwa kwa kina na kwa kirefu zaidi.

kumbuka uchaguzi mkuu ni Oct.2025,
jihadhari na wasaka vyeo, madaraka, matapeli na vibaka wa siasa nyakati hizi za uchaguzi :NoGodNo:
 
Hoja zako na za Mzee Wasira ni sawa. Mnatoa hoja as if mnaishi mwezini!
ukweli ndivyo ulivyo,
ni mchungu halafu una kera sana.

hata hivyo kusema ukweli ni neema na baraka ya Mungu isiyochosha kabisa.
kumbuka uchaguzi mkuu ni oct.2025, jihadhari na wasaka vyeo, vibaka na matapeli wa kisiasa nyakati hizi:pedroP:
 
Kumekuepo na hadaa za wanasiasa matapeli kuhubiri mabadiliko ya sheria za uchaguzi nnje kabisa ya wakati wa mabadiliko ya sheria na katiba, kana kwamba hayo ndiyo mahitaji muhimu zaidi kwa wananchi wa Tanzania kuliko maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara, miundombinu, usafirishaji n.k

Lakini pia,
matapeli hao wa kisiasa nchini wanaendelea kuhadaa wananchi zaidi kwamba hitaji la waTanzania ni vyeo na mamlaka. Kwamba wananchi wanahitaji sana matapeli hao wa kisiasa wapate vyeo, kuliko mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Na ndio maana,
agenda kubwa za wanasiasa hao waliofilisika hoja zimekua ni kujadili umri wa makamu mwenyekiti wa CCM bara, na na ubaguzi dhidi ya ukanda anakotoka rais Dr. Samia Suluhu Hassan na jinsia yake, kana kwamba ukiwa kiongozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka upande wa Zanzibari Bara, ni kosa na ni anasa kubwa mno, huku wakijua wazi kabisa kua hakuna mtu anaweza kupata uongozi wa kitaifa Tanzania bila waZanzibari.

Ni vizuri kama wanasiasa kuibua hoja zenye mashiko kwa wakati sahihi na muafaka, kuliko kubwekabweka na kuwahadaa wananchi kwa vimisemo vitakavyowaathiri wenyewe na kuwakosesha fursa na haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi ambao wanawataka kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Kumbuka,
hata mtua aimbe, alie, acheke, acheze au abwekebweke namna gani, uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania upo pale pale, ni Oct.2025 :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
Ccm tz imetualibia vipaji, chawa wataenda kufa midomo wazi
 
Hawa jamaa ni vibaraka wa vikundi fulani vilivyoko nchi za ulaya hususani Ubelgiji na Ujerumani. Lengo lao ni kuleta machafuko nchini kwetu kama yale yanayoendelea huko DRC ili wapore utajiri wa rasilimali wa nchi yetu. Hawa jamaa hawana tofauti na lile kundi la M23 ambalo ni kibaraka wa nchi ya Rwanda.

Si watu wa kubezwa kwani wanasema wazi wazi kuwa wamejipanga kuzuia kwa nguvu huu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wanasema wameamua kukinukisha mwaka huu. Hivyo inawezekana wanaandaa kikosi kama kile cha M23 kufanikisha azima yao hiyo. Kikosi tunachoweza kukiita M25. Hivyo wananchi na majeshi yetu inapaswa kufuatilia kwa kina mienendo ya vibaraka hawa na kuwa tayari kupambana nao wakati wo wote kuzia hicho wanachopanga kufanya. Ibaki no reform no election imaanishe no reform no chadema = no reform the end of chadema.
 
ASKOFU DKT. BAGONZA: KWA MUJIBU WA KIAPO CHA URAIS NA FALSAFA YA 4R YA RAIS SAMIA SASA RAIS SAMIA ANAO WAJIBU WA KIKATIBA KUIKARABATI MIFUMO INAYOTUMIKA KUFANIKISHA UHALIFU WA KISIASA KATIKA CHAGUZI AMBAPO UHALIFU HUO UNAOTEKELEZWA NA WANASIASA MATAPELI WANAOFUATA NYAYO ZA HAYATI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Screenshot_20250216_195403_TikTok.jpg

Je, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, na hasa kwa mujibu wa kiapo cha urais wake, Rais Samia Suluhu Hassan anao wajibu wa kikatiba kujitenga na mifumo inayotumika kufanikisha uhalifu wa kisiasa katika chaguzi, uhalifu huo ukiwa unatekelezwa na wanasiasa matapeli wanaofuata nyayo za hayati Rais John Pombe Magufuli?

Ndiyo. Ni kweli kwamba Rais Samia anatoka chama kile kile kilichokuwa kinaongozwa na hayati Rais John Pombe Magufuli.

Ndiyo. Hakuna utata kwamba Rais Samia alikuwa Makamu wa Rais wa hayati Rais John Pombe Magufuli.

Ndiyo. Ni wazi kwamba Rais Samia ni miongoni mwa wanufaika wakuu wa uhalifu wa kisiasa uliofanyika katika chaguzi ukiwa unatekelezwa na wanasiasa matapeli waliokuwa wanafuata maagizo ya hayati Rais John Pombe Magufuli.

Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan HALAZIMIKI kurithi misimamo haramu ya JPM kuhusu chaguzi zetu na HALAZIMIKI kuendeleza mahusiano yaliyogubikwa na uhasama kati yake na vyama vya upinzani.

Misimamo hiyo ya JPM ilivunja katiba ya nchi aliyokuwa ameapa kuilinda, ilivunja haki za binadamu na iliifunga nchi kiasi cha kututenganisha na dunia ya wanademokrasia.

Ndiyo maana, mara tu baada ya kiapo chake kama Rais mpya wa Tanzania, Rais Samia alifanya maboresho kwa kiasi fulani.

