Ni halali DOWANS kuuzwa kesi ingali mahakamani?

Ni halali DOWANS kuuzwa kesi ingali mahakamani?

Mwamatandala

Member
Joined
Jul 17, 2009
Posts
44
Reaction score
3
Bado ningali na kigugumizi na sintofahamu baada ya kampuni ya kimarekani symbion kununua mitambo ya dowans.Ninachofahamu,kwa mujibu wa utaratibu wa kimahakama,shauri lolote lililo mahakamani hakuna mtu wala taasisi inayoruhusiwa kulizungumzia wala kuendesha mchakato wowote.kama ni hivyo,kwanini dowans imeuzwa tena utaratibu ukipata baraka kutoka kwa kiongozi wa ngazi ya juu ya serikali ya marekani ambaye alitembelea mitambo hiyo.AU KUNA BAADHI YA WATU WAPO JUU YA SHERIA.?
NAWASILISHA.
 
Hivi iliyouzwa ni DOWANS au mitambo tu ? na yenye kesi ni Kampuni ya DOWANS au ni mitambo na mali zake ? maana sijaelewa mchakato mzima !
 
Mleta mada,kwa kweli watanzania tumeona ajabu sana. Hata mahakama ilitoa amri kuwa dowans isifanyiwe mazungumzo yoyote nje ya mahakama. Kwa ukaidi wa kutosha,dowans wamewarithisha business deal ile ile ya umeme,tena Tanesco na tayari tunaitumia tupende tusipende. Baada ya rais wetu kugundua kuwa mgao umemwendea mkoloni beberu marekani,ameamua kuikaribisha ikulu Symbion ltd ,na mama kilintoni wa marekani kukubaliana! Rais ni mjanja,ukigoma marekani waweza fanya lolote kama kule irak,afghan,n.k. Hawa watu ambao wamenunua mitambo ni mashushu wa marekani. Hapa tuandike mioyon kuwa tumerud kwenye ukoloni. Mpaka sasa hamna mtu yeyote au mwanasiasa yeyote mwenye jeuri la kuipinga marekani,tutulie mamekuja kufanya watakavyo!
 
Hivi iliyouzwa ni DOWANS au mitambo tu ? na yenye kesi ni Kampuni ya DOWANS au ni mitambo na mali zake ? maana sijaelewa mchakato mzima !

mkuu ukumbuke ktk sheria za mikataba mitambo ni yenye substantial interest. Ujue ktk dowans kuingia mkataba subject matter ilikuwa ni umeme na mitambo kwa kuwa umeme usingezaliwa bila mitambo. Vp kama subject matter is frustrated,au non existing,nini kinafuata? Labda utusaidie kupitia Law of contract,cap.345
 
Hii kitu inawezekana kwa Tz, Kesi ya msingi juu ya Dowan na mitambo ipo mahakaman alafu mitambo inauzwa kwa muwekezaji mwingine huku kesi inaendelea. Mahakama zetu pia haziko huru kwanini wasiwaite Symbion mahakamani kwa kuknunua mitambo yenye kesi

Kichekesho zaidi, raisi si alisema hawafahamu Dowan wala Richmond sasa mbona kawapokea Symbion kwanini aiwaulize hiyo mitambo mmenunua kwa nani ili amjue.

Njiiiiiiiiiii hiii itajengwa na wenye moyo sio kikwete
 
Wewe una nguvu ya kuhoji chochote kuhusu DO-ONCE? who are you by the way, unajifanya una uchungu sana na zis cantri ? Kuna mambo mengine mamlaka hazina pingamizi juu yake for your information.
1. Tulia uliwe........
2. Cha msingi tunataka amani na utulivu wakati umeme unawaka.

Sasa kama una hasira zima umeme kwako, sisi tunakusaidia kutatua tatizo wewe unataka haki, haki ipi? yaani tukae gizani kusubiri kesi?

lol --- viva watanzania -- aluta continyuaa --- tutafika tu kwenye nchi yetu ya ahadi ---- isharaaaa.
 
hivi yule jamaa wa chadema alivyoipuuza mahakama walimfanyaje vile?................. nikumbusheni tafadhari................ aaagh, nemesikia na mokiwa juzijuzi hapa naye kuna kitu mahakama ilisema juu yake,................ tukumbushane jamani.............. i am waiting for the same on symbion............
 
labda wataalamu wa sheria watwambie hapa mana almsot watu wengi hatuelewi,na JK bubu ngereja ndio kiroja kingine halafu tunasema ccm wamefanya mengi mazuri,ilhali vitu vingi viko gizani na hakuna maelezo
 
Back
Top Bottom