Mimi nadhani hamna tatizo vikao kufanyika Ikulu. Kwani Ikuku si makazi binafsi vile vile ya JK? sasa kuna kosa gani kuwaalika watu nyumbani kwake wakafanya mkutano kwenye sitting room yake?
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kwa ridhaa yenu wana/wenye nchi imeiweka madarakani kwa zaidi ya miaka 45 huku mkiipa mamlaka ya kutumia rasilimali zenu bila usimamizi wenu. Hili la ikulu sidhani kama ni la msingi sana labda mwenzetu una personal issue hapo ila wizi unaofanywa na CCM ni mkubwa mara million sabini ya kufanyaia kikao ikulu. Nimejaribu kuwa mkali kidogo ilkujibu uhalali wa swali lako?
Mkuu, naomba nikiwa nikufahamishe kuwa sina personal issue na mtu yeyote, na uandishi wangu hautawaliwi na hizo. Kama umesoma vizuri nimeuliza swali la kimsingi kuhusu kufanyia vikao vya chama tawala ikulu. Nakumbuka kuanzia enzi za TANU (ndiyo, nakumbuka vizuri sana) vikao vya chama vilifanyika katika ofisi za chama, hata wakati wa Chama kiliposhika hatamu, ndio kwanza makao makuu ya CCM Lumumba street, yakapata hadhi zaidi. Je kumekuwa na mabadiliko rasmi mapya yaliyotokea ambapo chama tawala kimeshika hatamu tena
CCM ndio chama tawala, sasa kufanyia vikao vya chama IKULU sioni kama kunatatizo. kwani kuna matatizo gani kwa wadanganyika kwa kufanyia vikao hapo IKULU??
Kinachotakiwa ni kuing'oa CCM madarakani ili mambo yawekwe sawa.
Mimi nadhani hamna tatizo vikao kufanyika Ikulu. Kwani Ikuku si makazi binafsi vile vile ya JK? sasa kuna kosa gani kuwaalika watu nyumbani kwake wakafanya mkutano kwenye sitting room yake?
Mimi nadhani hamna tatizo vikao kufanyika Ikulu. Kwani Ikuku si makazi binafsi vile vile ya JK? sasa kuna kosa gani kuwaalika watu nyumbani kwake wakafanya mkutano kwenye sitting room yake?
Ikulu ni makazi binafsi ya JK? Tangu lini?
Akiamua kuiuza anaweza? Akiamua kuivunja tu anaweza?
Acha mambo haya bwana. Sio tu ni vibaya Kikwete kuendesha vikao vya CCM Ikulu, rais hatakiwi kuwa mwenyekiti wa chama, there arises a conflict of interest hapo, kuna information nyingine ambazo rais anakuwa privy nazo ambazo hazina best interest ya CCM, katika situation hiyo rais atafanya kazi katika capacity gani, kama rais au mwenyekiti wa CCM?
Hilo ni tatizo