Ni haki Simba SC kumbadili kocha kipindi hiki

Hoja nyingi wanazotoa mashabiki hazina ushahidi wowote wa takwimu au matokeo. Ni hoja zinazosukumwa na unazi + hisia za kufikirika. Hebu tuzipitie hoja hizi;

1. Eti Simba ya Omog haifungi magoli mengi!!! Striker sijui mbovu, n.k. Hadi tunakwenda mitamboni, Simba ndio timu inayoongoza kwa idadi ya magoli ya kufunga, na pia kama haitoshi ina goal difference kubwa kuliko zote ktk ligi ya VPL
2. Eti Simba haichezi vizuri! Kucheza vizuri kulinganisha na nani? Kama kulinganisha na Ulaya sawa, lkn kama ni mpira wa Afrika Mashariki, big no!!! Takwimu karibu zote za kuonyesha ubora wa timu ktk mechi mbili za VPL zimeonesha ubora wa Simba
3. Eti Mkude hachezi! Ni mechi ya pili tu ya Ligi wapendwa! Pili, kocha hawezi kuchezesha viungo wa ulinzi watupu kwa timu kama Simba, tatu, kocha lazima atengeneze mfumo na kikosi cha kwanza kupitia mashindano, na anaendelea kuingiza wachezaji kadri anavyoona inafaa. Hata hivyo, Kotei kiufundi ni bora kuliko mkude labda tuseme Mkude anaujua mpira wa kibongo.
4. Eti timu haijafanya vizuri kwenye ligi. Hii ni hoja dhaifu kuliko zote. Timu iko nafasi ya pili, na imetoka sare na timu bora kabisa ya Azam ktk uwanja wa ugenini. Real Madrid imevimbiwa nyumbani na katimu kadogo kabisa huko Hispania, Man United nayo chupuchupu weekend iliyopita! Tujifunze kuheshimu mpira kwa kuheshimu timu pinzani.

Watu waseme labda wanataka kumfukuza kocha kwa ajili ya hasira za kukosa ubingwa msimu uliopita lakini sio kwa hoja hizi hapo juu.
 
Nimekuelewa mdau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ningependa Simba Sc impe muda kocha Omog kwani hu ndo mwanzo waligi ukizingatia Ana wachezaji wengi wapya na waliofanya vzr kwenye timu zao. NI vugumu wote kupata no first eleven

Hakika. Timu hutengenezwa, na unaona kabisa kocha ndio anajaribu kupata viongozi 2 wa ushambuliaji. Tayari Okwi yuko available lkn wakati kocha anatafuta combination kati yake na Boko, kukawa na majeruhi kwa upande wa Boko, Gyan, ndio katia timu, halafu watu wanapiga kelele kupita kiasi.

Ila Omog akae chonjo na begi mkononi, akumulikae mchana usiku atakuchoma tu. Najua sana tabia za viongozi na mashabiki wa soka wa nchi yetu. Wakikuchoka hata ufanyaje
 
Tatizo la viongozi wetu kila mmoja ana mchezaji wake na pindi huyo mchezaji asipopangwa maneno na chokochoko huanzia hapo, ndio maana timu inaishia kufanya vibaya tu..kwa maoni yangu Omog apewe muda aipeleke club mahali sahihi, sababu naona kuna kitu anacho tofauti na hawa wazawa!
 
Omogi ameshindwa kuunga stricking force na kingine kuchelewa kufanya sub. Haya si matatizo ya kumfukuza kocha. Ikifika mechi amwachiea Mayanja apange kikosi ushindi unapatikana tu. Bado mapema sana kuwaza hayo.

Umeona wapi kocha msaidizi akipanga kikosi kocha mkuu akiwepo
 
hivi ukiachana na omog ni kocha gani aliyeipeleka Simba mashindano ya kimataifa mala ya mwisho????
 
Na kweli aondoke tu mwaka jana katukosesha ubingwa kizembe kabisa wakati Yanga walishatepeta mwishoni mwa ligi na ukata kibao ulikuwa unawakabiri
 
Kwa kifupi wachezaji anao ila hawezi kupanga kikosi cha ushindi, ameshindwa mbinu za kufundisha strikers kufunga magoli
 
Wasituchanganye kocha katulia wao washaanza figisu,sio mbaya kama wanataka tusalie wa3 tena katika msimamo wa ligi kwa mara nyingine,sijaona sababu yeyote ya msingi kumuondoa omog,ata me nimeckia keshapewa mechi kadhaa endapo ata loose bac fagio litampitia..,bongo tukiendelea kwa style hii tusaau kupanda juu kisoka.
 
Back
Top Bottom