Mfano, aliamua kuondoa mazuio ya mikutano yaliyokuwa yanavunja katiba, alitamka hadharani kufungua nchi na alizindua falsafa ya 4R.

Lengo lake lilikuwa na huenda bado ni kuliepusha taifa na sifa mbaya ya kuvunja haki za binadamu na kukiuka kanuni za kikatiba kuhusu utawala bora.

Kuhusu chaguzi zetu, yeye binafsi na pia wasaidizi wake walitamka hadharani kuwa yaliyotokea 2019 na 2020 hayapaswi kujitokeza tena.

Niliwahi kueleza kuwa mimi “ninaogopa” kuamini ahadi hizo kwa kuwa hazina misingi ya kisheria na kikatiba.

Lakini kwa kuwa zilitolewa na viongozi walioapa kwa kutumia misahafu kuilinda katiba ya nchi niliamua kuishi kwa imani.

Imani yangu hii ndio inanifanya kuuliza na kujaribu kujibu baadhi ya maswali kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi. Maswali na majibu yangu yanafuata.

Swali 01: Kwa Nini Tunapaswa Kukubaliana Kwamba Uchaguzi Ufanyike Baada ya Marekebisho ya Maeneo Muhimu ya Katiba ambayo yatakuwa ni “Minimum Reforms”?

Kufuatia kuapishwa kuwa Rais baada ya uchaguzi wa 2015, JPM alitoa amri ya mdomo ya kukataza shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani.

Amri hiyo ilikiuka Katiba ya JMT hususan Ibara za 12 hadi 21.

Kwa bahati mbaya watu na taasisi waliotegemewa kupinga au hata kukemea ukiukwaji huo wa Katiba ya JMT, walikaa kimya kana kwamba jambo hilo haliwahusu.

Wafuatao walipaswa angalau KUNUNA kwa sababu ya ukiukwaji huo:
  1. CCM na UONGOZI WA JUMUIYA ZAKE. Kwa kuwa CCM haina baraza la Wazee, wale wazee wachache waliofunua midomo yao na kunong'ona, JPM aliwatisha kuwa wakome "kuwashwa washwa"
  2. Bunge la JMT lenye mamlaka ya kuishauri na kuisimamia Serikali nalo liliufyata na kuanza kuimba masifu na mapambio kwa JPM
  3. Mwanasheria mkuu wa Serikali
  4. .Msajili wa Vyama vya siasa.
  5. Viongozi wa Asasi za Kiraia zinazohusika na utetezi wa HAKI ZA BINADAMU
  6. Viongozi wa Makanisa yanayowafundisha kwamba "MUNGU WETU NI MUNGU WA HAKI" na kwamba "MAMLAKA YOTE HUTOKA KWA MUNGU" huyo.
  7. Viongozi wa Misikiti wanaomwakilisha Mungu anayetaka HAKI SAWA KWA WOTE.
  8. Jumuiya ya Kimataifa inayohimiza serikali za dunia kuheshimu tunu na kanuni za demokrasia na utawala bora.
  9. Raia mmoja mmoja mwenye jukumu la kulinda ukamilifu wa Katiba ya nchi kwa kupinga utawala holela wenye sura ya uongozi wa kiimla.
Pamoja na hayo Mtu pekee aliyejitokeza kupinga ukiukwaji huo wa haki za Kilatiba kwa njia ya UJASIRI na UWAZI ni mmoja tu.

Yaani TUNDU ANTIPAS LISSU ambaye alikuwa Rais wa TLS wakati huo.

Matokeo yake alishambuliwa kwa risasi nyingi.

Ni Rais Samia pekee aliyejitoa mhanga akiwa Makamu wa Rais aliyefika Nairobi kumjulia hali Tundu Lisu.

Ilipofika 2019, Rais JPM alitoa tamko jingine la kuvunja KATIBA pale alipowaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini (DED) kutowatangaza wapinzani kama Washindi kwenye chaguzi zote za Serikali ukiwemo Uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kwa uwazi kabisa amri hiyo ya JPM ilikiuka matakwa ya Katiba ya Tanzania inayosema kuwa Tanzania ni dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia.

Kwa mujibu wa Katiba hii mamlaka yote ya kiutawala yanapaswa kutoka kwa umma wa wapiga kura, kwa njia ya uvhaguzi ulio huru, wazi na shindanishi, kama ilivyoandikwa kwenye ibara ya 8 ya Katiba(1977).

Na, kama ilivyokuwa kwa amri ya awali ya katazo la shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani, WADAU WOTE WALIOPASWA KUIPINGA UKIUKWAJI WA KATIBA YANNCHI walinyamaza kimya.

Baada ya kifo cha JPM, Rais Samia Suluhu Hassan, hatimaye alitengua katazo la shughuli za mikutano ya kisiasa nchini

Lakini Rais Samia, BILA SHAKA KWA MAKUSUDI hakusema kitu juu ya Amri ya pili ya mtangulizi wake, ya kuzuia washindi wa upinzani kutangazwa kama washindi halali pale wanaposhinda.

Matokeo yake uliotegemewa kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 umechukua sura ile ile ya uchaguzi wa 2019. Yaani:
  1. Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  2. Kuwaengua wagombea wao wengi,
  3. Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani na
  4. Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Hili ni donda ndugu linalochafua uhalali (“legitimacy”) wa viongozi wetu wa vitongoji waliopatikana kutokana na mchakato huo haramu, maana malengo halali ya kuunda serikali hayapaswi kuhalalisha mbinu haramu za uchaguzi.

Kama ilivyokuwa mwaka 2019 na mwaka 2020, mchakato wote wa Uchaguzi wa 2024 umekiuka Katiba ya JMT, sheria zote husika na misingi ya kuendesha Uchaguzi kwa jamii inayojitambulisha kama Taifa ambalo ni Jamhuri ya Kidemokrasia na inayopaswa kujiheshimu kulingana na utambulisho huo wa Kikatiba.

