Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Or dear. Wale wanaotaka kutenganisha Uenyekiti wa chama na Urais wana point.

Bonge la point, lakini dhambi alizochuma anaona usalama lumumba utakuwa mdogo she**nz taip
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mbona Obama na Bush walifanya mikutano na kulisha futari waIslamu pale White House. Tanzania ina issues kubwa sasa hivi. Hivi zingine fumbeni macho.

Dini ni suala la imani,lakini kamati kuu ni suala la itikadi brother!
 
big up wakazi wa mbeya kwa kunipopolea mawe yule kiongozi wa serikali aliekuja na msafara wa magari ya serikali kwenye mkutano wa ccm.. nimechelewa kujua hiki kikao cha nec ikulu.. ningewastua mje mnipopolee na hawa.. ndo dawa yao hiyo..
 
Duh! Kweli bongo watu wanapeleka nchi kihuni!

Hapo kama kwa wenzetu kashfa hii mtu anang'oka
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ivi mumeshau namna wanavyotumia magari ya serikali kwenye shughuli za chama/sembuse ofisi?
 
Ikulu kwa ufahamu wangu ni ya Taifa zima..

Si ya chama hata iwe kilichotoa Rais!

Rais ama Urais ni taasisi,na ikulu ni ofisi ya taasisi hiyo.. Sasa chama kinapoitumia taasisi hiyo kama mali yake,ujue kuna udhaifu mkubwa wa matumizi ya mamlaka hayo!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ukweli ni kwamba watanzania wengi wakiwemo viongozi hawajui tofauti kati ya serikali na chama, hasa chama tawala. Ndiyo sababu hata vyombo vya dola kama polisi vinatumiwa na ccm kukandamiza vyama vingine na hata wasiokuwa wanachama wa chama chochote pale wanapoona ccm iko mashakani. Ni mara ngapi kwenye shughuli za kiserilaki unakuta Waziri Mkuu, Waziri au Mkuu wa Mkoa wamezungukwa na wapambe wa ccm, bila aibu wakiwa na sare za chama chao? Hayo huwezi kuyaona kwenye nchi zingine zenye uelewa wa masuala ya kikatiba. Tanzania imeingia kwenye mfumo wa vyama vingi lakini dhana za walio madarakani na wapambe wao bado ni zile zile za chama kimoja. Wakati huo hatukuwa na mipaka kati ya chama na serikali. Katibu wa CCM wa Mkoa ndiye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa CCM ndiye kwa kipindi kirefu aliyekuwa Rais, n.k. Sasa ndipo tunapolia na kubadilisha katiba ili mipaka hiyo iwekwe wazi. Lakini cha maana zaidi ni kutoa elimu ya uraia kwa watanzania walio wengi, ili waweze kuhoji kila inapotokea dola au serikali kutumika kichama badala ya kuwa msimamizi wa haki na maslahi ya watanzania bila kujali itikadi zao.

Tunakumbuka sana wakati jeshi la polisi lilipozuia maandamano ya kudai nyongeza za posho za wabunge yaliyoitishwa na CHADEMA kwa madai ya kuwa taarifa za kiinteligensia zinasema kuna tishio la 'Al Sababu...' Lakini, sherehe za miaka 50 ya 'Uhuru' wa Danganyika na mikusanyiko yote ya watu, hapakuwa na tishio la 'Al Sababu...' Huo ni mmoja tu wa mifano hai ambayo inaonyesha jinsi gani jeshi la polisi limetekwa katika kukilinda chama cha magamba, badala ya kuwalinda watanzania na haki zao.
 
Hamna majungu mkuu. Juzi aliwaita CHADEMA na kufanya mazungumzo nao pale. Rais ana ukumbi wa kufanyia mazungumzo.

Watanzania mna mambo mengi ya kulalamika. Lakini hili sio moja.

Ni kweli hakuna majungu Zakumi, mbona viliendeshwa vikao vya vyama vya siasa Ikulu, walianza CHADEMA, CUF na baadaye NCCR - Mageuzi. Leo wamekwenda CCM hata kama mada si katiba mpya wanaona ni tatizo?
 
