Inaonyesha huijui historia ya Tanzania.
Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 ikiwa na katiba ya vyama vingi. Chama cha TANU ndicho kilichoshinda uchaguzi na kuunda serikali ya kwanza ya Tanganyika huru.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuzaa nchi inayoitwa Tanzania. Bado wakati huo tulikuwa na vyama vingi. Zanzibar ilikuwa inaongozwa na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini kulikuwa na vyama vingine.
Tanzania ikabadilisha katiba na kuleta chama kimoja, TANU. Lakini ikumbukwe kuwa Zanzibar walikuwa na ASP.
Mwaka 1977 TANU na ASP vikaungana kuunda chama kimoja nchi nzima, CCM.
Wakati wa CCM kulikuwa na kipengele cha chama kushika hatamu, na kuwa na kofia mbili. Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti wa Chama (Taifa) Mwalimu Nyerere akiwa ni 'automatically' Rais wa Jamhuri, Katibu wa CCM Mkoa akawa automatically Mkuu wa Mkoa n.k. Kwa kifupi NEC ilikuwa ndiyo kauli yenye nguvu kuliko Bunge. Uchaguzi wa Rais ulikuwa na mgombea mmoja, kura zilikuwa za Ndiyo na Hapana!
Kama Nyerere wakati ule alikuwa anafanya vikao vya NEC Ikulu alikuwa ndani ya mamlaka aliyokuwa nayo kikatiba, kweni chama kilikuwa kimeshika hatamu!
Sasa tuna vyama vingi tangu 1992. Ikulu ni ofisi ya SERIKALI, siyo ofisi ya CHAMA CHOCHOTE! Yeyote anayetumia ofisi za serikali kufanyia vikao vya chama anakiuka katiba hata hii ya sasa yenye mapungufu! Nina hakika jk analijua hilo ila anafanya makusudi hasa kwa kuwa anafikiri watanzania wengi hawajui katiba inasema nini katika hilo. Na kwa jinsi mjadala huu unavyoendelea humu jamvini, ninaamini wengi sana bado hawajafahamu tofauti hiyo!
Mungu Ibariki Tanzania!