PIA, MILA ZETU ZA KIAFRIKA ZINASISITIZA KWAMBA KUNA KIWANGO CHA CHINI KABISA CHA MTU AU JAMII KATIKA SUALA LA KUJIHESHIMU, ISIPOKUWA KAMA MTU NI PUNGUANI.

Swali 02: Kama tukishindwa kukubaliana kuhusu umuhimu na ulazima wa mageuzi ya kimfumo kabla ya uchaguzi wa 2025 na hivyo tukalazimishwa kwenda kwenye uchaguzi wa 2025 kabla ya marekebisho ya kimfumo kufanyika kutatokea nini?

Kwa maoni yangu, kama tukisoma alama za nyakati kwa umakini tutakubaliana kuwa endapo tutaenda kwenye uchaguzi wa 2025 kabla ya marekebisho ya kimfumo basi uhalifu uliofanyika kwenye chaguzi za 2019, 2020 na 2024 utafanyika tena.

Hatimaye Raia wa Tanzania wataendelea kuishi kama watumwa ndani ya nchi yao kwa sababu ya kutawaliwa na serikali haramu kama ilivyokuwa enzi za ukoloni wa Wazungu na zama za utumwa wa Waarabu.

Nitaeleza kwa nini natabiri hivyo na kwa tunapswa kuepuka haya ninayoyatabiri.

Kwanza, Rais Samia bado hajatengua amri ya JPM ya KUWAKATAZA ma DED kuwatangaza WAPINZANI kama washindi wa Ubunge na Udiwani.

Pili, Tume ya Uchaguzi iliyobatizwa jina la HURU bado ni ileile kuanzia uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu wake na wajumbe wengine.

Ni hivyo hivyo kwa Mkurugenzi na Sekretarieti ya Tume.

Tatu, watendaji wengi walioratibu na kutekeleza hujuma za uchaguzi wa 2019, 2020 na 2024 bado wako ofisini wakuwa na uzoefu wao wa kihalifu.

Na jambo baya zaidi ni kwamba, uchaguzi wa 2019, 2020 na 2024 UMESABABISHA MAJERAHA MAKUBWA KWA DHAMIRI ZA WATANZANIA WOTE walioshiriki kuuandaa, kuusimamia na kutangaza Matokeo yake.

Waasisi wa Taifa letu na hususan Mwalimu J.K Nyerere walifanya kazi kubwa ya kutufanya wamoja.

TUNAISHI, TUNAFANYA SHUGHULI ZOOTE ZA KISIASA, KIJAMII, KIDINI bila kujali makabila yetu, dini zetu, rangi zetu, hali ya maisha nk.

Kwa sababu hiyo hakuna siri miongoni mwa Watanzania kuhusu uhalifu wa kiuchaguzi unaofanywa na serikali ya CCM mwaka hadi mwaka.

Hujuma zote zilizofanyika kwenye chaguzi zetu zinajulikana na zimesamba kabisa miongoni mwa Watanzania.

Nne, uhalifu wa kisiasa unaofanyika kupitia uchaguzi utaendelea kujenga ujasiri wa kihalifu katika mioyo ya watu kwenye sekta baki za maisha ya kila siku.

Hakuna ubishi kwamba kutokana na chaguzi hizo haramu CCM na Serikali yake wamefanikiwa kujenga jamii ya mamilioni ya watu wengi wenye dhamiri zilizokufa kimaadili.

Wengi wao wanaamini kuwa malengo halali ya kisiasa yanaweza kufukuziwa kwa kutumia mbinu zozote bila kujali kama ni halali, nusu halali au haramu. Hii ni itikadi hatari ya Umachiaveli.

Watu hawa sasa wamegeuka matapeli wa siasa kutokana na tabia yao isiyokoma ya kufanya UDANGANYIFU wa wazi kwenye hatua zote za mchakato wa uchaguzi utafikuri ni wapagani.

Hawa ni pamoja na baadhi ya:

  • Wakuu wa mikoa--Ma RC,
  • Makatibu Tawala wa Mikoa--Ma-RAS,
  • Wakuu wa Wilaya--Ma-DC,
  • Makatibu Tawala wa Wilaya--ma-DAS,
  • Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya--Ma-DED,
  • Maafisa Watendaji wa Kata --Ma-WEO
  • Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama,
  • Mahakimu na majaji wanaoshughulikia kesi za uchaguzi
  • Wasimamizi wa uchaguzi vituoni ambao kwa sasa ni watumishi wa Umma kama vile Walimu.
  • Na baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa wenye hulka ya kuganga njaa.
Tukiondoa wahusika ambao ni makada wa CCM, watu waliobaki wanatii amri ili kutunza ajira zao.

Si ajabu hata mimi Askofu Bagonza ningefanya utii kama wao labda kwa sababu ya nidhamu ya woga.

Lakini sasa matokeo yake sasa tumegeuka Taifa la WEZI, Taifa la WAONGO, Taifa la WALAGHAI, Taifa la MATAPELI, Taifa la WANAOGHUSH matokeo nk.

Watu ni waongo, mifumo ya Tehama inachezewa, na taifa linabomolewa na watu wanaoitwa wataalam wa TEHAMA (ICT).

Tukiendekeza wizi na ulaghai kwenye chaguzi zetu, tutazidi kubomoa JINA na HESHIMA YA NCHI YETU ILIYOJENGWA KWA JUHUDI, MAARIFA NA KUJITOA SANA KWA WAASISI WETU. SASA TUNAKARIBIA KUIPIKU NCHI YA NIGERIA.

Mambo haya yanaathiri utambulisho wa taifa letu. Baadhi yetu tumefaidi matunda ya jina zuri la taifa letu lililojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wa taifa letu.

Niliwasikia kwa masikio yangu baadhi ya viongozi wa sasa wa serikali yetu wakijiapiza kuwa “yaliyojitokeza katika awamu ya tano, yasiruhusiwe tena”.