CCM ndiyo chama tawala bana!

Hata kama ccm ni chama tawala, wana ofisi za chama Lumumba na Makao Makuu ya chama yako Dodoma, wanaweza kufanya vikao vyao kwenye maeneo yao, siyo kwenye ofisi za serikali.

Hata siku moja huwezi kuona Waziri Mkuu wa Uingereza akifanya kikao cha chama chake (Tories) Downing Street. Ikiwa Rais anakutana na viongozi wa vyama vingine Ikulu, anakutana nao kama Rais wa nchi, na sio kama mwenyekiti wa chama cga magamba. Ikulu na ofisi ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ni mahali pa kufanyia kazi za serikali kama kiongozi wa serikali. Kuitisha vikao vya ccm Ikulu ni KOSA!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hamna majungu mkuu. Juzi aliwaita CHADEMA na kufanya mazungumzo nao pale. Rais ana ukumbi wa kufanyia mazungumzo.

Watanzania mna mambo mengi ya kulalamika. Lakini hili sio moja.
Hao CHADEMA walimfuata RAIS au Mwenyekiti wa CCM? Hata hao vyama vingine baadaye vilisema vinaenda kumuona Rais au M/Kiti wa CCM? Na hao uliowaona pichani wakiwa ndani ya jezi wajadili mambo ya chama wanaongozwa na Rais au Mwenyekiti wao? Kwenye mahudhurio yao ya Muhtasari wa kikao unafikiri wamemuandika Rais?
 
Mbona Obama na Bush walifanya mikutano na kulisha futari waIslamu pale White House. Tanzania ina issues kubwa sasa hivi. Hivi zingine fumbeni macho.

Kuhusu futari tunaenda nje ya mjadala. Tuongelee mambo yanayohusu vyama. kusema tufumbie macho haya mambo madogo si sahihi kwa vile hayo madogo leo, kesho yatakuwa makubwa. Wahenga walisema, 'Usipoziba ufa, utajenga ukuta'!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Jamani serikali hii inaitwa ya CCM. Baba akimtembelea mwanae kwa mazungumzo wayafanyie kivulini, mwembeni? Mtoto atakosa laana kweli! Tusubiri KATIBA MPYA iyaweke haya wazi. Hakuna kipengere cha Katiba ya sasa kilichovunjwa hapo wala sheria yoyote ya nchi.
 
CCM ndiyo chama tawala bana!

Hapa naona elimu ya uraia imepungua.

Inabidi kutofautisha kati ya chama na serikali. Mambo ya chama tawala katika serikali yanaingia tu katika sera zake, ambazo kimsing,i katika utekelezaji wake, utakuwa umepitishwa na bunge ambalo hata hivyo ni la vyama vingi. Uendeshaji wa chama kamwe hauhusishi serikali maana chama kina muundo wake. Tukumbuke kuwa serikali ya Tz sio ya ccm pekee, tofauti na wakati ule wa chama kimoja ambapo chama kilishika hatamu na sera hiyo kuelezwa kwa wananchi kikamilifu. Tangu mfumo wa vyama vingi uanze, sera ya chama kushika hatamu iliondolewa kimsingi, ila bado mazoea ndiyo yanaendeleza dhana hiyo kama tuonavyo katika mjadala huu.

Kuna haja ya kuweka wazi, hasa katika katiba mpya inayokuja, kuhusu utengano wa chama na serikali na majukumu ya kila mmojawapo
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Si anamwiga Nyerere.

Inaonyesha huijui historia ya Tanzania.

Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 ikiwa na katiba ya vyama vingi. Chama cha TANU ndicho kilichoshinda uchaguzi na kuunda serikali ya kwanza ya Tanganyika huru.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuzaa nchi inayoitwa Tanzania. Bado wakati huo tulikuwa na vyama vingi. Zanzibar ilikuwa inaongozwa na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini kulikuwa na vyama vingine.
Tanzania ikabadilisha katiba na kuleta chama kimoja, TANU. Lakini ikumbukwe kuwa Zanzibar walikuwa na ASP.
Mwaka 1977 TANU na ASP vikaungana kuunda chama kimoja nchi nzima, CCM.

