Binafsi in the sense kwamba anaishi pale rasmi kama makazi yake. Si kwamba ana ownership kwamba anaweza kubomoa. Ni sawa na wewe kama unapewa nyumba ya kuishi na mwajiri wako. Unaweza kuitumia kwa matumizi yako binafsi. Naye anaweza kuitumia, kama kumtoa mwali, vikao vya arusi ya mtoto wake, na hivyo vya CCM, n.k. Si anaishi hapo kama makazi yake? Sasa akipata wageni wake binafsi kama wakwe anawapeleka wapi?? Labda issue ingekuwa mkutano huo unafanyika ofisini hapo Ikulu au kwenye Living room yake? Sijui Ikulu imetenganishwa vipi kati ya Office wing and residence wing.
Suala la yeye kuwa M'kiti wa CCM na Raisi vile vile nadhani ni issue tofauti na hii tunayoongelea
Unachoshindwa kufahamu au kuweka wazi ni kwamba, mtu binafsi kufanya shughuli binafsi kama kutoa mwali na vikao vingine vya kibinafsi si sawa na Kikwete kufanya vikao vya CCM. Kikwete anaweza kumtoa mwali Ikulu, hiyo ni shughuli binafsi.Kikwete kufanya kikao cha CCM ikulu si sawa, kwa sababu hii ni shughuli ya chama, si shughuli binafsi ya Kikwete.
Ikulu si makao binafsi ya Kikwete, ni makao rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pale Kikwete hakai kwa kofia ya mwenyekiti wa chama, anakaa kama rais, bajeti ya Ikulu haitoki CCM, CCM hawalipii maji wala umeme wa Ikulu, serikali inalipia.
Sasa kwa nini CCM watumie resources za serikali? Kwa nini CCM wasifanye vikao vyao Lumumba au kwenye jengo linguine la CCM badala ya kufanya unyonyaji huu wa kutumia majengo na resources nyingine za serikali?
Watu wa CUF na CHADEMA nao wakisema wanataka kufanya vikao vyao Ikulu kama wanavyofanya CCM,ikulu itakubali?
Kwamba Kikwete ameshinda uchaguzi kwa tiketi ya CCM na kuunda serikali ya CCM ahaina maana CCM inaweza kutumia resources za serikali itakavyo, si sawa, si haki, ni unyonyaji, ni utovu wa maadili, kuna conflict of interest, kuna double standard.
Kama nilivyosema mwanzo, usuluhishi mzuri ungekuwa kufanya rais na mwenyekiti wa CCM kuwa watu wawili tofauti.