Rais Samia ana historia ya kujenga na tayari anayo. Ana Legacy ya kuacha, si kubebana na ya awamu ya tano.

Lakini pia CCM bado inao uwezo mkubwa wa kushinda chaguzi bila ulazima wa “kuonekana” inaiba kura.

Naogopa kuamini kuwa sifa ya mwana CCM ni kuiba kura! Inatisha.

Si dalili njema kuona vijana wengi wameanza kushabikia uongozi wa kibabe (Trump na Traore) huku wakibeza demokrasia.

Na wengine wengi wanamkumbuka JPM na kutamani arudi.

JPM alikuwa na mazuri yake lakini si katika eneo hili la demokrasia na utawala bora.

Swali 03: Kusudi tuweze kuepuka madhara haya tufanye nini ili tuweze kulirejesha Taifa la Tanzania kwenye misingi ya dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia katika mtazamo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kama ilivyoandikwa kwenye Katiba yetu?

Binafsi nawasihi Watanzania wote tuamke. Sote tuingie ulingoni, tupaze sauti. Mageuzi ya kimfumo niliyoyaongelea hapo juu ni ajenda yetu sote.

Tusiruhusu madai ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kumilikiwa na chama chochote cha siasa, azaki yoyote, au kikundi kingine chochote cha kisekta.

Hii ni kazi ya watu wote wenye mapenzi mema na taifa letu.

Hivyo namwalika kila mmoja na kila kikundi katika nafasi yake kuandaa "TAMKO LA KUUNGA MKONO MAGEUZI YA KIMFUMO KABLA YA UCHAGUZI MKUU WA 2025" na kulitangaza tamko hilo kwa umma ili kujenga hamasa na kulipa uzito suala hili.

Mie tayari nimetimiza wajibu wangu wa kutoa "tamko" kupitia andiko hiki.

Nawe tafakari na chukua hatua leo. Liwezekanalo leo lisingoje kesho.

ASEMAVYO ASKOFU DKT. BAGONZA: RAIS SAMIA HALAZIMIKI KUFUATA NJIA YA JPM KUHUSU CHAGUZI ZETU.

Ndiyo. Rais Samia anatoka chama kile kile alichoongoza hayati JPM.

Ndiyo. Rais Samia alikuwa Makamu wa JPM, lakini HALAZIMIKI kurithi misimamo ya JPM kuhusu chaguzi zetu na mahusiano mabaya na vyama vya upinzani.

Misimamo hiyo, ilivunja katiba, ilivunja haki za binadamu na iliifunga nchi.

Ndiyo maana Rais Samia aliamua kuondoa mazuio yaliyovunja katiba, akatamka hadharani kufungua nchi na kuzindua falsafa ya 4R ili kuliepusha taifa na sifa mbaya ya kuvunja haki za binadamu na kukosa utawala bora.

Kuhusu chaguzi zetu, yeye binafsi na pia wasaidizi wake walitamka hadharani kuwa yaliyotokea 2019 na 2020 hayatajitokeza tena.

Niliwahi kueleza kuwa mimi “ninaogopa” kuamini ahadi hizo kwa kuwa hazina misingi ya kisheria na kikatiba. Lakini kwa kuwa zilitolewa na viongozi walioapa kwa misahafu, niliamua kuishi kwa imani.

Swali: KWA NINI TUSIKUBALI UCHAGUZI KUFANYIKA KABLA YA MAREKEBISHO YA MAENEO MUHIMU YA KATIBA (Minimum Reforms).

Kufuatia kuapishwa kuwa Rais baada ya uchaguzi wa 2015, JPM alitoa amri ya mdomo ya kukataza shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani.

Amri hiyo ilikiuka Katiba ya JMT hususan Ibara za 12 hadi 21.

Kwa bahati mbaya watu na taasisi waliotegemewa kupinga au hata kukemea ukiukwaji huo wa Katiba ya JMT, walikaa kimya kana kwamba jambo hilo haliwahusu.

Wafuatao walipaswa angalau KUNUNA kwa ukiukwaji huo:

1. CCM na UONGOZI WA JUMUIYA ZAKE.

Kwa kuwa CCM haina baraza la Wazee, wale wazee wachache waliofunua midomo yao na kunong'ona, JPM aliwatisha kuwa wakome "kuwashwa washwa".

2.Bunge la JMT lenye mamlaka ya kuishauri na kuisimamia Serikali nalo liliufyata na kuanza kuimba masifu na mapambio kwa JPM.

3.Mwanasheria mkuu wa Serikali.

4.Msajili wa Vyama vya siasa.

5.Viongozi wa Asasi mbali mbali zinazohusika na utetezi wa HAKI
ZA BINADAMU.

Mtu pekee aliyejitokeza kupinga ukiukwaji huo wa Katiba kwa njia ya UJASIRI na UWAZI ni TUNDU ANTIPAS LISSU ambaye alikuwa Rais wa TLS wakati huo.

Matokeo yake alishambuliwa kwa risasi nyingi. Ni Rais Samia pekee aliyejitoa mhanga akiwa Makamu wa Rais aliyefika Nairobi kumjulia hali Tundu Lisu.

Ilipofika 2019, JPM alitoa tamko jingine la kuvunja KATIBA pale alipowaagiza Wakurugenzi (DED) kutowatangaza wapinzani kama Washindi kwenye chaguzi za Serikali za mitaa na mwaka uliofuata,2020 uchaguzi mkuu.

Amri hiyo ya JPM ilikiuka Katiba kwa uwazi kabisa.

Na, kama ilivyokuwa kwa amri ya awali ya katazo la shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani, WOOTE WALIOPASWA KUIPINGA walinyamaza kimya.

Baada ya kifo cha JPM, Rais SSH, hatimaye alitengua katazo la shughuli za kisiasa lakini BILA SHAKA KWA MAKUSUDI hakusema kitu juu ya Amri ya pili ya mtangulizi wake.

Matokeo yake uliotegemewa kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 umechukua sura ile ile ya uchaguzi wa 2019. NI KUTOANDIKISHA WAPIGA KURA KWENYE NGOME ZA WAPINZANI, KUWAENGUA WAGOMBEA WAO WENGI, KUTOWARUHUSU MAWAKALA WA VYAMA VYA UPINZANI na KUTOWATANGAZA WAPINZANI hata pale walipoonekana kushinda. Hili ni donda ndugu linalochafua “Legitimacy” ya viongozi wetu wa vitongoji.

Kama ilivyokuwa 2019 na 2020, mchakato wote wa Uchaguzi wa 2024 umekiuka Katiba ya JMT, sheria zoote husika na MISINGI ya kuendesha Uchaguzi KWA JAMII INAYOJIESHIMU.

MILA ZETU ZA KIAFRIKA ZINASISITIZA KWAMBA KUNA KIWANGO CHA CHINI KABISA CHA MTU AU JAMII KUJIHESHIMU, ISIPOKUWA KAMA MTU NI PUNGUANI.

Swali: NINI KITATOKEA ENDAPO TUTAENDA KWENYE UCHAGUZI WA 2025 BILA MAREKEBISHO?

Kwanza,Rais SSH bado hajatengua amri ya JPM ya KUWAKATAZA ma DED kuwatangaza WAPINZANI kama washindi wa Ubunge na Udiwani.

Pili,Tume ya Uchaguzi iliyobatizwa jina la HURU bado ni ileile kuanzia uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu wake na wajumbe wengine. Ni hivyo hivyo kwa Mkurugenzi na Sekretarieti ya Tume.

Tatu, na jambo baya zaidi ni kwamba uchaguzi wa 2019,2020 na 2024 UMESABABISHA MAJERAHA MAKUBWA KWA DHAMIRI ZA WATANZANIA WOTE walioshiriki kuuandaa, kuusimamia na kutangaza Matokeo yake.

Waasisi wa Taifa letu na hususan Mwl.J.K Nyerere walifanya kazi kubwa ya kutufanya wamoja.

TUNAISHI, TUNAFANYA SHUGHULI ZOOTE ZA KISIASA,KIJAMII,KIDINI bila kujali Makabila yetu,dini zetu,rangi zetu, hali ya maisha nk. Kwa sababu hiyo hakuna siri miongoni mwa Watanzania.

Hujuma zoote zilizofanyika kwenye chaguzi zetu zinajulikana na kusambaa haraka miongoni mwa Watanzania.

Kutokana na chaguzi hizo CCM na Serikali yake imefanikiwa kujenga jamii ya mamilioni ya watu ambao dhamiri zao zimekufa;

1. Wanafanya UDANGANYIFU kwenye hatua zote za mchakato wa uchaguzi.
Hawa ni. Ma RC, MaRAS, Ma DC, ma DAS, MaDED, WATENDAJI WA KATA, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, Wasimamizi ambao ni watumishi wengine wa Umma kama Walimu nk.

Ukiondoa walio makada, waliobaki wanatii amri ili kutunza ajira zao (si ajabu hata mimi ningefanya labda!)

Matokeo yake tumegeuka Taifa la WEZI, WAONGO, WALAGHAI, MATAPELI, WANAOGHUSHI nk. Watu ni waongo, mifumo ya Tehama inachezewa na taifa linafilisiwa na wanaoitwa wataalam wa IT (TEHAMA).

Tukiendekeza wizi na ulaghai kwenye chaguzi zetu, tutazidi kubomoa JINA na HESHIMA YA NCHI YETU ILIYOJENGWA KWA JUHUDI, MAARIFA NA KUJITOA SANA KWA WAASISI WETU. TUNAIKARIBIA NIGERIA.

Mambo haya yanaathiri utambulisho wa taifa letu. Baadhi yetu tumefaidi matunda ya jina zuri la taifa letu lililojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wa taifa letu.

Niliwasikia kwa masikio yangu baadhi ya viongozi wa sasa wa serikali yetu wakijiapiza kuwa “yakiyojitokeza katika awamu ya tano, yasiruhusiwe tena”.

Rais Samia ana historia ya kujenga na tayari anayo. Ana Legacy ya kuacha, si kubebana na ya awamu ya tano. CCM bado inao uwezo mkubwa wa kushinda chaguzi bila ulazima wa “kuonekana” inaiba kura. Naogopa kuamini kuwa sifa ya mwana CCM ni kuiba kura! Inatisha.

Si dalili njema kuona vijana wengi wameanza kushabikia uongozi wa kibabe (Trump na Traore) huku wakibeza demokrasia. Na wengine wengi wanamkumbuka JPM na kutamani arudi.

JPM alikuwa na mazuri yake lakini si katika eneo hili la demokrasia na utawala bora. Tuamke. Madai ya mabadiliko ya mfumo wa chaguzi zetu yasimilikiwe na chama chochote bali watu wote wenye mapenzi mema na taifa letu.
huyu askofu namuheshimu sana,

nakumbuka alilalamika sana japo kwa unafiki wa mafumbo mitandaoni kuhusu uchaguzi wa mkuu wa kanisa la KKKT, mpaka akasusa na kukimbia ukumbi wa uchaguzi, baada ya kuona hata hakupendekezwa na waliodai anafaa kua mkuu wa kanisa hilo kabla.

ingekua amechochea walau mageuzi kidogo tu ya sheria na katiba walau ya kanisa lake kuhusu chaguzi ningemtilia maanani kidogo, lakini vinginevyo ni sawa na hawa vibaka na matapeli wa siasa za Tanzania tu,

ni muhimu akapuuzwa pia :NoGodNo:
 
Samahani. Nataka kuona majibu yako dhidi ya hoja za Dr. Bagonza, with counter evidence provided formally.