Wakati wa CCM kulikuwa na kipengele cha chama kushika hatamu, na kuwa na kofia mbili. Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti wa Chama (Taifa) Mwalimu Nyerere akiwa ni 'automatically' Rais wa Jamhuri, Katibu wa CCM Mkoa akawa automatically Mkuu wa Mkoa n.k. Kwa kifupi NEC ilikuwa ndiyo kauli yenye nguvu kuliko Bunge. Uchaguzi wa Rais ulikuwa na mgombea mmoja, kura zilikuwa za Ndiyo na Hapana!

Kama Nyerere wakati ule alikuwa anafanya vikao vya NEC Ikulu alikuwa ndani ya mamlaka aliyokuwa nayo kikatiba, kweni chama kilikuwa kimeshika hatamu!

Sasa tuna vyama vingi tangu 1992. Ikulu ni ofisi ya SERIKALI, siyo ofisi ya CHAMA CHOCHOTE! Yeyote anayetumia ofisi za serikali kufanyia vikao vya chama anakiuka katiba hata hii ya sasa yenye mapungufu! Nina hakika jk analijua hilo ila anafanya makusudi hasa kwa kuwa anafikiri watanzania wengi hawajui katiba inasema nini katika hilo. Na kwa jinsi mjadala huu unavyoendelea humu jamvini, ninaamini wengi sana bado hawajafahamu tofauti hiyo!

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Rais kaona ni bora kufanyia kikao ikulu ili kuepusha gharama za yeye kufanyia kikao Lumumba au Dodoma. Ingebidi achome mafuta mengi, posho za wasaidizi wake, pamoja na gharama nyingine za usalama. So akaamua kufanya kikao white house kama best strategy, au vipi?
 
Muoneeni huruma jk mana ana hang over ya urais,hajui hata aongoze vp maskini
 
Inaonyesha huijui historia ya Tanzania.

Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 ikiwa na katiba ya vyama vingi. Chama cha TANU ndicho kilichoshinda uchaguzi na kuunda serikali ya kwanza ya Tanganyika huru.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuzaa nchi inayoitwa Tanzania. Bado wakati huo tulikuwa na vyama vingi. Zanzibar ilikuwa inaongozwa na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini kulikuwa na vyama vingine.
Tanzania ikabadilisha katiba na kuleta chama kimoja, TANU. Lakini ikumbukwe kuwa Zanzibar walikuwa na ASP.
Mwaka 1977 TANU na ASP vikaungana kuunda chama kimoja nchi nzima, CCM.

Wakati wa CCM kulikuwa na kipengele cha chama kushika hatamu, na kuwa na kofia mbili. Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti wa Chama (Taifa) Mwalimu Nyerere akiwa ni 'automatically' Rais wa Jamhuri, Katibu wa CCM Mkoa akawa automatically Mkuu wa Mkoa n.k. Kwa kifupi NEC ilikuwa ndiyo kauli yenye nguvu kuliko Bunge. Uchaguzi wa Rais ulikuwa na mgombea mmoja, kura zilikuwa za Ndiyo na Hapana!

Kama Nyerere wakati ule alikuwa anafanya vikao vya NEC Ikulu alikuwa ndani ya mamlaka aliyokuwa nayo kikatiba, kweni chama kilikuwa kimeshika hatamu!

Sasa tuna vyama vingi tangu 1992. Ikulu ni ofisi ya SERIKALI, siyo ofisi ya CHAMA CHOCHOTE! Yeyote anayetumia ofisi za serikali kufanyia vikao vya chama anakiuka katiba hata hii ya sasa yenye mapungufu! Nina hakika jk analijua hilo ila anafanya makusudi hasa kwa kuwa anafikiri watanzania wengi hawajui katiba inasema nini katika hilo. Na kwa jinsi mjadala huu unavyoendelea humu jamvini, ninaamini wengi sana bado hawajafahamu tofauti hiyo!

Mungu Ibariki Tanzania!

Baada ya kusoma posti hii, nimeijua historia ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom