Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Companero... Hao wengine hudandia hoja, hawana muda wa kujifunza zaidi ya kuangalia ya JF na ku-recycle matokeo yake wanaishia kuwa mislead and misinformed

Zakumi anajua sana ila ana chuki binafsi na fikra na utendaji wa Mwalimu Mweledi
 
lipo tatizo kubwa na tatizo dogo; kubwa ni matumizi ya raslimali za serikali kwa ajii ya CCM. Watumishi wanaowahudumia ni wa serikali, vinywaji (I suppose) ni vya serikali n.k Lakini tatizo hili kubwa vile vile linakuja pale ambapo muda wa kazi za serikali unafanywa na kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama kwenye jengo la serikali.

Ukubwa wa tatizo hili unaweza kuja hivi zaidi - kiongozi wa chama cha siasa (sema cdm) anaweza kuitisha kikao cha chama kwenye ofisi ya serikali na kikahudumiwa na raslimali za serikali? NIna u hakika mkubwa watu wengi watakataa kuwa haifai lakini tukifuata mfano wa Rais leo (na ameshawahi kufanya hivyo huko nyuma tukazungumza) jibu ni kuwa kuanzia sasa ni ruhusa kwa viongozi wa kisiasa (bila kujali vyama) kufanya vikao na mikutano yao sehemu zao za kazi. hili ni tatizo kubwa.

Tatizo dogo - nani atamwambia Rais ukweli huu kwa sababu hili linawezekana kwa sababu moja tu - anayefanya hivyo ni Rais; kiongozi mwingine hawezi kufanya hivyo akaachiliwa!

Hili linatuleta kwenye swali jingine angavu: je Rais anaongozwa na sheria/taratibu nyingine ambazo zinafuatwa na viongozi wengine wa umma? Do we have another set of laws zinazompa Rais impunity rais ya kufanya lolote?
 
ccccm.JPG

ccccm1.JPG

JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012

nilisha sema nchi hii hakuna democrasia bali kuna ubakaji wa democrasia ona mambo mengine makamu wa rais akiwa na gari za serikali anagawa kadi za chama sasa na mkuu wa nchi naye tena.kesho kwenye jukwaa anasema amekuza democrasia achane masiala nyie mambo yatakuja kubadirika hapa mnachezea amani.
 
Companero... Hao wengine hudandia hoja, hawana muda wa kujifunza zaidi ya kuangalia ya JF na ku-recycle matokeo yake wanaishia kuwa mislead and misinformed

Nakubaliana na wewe kuwa nadandia tu. Lakini mpaka sasa hamjaonyesha kuwa kitendo kilichofanyika ni kuvunja sheria au utaratibu.
 
Nakubaliana na wewe kuwa nadandia tu. Lakini mpaka sasa hamjaonyesha kuwa kitendo kilichofanyika ni kuvunja sheria au utaratibu.

ukijikita sana kwenye maandiko ya sheria badala ya roho ya sheria hata watuhumiwa wa epa kurudisha fedha bila kushitakiwa utasema ni kitendo cha kawaida tu ndani ya taratibu zetu
 
Zakumi,
Naona Companero ameniwahi. Nyerere alitawala under one party state. Sasa tukubali kuwa tuna multi party na lazima
tubadilike kuendana na hali halisi. Mambo ya serikali yawe ya serikali na ya chama yawe ya chama. Hii ya Obama kuwakaribisha Waislamu kufuturu haina mshiko. Wale Waislamu walikuwa wanachama wa Democratic?

Ngoja nikalale. Naona hii imekuwa therapy sasa.
 
ukijikita sana kwenye maandiko ya sheria badala ya roho ya sheria hata watuhumiwa wa epa kurudisha fedha bila kushitakiwa utasema ni kitendo cha kawaida tu ndani ya taratibu zetu

Jamani najua kabisa Rais Kikwete anatukanwa sana,hiyo mimi hainipi shida.Kwa jambo hili linaloongelewa hapa,yeye ni Rais wa kwanza kufanya hivi,tumwache Nyerere Mkapa alifanya na Mwinyi alifanya.Tujenge utamaduni wa kuthamini utendaji wa watu tusiowapenda si kuwalaumu kwa kila kitu
 
Well, maybe it is time we put this to an end. Mambo ya chama yawe ya chama na ya serikali yawe ya serikali.

Hujasikia hata ziara ya makamu wa rais juzi ilikuwa ya kiserikali ila walikuwa wakiondoa bendera za cdm kitu ambacho kilitudhihirishia alikuwa kichama zaidi na cha kushangaza zaidi hakuna hata chombo kimoja cha habari kiliripoti sijui nao ccm sasa
 
2015 kodi yao ya ikulu inaisha,tunatupa kule!tunawapangisha makamanda wa kazi nao,watuokoe na huu usanii
 
ukijikita sana kwenye maandiko ya sheria badala ya roho ya sheria hata watuhumiwa wa epa kurudisha fedha bila kushitakiwa utasema ni kitendo cha kawaida tu ndani ya taratibu zetu

Unitambua kuwa nipo single-minded. Tusichanganye masuala ya EPA na vikao vya Ikulu.
 
Jamani najua kabisa Rais Kikwete anatukanwa sana,hiyo mimi hainipi shida.Kwa jambo hili linaloongelewa hapa,yeye ni Rais wa kwanza kufanya hivi,tumwache Nyerere Mkapa alifanya na Mwinyi alifanya.Tujenge utamaduni wa kuthamini utendaji wa watu tusiowapenda si kuwalaumu kwa kila kitu

nani kakuambia hatumpendi? hivi kama babu na baba yako walikuwa wanavaa pekosi lazima na wewe uvae pekosi?
 
Unitambua kuwa nipo single-minded. Tusichanganye masuala ya EPA na vikao vya Ikulu.

katika dunia ya sasa lazima ufanye 'lateral thinking', hebu soma tena posti ya mwanakijiji hapo juu kuhusu tatizo kujenga matatizo
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Watanzania wenzangu, tuna lalamila mno hadi hata tukilalamikia mambo genuine tunaonekana hatina point kwa sababu ni kawaida yetu. Inaongeza au kupunguza nini Kamati kuu ya CCM ikikutana ikulu?
 
Back
Top Bottom