Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?


Mimi naona zigo hili atupiwe Tendwa kwa maana yeye hasa ndiye anayetakiwa kusimamia sheria za vyama tumuone jinsi anavyoweweseka kama kuna mwandishi Please mtupie hili swali Tendwa afafanuwe kuwa inakuwaje CCM kutumia rasimali za nchi kuendeshea vikao vyao vya chama kinyume na utaratibu wa sheria za kusimamia vyama vya siasa ???
 
Reactions: EMT

unamaanisha kukiepushia chama tawala gharama japo kinapata ruzuku ya serikali kutoka kwenye kodi ya wananchi kama vyama vingine ?
 
Reactions: EMT

''Sizitaki mbichi hizi'' Spika kutogombea ubenge katika jimbo lake. - YouTube
 
lol kweli maboksi yanadatisha, hivi unayabebea kipande ipi kwa obamaphil?

Lol, naona napewa shule. Siku hizi mna hasira sana. Anyway, maboksi nayapiga kama kilometer mbili hivi kutoka ofisini kwa mjaluo.
 
Hamna majungu mkuu. Juzi aliwaita CHADEMA na kufanya mazungumzo nao pale. Rais ana ukumbi wa kufanyia mazungumzo.

Watanzania mna mambo mengi ya kulalamika. Lakini hili sio moja.

Inaonyesha ni mtupu kikatiba na vifungu vyake, pia ni mtupu kwa masuala ya sheria ya vyama vya siasa.Kwa masitakabari huo si vyema kundandia mambo usiyo yafahamu waachie wachambue mada wanaofahamu.Kuita wawakilishi wa vyama vya siasa ni katika msitakabari wa kiutawala katika kuandika katiba mpya ambayo yeye ndo msimamizi mkuu na amekula kiapo kuilinda.Hivyo kuwaita ikulu ni katika masuala ya kiutawala hata kama anakutana na wakulishi wa vyama vya siasa.
Kufanyia vikao vya kichama ikulu si sahihi kwa sheria ya vyama vingi.Ikulu ni kiutawala na si mambo ya kisiasa ya chama fulani kufanyia vikao vya kichama mahala pale.Huko ni kukiuka kutumia amali za watanzania na fedha za watanzania kukidhi masuala ya chama fulani ni kinyume .Kama kuna uthibitisho anapaswa kushitakiwa kutumia madaraka vibaya kukidhi haja ya kisiasa kinyume na kiapo na katiba ya nchi kwa kuvunja sheria ya vyama vingi inayokataza kufanya mambo ya kisiasa kwa kutumia mali ya serikali na kwenye ofisi za serikali kama ikulu.
 
Reactions: EMT
Sasa kama hapo wanalipana posho za chama au za sirikali.
 
Reactions: EMT
Nakubaliana na wewe kuwa nadandia tu. Lakini mpaka sasa hamjaonyesha kuwa kitendo kilichofanyika ni kuvunja sheria au utaratibu.

Kwani Hitler alivyoua watu zaidi ya milioni sita alivunja sheria yoyote ya Ujerumani?

....tumwache Nyerere Mkapa alifanya na Mwinyi alifanya.Tujenge utamaduni wa kuthamini utendaji wa watu tusiowapenda si kuwalaumu kwa kila kitu
Another ill formed argument example. Tokea lini kosa la mtu likahalalisha kosa la mtu mwingine?
 

Nakubali kuwa mimi ni mtupu. Naomba tu kipengele cha sheria au katiba hili na mimi nielimike.
 
Nimesoma. Hayo ndio mambo tunayolalamika hapa Marekani. George Bush alipokuwa rais, Democrats walikuwa wanasema anatumia F1 kwa safari za kisiasa. Sasa hivi yupo messiah Obama. Yeye anafanya yale ya Bush.

Walikuwa wanafanya hivyo kama marais au wenyeviti wa vyama vyao?
 



JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012

Hivi mbunge monduli yule EDWARD LOWASSA hayumo kwenye kamati kuu mbona simuoni hapa???.....nawaona kina january makamba na wengine wengi?tuko wapi mbunge wa monduli
 
Humu JF kuna vilaza wengi sana wanajaza posts unnecesarily
 
Mkuu msamehe tu huyo kilaza,unajua watu wengine wana ubongo wa kuku

Hapo utakuwa umempendela. Heri ubongo wa kuku maana wao wakiona giza linaingia ubongo wao unawatuma kutafuta sehemu ya kulala. Mie namweka kwenye kundi la chura. Jaribu kumchukua chura, mweke kwenye sufuria yenye maji baridi, then chemsha hayo mpaka yachemke wakati akiwa kwenye hayo maji uone kama ataruka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…