Usijadili haiba wala dosari binafsi za mleta hoja.

Unafanya kosa la kimantiki liitwalo ARGUMENTUM AD HOMINEM.

You are attacking the arguer instead of addressing the argument.

Hata wewe unazo dosari zako binafsi.

Mfano kuna demu mmoja anasemaga kuwa wewe ni "shoka moja mbuyu chini" na hujawahi kukanusha.

Lakini tuhuma hizi hata kama ni za kweli hazina umuhimu wala ulazima ktk jukwaa hili wala kwenye hoja yako ya leo.

Kuna watumishi wa umma ni wala rushwa lakini wakisema kula rushwa ni kosa la jinai wanakuwa wamesema ukweli wenye manufaa.

Kwa mfano Rais Samia alisema kuwa kwa maoni yake kitendo cha MTUMISHI WA UMMA KULA RUSHWA KATIKA MIPAKA YA UREFU WA KAMBA YAKE NI HALALI.

Lakini bado Rais Samia huyu huyu akisema kuwa kitendo cha kula rushwa ni jambo haramu kila mahali, kila wakati na kwankila mhusika anakuwa amesema ukweli tunaopaswa kuukubali mara moja.

Hivyo epuka hoja zenye upindifu wa kimantiki unaokufanya uonekane semi-iliterate proper

Yaani epuka logical fallacies. Hazifai katika mchakato wa kuchuja ukweli dhidi ya uwongo unaoendelea hapa.

Usipozingatia mwongozo huu kuhusu mbinu sanifu za kufanya tafakari (standard principles of sound reasoning) utanipa sababu ya kuhitimisha kwamba kichwani mwako kuna mashudu ya ng'ombe kama sio kinyesi kama picha inavyoonyesha hapa chini.

1739722359761.png

Kinachoweza kuonekana kwenye kichwa cha Tlaatlaah kwa mujibu wa picha ya X-ray itakayopigwa baadaye
 
Hawa jamaa ni vibaraka wa vikundi fulani vilivyoko nchi za ulaya hususani Ubelgiji na Ujerumani. Lengo lao ni kuleta machafuko nchini kwetu kama yale yanayoendelea huko DRC ili wapore utajiri wa rasilimali wa nchi yetu. Hawa jamaa hawana tofauti na lile kundi la M23 ambalo ni kibaraka wa nchi ya Rwanda.

Si watu wa kubezwa kwani wanasema wazi wazi kuwa wamejipanga kuzuia kwa nguvu huu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wanasema wameamua kukinukisha mwaka huu. Hivyo inawezekana wanaandaa kikosi kama kile cha M23 kufanikisha azima yao hiyo. Kikosi tunachoweza kukiita M25. Hivyo wananchi na majeshi yetu inapaswa kufuatilia kwa kina mienendo ya vibaraka hawa na kuwa tayari kupambana nao wakati wo wote kuzia hicho wanachopanga kufanya. Ibaki no reform no election imaanishe no reform no chadema = no reform the end of chadema.
una hoja ya maana sana gentleman,

kanuni mojawapo muhimu sana kwenye siasa ni kwamba kamwe usimua underrate opponent wako hata kama hana nguvu kabisa kisiasa mnapoelekea kwenye uchaguzi.

nikuhakikishie tu,
taasisi za kisiasa nchini pamoja na vyombo husika vya kiusalama nchini viko chonjo mbaya sana kufuatilia kila mipango na kila hatua ya kila mwanasiasa hususani hawa vibaka na matapeli wa siasa nchini.

no threats at all kutoka kwa kibaraka yeyote wa mabwenyenye ya magharibi anweza kujipenyeza na kujaribu kuharibu umoja, amani na utangmano miongoni mwa waTanzania.

binafsi,
ushauri wangu kwa waTanzania ni kwamba,
wananchi wajiepushe na wimbi la kutapeliwa pesa na ombaomba wa kisiasa kirahihisi na wanansiasa wasio na maono dhidi ya mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Taifa letu lipo salama mno chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan, rais na kipenzi cha waTanzania wote.

bigup kwa comment mujarabu :ClapHD: :KasugaYeah:
 
Samahani. Natamani kuona majibu yako dhidi ya hoja zake, with counter evidence provided. Usijadili dosari za mleta hoja. Hata wewe unazo dosari zako. Mfano kuna demu mmoja anasemaga kuwa wewe ni "shoka moja mbuyu chini". Lakini tuhuma hizi hata kama ni za kweli hazina umuhimu wala ulazima ktk jukwaa hili wala kwenye hoja yako ya lei. Kuna watu ni wezi lakini wakisema wizi ni kosa la jinai wanakuwa sahihi. Epuka hoja zenye upindifu wa kimantiki. Yaani logical fallacies.
my lady,
ni kupoteza muda kujadili hoja ya mtu mwenye dosari na kasoro lukuki, anazolalamikia kwa uchungu sana kwenye taasisi yake na hajazifanyia kazi, eti halafu anakuja kuibua dosari na kasoro kwenye taasisi nyingine,

nadhani huko kutakua ni kutapeliwa kifikra sasa, na kwahivyo hakuna haja ya kubabaika na hoja za askofu tapeli kisiasa:pulpTRAVOLTA:
 
mi nadhani bado ipo changamoto kuhusu uelewa na ufahamu wa wanasiasa juu ya nini hasa mahitaji ya wananchi.

naona ni mwendo wa kuzungumzia mahitaji ya viongozi tu ya vyeo na madaraka.

kwanini matapeli na vibaka wa kisiasa hawapendi kuzungumza kuhusu mahitaji ya kila siku ya wananchi, mathalani maji, elimu na afya?

