Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Vikao vya Kamati Kuu ya CCM vimekuwa vikifanyika Ikulu tangu enzi za Mwl. Nyerere hadi leo enzi za Mama. Hakuna la ajabu hapo.
Enzi za Nyerere, Chama kilikuwa kimeshika UTAMU .......!!

Mkapa was so principled, sikumbuki yeye kufanyia mikutano ya chama Magogoni.
 
Kwa sababu aliyekabidhiwa hiyo ofisi ni mwana ccm tena mwenyekiti.
 
KWA HIYO KITU KIKIFANYIKA MARA NYINGI HUGEUKA KUWA HALALI HATA KAMA NI HARAMU?

Usisahau, mtu anayekuwa Rais, huwa anakuwa na madaraka au majukumu mbalimbali... Sasa kila huko aliko na jukumu wakiamua waende ikulu kujenga mambo yao watakuwa wanafanya halali? Mfano, rais yeyote aliyeko madarakani, huwa vile vile ni baba au mama wa familia...
Usisahau kuwa Ikulu pia ni Makazi Rasmi ya Rais na familia yake. Hivyo, ni ruksa kwa vikao vya familia kufanyikia hapo. Hata vya Kitchen Party!!
 
Nchi yetu ni mali ya watanzania na muongozo wake ni katiba tuliyonayo.

Jana kwa hofu tena na aibu juu kamati kuu ya CCM imekutana usiku ikulu katika kujadiri mambo ya chama...
Kwa hiyo ccm sio sehemu ya hao wanaounda umma? 😂😂
 
Nchi yetu ni mali ya watanzania na muongozo wake ni katiba tuliyonayo.

Jana kwa hofu tena na aibu juu kamati kuu ya CCM imekutana usiku ikulu katika kujadiri mambo ya chama...
Wafanyie tu kwani mm mwananchi wa kawaida CCM kufanyia Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Ikulu naathirika na nini? Tuko busy na tozo za vifurishi, hayo mangine hatuna mzuka nayo
 
Vikao vya Kamati Kuu ya CCM vimekuwa vikifanyika Ikulu tangu enzi za Mwl. Nyerere hadi leo enzi za Mama. Hakuna la ajabu hapo.
Nyerere kuvunja katiba na sheria haihalalishi kuwa CCM ya sasa hivi nayo ikivunja katiba na sheria kuwa ni sawa.
 
Uoga wake ndiyo umetufikisha hapa, watu wanakula pesa ya umma bila uoga, hata Iddi Amini ilikuwa ni mamlaka kama zilivyo zingine.
Uoga wake ndio usalama wa nafsi yake.....

Wewe si muoga haya kaandamane wanapokataa maandamano....

#KaziIendelee
#SerikaliMbiliMilele
 
Sheria gani imevunjwa? Iweke hapa tuione.
Unahitaji sheria kujua kuwa ofisi za uma hazipaswi kutumika na vyama vya siasa kufanya siasa zao?Yaani unahitaji sheria kujua kuwa Chadema hawawezi kutumia ikulu kama ofisi yao ya kuendeshea shughuli zao za kisiasa?
 
Wajuzi wa Mambo ya SIASA za TANZANIA naomba Kuuliza Yafuatayo

[emoji117]JE ni Sahihi CCM kufanyia Vikao vya Chama IKULU?

[emoji117]JE KATIBA inaruhusu Vikao vya Vyama kufanyikia Kwenye Majengo ya SERIKALI

[emoji117]JE Kama CCM ni Chama Tawala kwanini BENDERA ya CHAMA Hazipeperushwi kwenye Majengo ya SERIKALI?
 
Ndio ni sahihi kwa sababu Mkiti ni Rais wa chama husika.
Angekuwa Rais kofia hiyo tu na Mkiti wa chama tawala kofia yake kwa chama hichohicho tungehoji.
 
Pamoja na mabadiliko ya katiba ya mwaka 1992 na kuruhusu vyama vingi, inaonekana ni kwenye karatasi kwani CCM hawaoni tofauti kati ya chama na serikali hata kidogo.
De facto monoparty
 
Back
Top Bottom