Ni haki DCC kukamata toyo za kuchaji, kuzipiga faini na kulipisha Tsh 50,000 ya maegesho kila mwezi?

Ni haki DCC kukamata toyo za kuchaji, kuzipiga faini na kulipisha Tsh 50,000 ya maegesho kila mwezi?

maddox

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2010
Posts
2,086
Reaction score
4,669
Niaje niaje, lengo la uzi wangu sio kubishana na mamlaka za serikali bali naomba kupata ufafanuzi. Nimelileta hapa jukwaani suala la DCC kukamata vile vitoyo vya kuchaji na kuvipiga faini kwa kupaki mjini na kuvilipisha parking ya tsh 50,000 kwa kila mwezi.

Je, ni sawa kulipisha hiyo pesa? Ipo kwa mujibu wa sheria? Maana isije kuwa mnatafuta sifa ili kumharibia Rais Samia kwenye kuelekea uchaguzi mkuu hapo baadaye

Kulikuwa na maneno mpaka kudai leseni ya kuendesha vile vidubwasha ambavyo kwa asilimia kubwa vimewaajili vijana walioamua kukataa tabia mbaya za mitaani na kuamua kujishughulisha

Je, ni sawa kulipisha pesa hiyo ya elfu 50 kwa mwezi?

Naomba wasomi na wachambuzi hapa jukwaani tulipitie kwa kina
 
Zimekamatwa kama 200 na wamepigwa faini kuanzia 200,000 mpaka 100,000...........na huu mchongo waratibu ni polisi kwa kushirikiana na DCC
 
Zimekamatwa kama 200 na wamepigwa faini kuanzia 200,000 mpaka 100,000...........na huu mchongo waratibu ni polisi kwa kushirikiana na DCC
Kuna kamoja ka mshikaji nimepanda jana hapa Segerea nikawa namhoji, kasema kwanza havisajiliwi na hasumbuliwi kabisa na trafiki.
 
Back
Top Bottom