au mambo hayo yamefanyika vizuri zaidi na kuwatosheleza wananchi kiasi kwamba waone sheria za uchaguzi ndio muhimu zaidi ya mahitaji mengine ya kila siku? :DisGonBGud:
Hayo maji elimu na afya viko wapi?mara ngapi wananchi wanavilalamikia hawavipati?
 
my lady,
ni kupoteza muda kujadili hoja ya mtu mwenye dosari na kasoro lukuki, anazolalamikia kwa uchungu sana kwenye taasisi yake na hajazifanyia kazi, eti halafu anakuja kuibua dosari na kasoro kwenye taasisi nyingine,

nadhani huko kutakua ni kutapeliwa kifikra sasa, na kwahivyo hakuna haja ya kubabaika na hoja za askofu tapeli kisiasa:pulpTRAVOLTA:

Napinga pendekezo lako kwa njia ya hoja inayoambatana na ushahidi usiokanushika

Kuna utapeli mkubwa kuliko kitendo cha kusaka ushindi wa kisiasa kwa kutumia mbinu haramu za (1) PREMARKED BALLOTS na (2) KUENGUA WAGOMBEA HALALI KWA KUTUMIA HADAA ZA KISHERIA tena katika nchi nzima kwenye chaguzi tatu mfululizi hapa nchini Tanzania katika miaka ya 2019, 2020, na 2024?

Kuna unyani mkubwa kuliko kitendo cha MKUTANO MKUU WA CCM kumpitisha mgombea Urais 2025 ambaye bado hajajaza fomu kwa mujibu wa Kanuni za chama wakati mkutano haukutaja kabisa ajenda ya kutengua kanuni hizo kwa muda ili kuhalalisha ajenda yao ya kumteua Samia anayeogopa uchaguzi?

Yaani wajumbe wote 2000 wa mkutano mkuu, wakiwemo wanasheria kama vile kina Dr. Tulia Ackson (spika wa bunge) hawakuweza kuona dosari hii ya kikanuni, halafu wewe unataka Taifa liendelee kuamini tena uwezekano wa mkutani mkuu wa CCM kuendelea kuisimamia serikali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni na taratibu zilizopo?

Hak8ka unabahatisha na kujitoa ufahamu sana we jamaa. Lakini kumbuka haya:

Tunaweza kuwapotosha watu wachache siku zote. Tunaweza kuwapotosha watu wote kwa siku chache.Lakini hatuwezi kuwapotosha watu wote siku zote.

Sababu: Uvumilivu unatokana na taarifa haba huwa na ukomo. Ukomo ni pale picha kubwa ta ukweli wote inaoifahsmika kwa watu wite.

Na sasa ukomo huo umefika tayari. Saa ya mageuzi ya kimfumo ni sasa na sio baadaye.

Hata mgombea wa urais aliyeteuliwa na mkutano mkuu wa CCM alikwepa kuchaguliwa kupitia mchakato rasmi wa kikanuni maana anajua matokeo ya uchaguzi hayawezi kuwa upande wake.

Alionekana akisema kwa lugha ya mwili (body language) kwamba: "NAOGOPA UCHAGUZI, NAOMBA MNITEUE" ili tumalize mambo yote leo nami niweze kupata usingizi.

Wewe pekee ndiye bado kipofu!

1739786004523.png
 
Kuna utapeli mkubwa kuliko kitendo cha kusaka ushindi wa kisiasa kwa kutumia mbinu haramu za (1) PREMARKED BALLOTS na (2) KUENGUA WAGOMBEA HALALI KWA KUTUMIA HADAA ZA KISHERIA tena katika nchi nzima kwenye chaguzi tatu mfululizi hapa nchini Tanzania katika miaka ya 2019, 2020, na 2024?

Kuna usanii mkubwa kuliko kitendo cha MKUTANO MKUU WA CCM kumpitisha mgombea Urais 2025 ambaye bado hajajaza fomu kwa mujibu wa Kanuni za chama wakati mkutano haukutaja ajenda ya kutengua kanuni hizo kwa.muda ili kuhalalisha ajenda husika?

Unabahatisha sana. Lakini kumbuka:

Tunaweza kuwapotosha watu wachache siku zote. Tunaweza kuwapotosha watu wote kwa siku chache. Lakini hatuwezi kuwapitosha watu wote siju zote. Uvumilivu huwa na ukomo. Na ukomo umefika tauari. Saa ya mageuzi ya kimfumo ni sasa.
hayo mambo ya udanganyifu katika kura huwa ni dhana potofu na drama tu za kisiasa, hayanaga ukweli wowote my lady,

wagombea wasio kidhi sifa na vigezo stahiki vya kisheria na kikatiba hawastahili kupewa fursa ya kugombea, ni muhimu sana kuenguliwa na hata kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi October wataenguliwa tu vizuri sana kwasababu hawana sifa za kikatiba kua viongozi.

kuhusu CCM,
nadhani jambo ni lao na wameamua kadiri walivyoona inafaa kulingana na sheria na katiba yao, na binafsi naona ni miongoni mwa maamuzi muhimu sana ya kihistoria wameyafanya CCM na kuviacha vyama vingine vya siasa vilivyo kua vinasubiri wagombea wa kuokoteza watakao enguliwa kwenye mchachakato wakiwa waneduwaa wasijue la kufanya.

Jambo la mwisho,
nasisitiza kujiepusha kurubuniwa na kutapeliwa kifikra na vibaka wa kisiasa nchini.

Mageuzi katika nchi hii hayafanyiki bila kwanza CCM kuamua. Na hii ni kumaanisha, mustakabali wa taifa letu upo chini ya serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia suluhu Hassan 🐒
 
Kumekuepo na hadaa za wanasiasa matapeli kuhubiri mabadiliko ya sheria za uchaguzi nnje kabisa ya wakati wa mabadiliko ya sheria na katiba, kana kwamba hayo ndiyo mahitaji muhimu zaidi kwa wananchi wa Tanzania kuliko maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara, miundombinu, usafirishaji n.k

Lakini pia,
matapeli hao wa kisiasa nchini wanaendelea kuhadaa wananchi zaidi kwamba hitaji la waTanzania ni vyeo na mamlaka. Kwamba wananchi wanahitaji sana matapeli hao wa kisiasa wapate vyeo, kuliko mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Na ndio maana,
agenda kubwa za wanasiasa hao waliofilisika hoja zimekua ni kujadili umri wa makamu mwenyekiti wa CCM bara, na na ubaguzi dhidi ya ukanda anakotoka rais Dr. Samia Suluhu Hassan na jinsia yake, kana kwamba ukiwa kiongozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka upande wa Zanzibari Bara, ni kosa na ni anasa kubwa mno, huku wakijua wazi kabisa kua hakuna mtu anaweza kupata uongozi wa kitaifa Tanzania bila waZanzibari.

Ni vizuri kama wanasiasa kuibua hoja zenye mashiko kwa wakati sahihi na muafaka, kuliko kubwekabweka na kuwahadaa wananchi kwa vimisemo vitakavyowaathiri wenyewe na kuwakosesha fursa na haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi ambao wanawataka kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Kumbuka,
hata mtua aimbe, alie, acheke, acheze au abwekebweke namna gani, uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania upo pale pale, ni Oct.2025 :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
Chama hakina wanachama huku chini. Hakina uongozi eti nacho kinajigamba kuwa ikiwepo Tume Huru ya Uchaguzi eti kitashinda Urais. Urais wa JMT sio sawa na kuwa Mwenyekiti wa SACCOS kama Chadema.
 
Hayo maji elimu na afya viko wapi?mara ngapi wananchi wanavilalamikia hawavipati?
umejiuliza mbona kibaka na tapeli wa siasa havizungumzii?

sasa kama kibaka wa siasa hazungumzii hivyo, anazungumzia uchaguzi tu, wewe si utakua mpotoshaji gentleman?🐒
 
Kumekuepo na hadaa za wanasiasa matapeli kuhubiri mabadiliko ya sheria za uchaguzi nnje kabisa ya wakati wa mabadiliko ya sheria na katiba, kana kwamba hayo ndiyo mahitaji muhimu zaidi kwa wananchi wa Tanzania kuliko maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara, miundombinu, usafirishaji n.k

Lakini pia,
matapeli hao wa kisiasa nchini wanaendelea kuhadaa wananchi zaidi kwamba hitaji la waTanzania ni vyeo na mamlaka. Kwamba wananchi wanahitaji sana matapeli hao wa kisiasa wapate vyeo, kuliko mahitaji yao muhimu ya kila siku.

Na ndio maana,
agenda kubwa za wanasiasa hao waliofilisika hoja zimekua ni kujadili umri wa makamu mwenyekiti wa CCM bara, na na ubaguzi dhidi ya ukanda anakotoka rais Dr. Samia Suluhu Hassan na jinsia yake, kana kwamba ukiwa kiongozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka upande wa Zanzibari Bara, ni kosa na ni anasa kubwa mno, huku wakijua wazi kabisa kua hakuna mtu anaweza kupata uongozi wa kitaifa Tanzania bila waZanzibari.

Ni vizuri kama wanasiasa kuibua hoja zenye mashiko kwa wakati sahihi na muafaka, kuliko kubwekabweka na kuwahadaa wananchi kwa vimisemo vitakavyowaathiri wenyewe na kuwakosesha fursa na haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi ambao wanawataka kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Kumbuka,
hata mtua aimbe, alie, acheke, acheze au abwekebweke namna gani, uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania upo pale pale, ni Oct.2025 :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
Ninyi mliojiunga na JF recently hususani 2020s mpo KICHAWA. Huwezi kupinga kwamba ubovu wa hali hapa nchini sababu yake ni utawala mbovu na chanzo ni uchaguzi hufanyika kama kiini macho kwasababu ya tume mbovu ya uchaguzi. Ili kukukumbusha ubovu wenyewe mfano halisi ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Ule siyo uchaguzi huru bali wizi huru wa kura.
 
hayo mambo ya udanganyifu katika kura huwa ni dhana potofu na drama tu za kisiasa, hayanaga ukweli wowote my lady,

wagombea wasio kidhi sifa na vigezo stahiki vya kisheria na kikatiba hawastahili kupewa fursa ya kugombea, ni muhimu sana kuenguliwa na hata kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi October wataenguliwa tu vizuri sana kwasababu hawana sifa za kikatiba kua viongozi.

kuhusu CCM,
nadhani jambo ni lao na wameamua kadiri walivyoona inafaa kulingana na sheria na katiba yao, na binafsi naona ni miongoni mwa maamuzi muhimu sana ya kihistoria wameyafanya CCM na kuviacha vyama vingine vya siasa vilivyo kua vinasubiri wagombea wa kuokoteza watakao enguliwa kwenye mchachakato wakiwa waneduwaa wasijue la kufanya.

Jambo la mwisho,
nasisitiza kujiepusha kurubuniwa na kutapeliwa kifikra na vibaka wa kisiasa nchini.

Mageuzi katika nchi hii hayafanyiki bila kwanza CCM kuamua. Na hii ni kumaanisha, mustakabali wa taifa letu upo chini ya serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi na kipenzi cha waTanzania Dr Samia suluhu Hassan

Napinga wazo lako. Kumbuka:

Kuna njia tatu za kuthibitisha ukweli wa kauli: kutamka jambo kwa kupaza sauti kubwa, kurudia rudia kaulli kwa ukali, na kuweka ushahidi mezani kwa upole.

Natumia mbinu ya tatu kuthibitisha utapeli wa kisiasa katika uchaguzi unaofanywa na ccm kama ifuatavyo:

Back
Top Bottom