Ni halali kununua dawa maduka ya nje,na nina bima ya NHIF..kisa hospital niliyotibiwa hizo dawa hamna?

Ni halali kununua dawa maduka ya nje,na nina bima ya NHIF..kisa hospital niliyotibiwa hizo dawa hamna?

ryan riz

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
423
Reaction score
683
Leo nimepata hasira sana,hiv wa mabwanyenye huko juu kwenye uongozi huwa yanatumia akili au ma..alio kufikiri?

Hela ilivyongumu hivi nakatwa mchango wa NHIF alafu nimepanga foleni toka asubuhi mpaka saa 10 jion,majibu yanatoka na andikiwa dawa ila zingine kwenye stoo yao wanasema hamna .

Alafu naambiwa nikanunue nje hii maana yake nini?

Hivi mimi nitajuaje km ugonjwa naumwa ni upi na hosptl dawa zake zipo au hamna..?

Hivi huko ni kukomesha wizi wa madawa au kutukomesha wagonjwa?

Wandugu naombeni utaratibu wa mimi kupata dawa ambazo zimekosekana kituo nilichotibiwa ila ziko kwenye BIMA..
 
Mbona hiyo ni kawaida na tumeshazoea?

Hata watoto wadogo tunaambiwa matibabu ni bure ila ukiempeleka mtoto hospital mara nyingi dawa unaandikiwa ukanunue.

Watanzania tutafika mbinguni tukiwa tumechoka sana
 
Pole sana !! Ukikutana na hali hii unawezafikiri ni kama vile uko kwenye njozi kumbe ndio hali halisi. Sasa unajiluliza maana ya hizi bima ni nini haswa !!
 
Hakika hii nchi ina wamiliki wake wachache na si sisi WANANCHI..
 
Utaratibu uliowekwa kwa walio buni hizo bima ni kwamba walau 95 % kama siyo 100% ya dawa lazima zipatikane kwa huyu mtoa huduma aliyechaguliwa. Ikitokea mtoa huduma hana dawa fulani anatakiwa akuandikie fomu maalum ili hiyo dawa ukaipate kwenye maduka yaliyochaguliwa kutoa hiyo services. But ukija kwenye uhalisia ndiyo Kasheshe sasa..
 
Ndugu sasa hivi wanasema hawaandiki ndio utaratibu waliopewa,sa nikawauliza nifanyaje hili nizipate? Wakanijibu huna jinsi kanunue tu..
Nikawauliza nikienda kupima upya hsptl nyingine? Nikajibiwa hilo nalo haliwezekani..!

Ndugu dawa hizo nimeulizia bei naambiwa elfu 32.. sasa hapa BIMA imenisaidia nn kwa usawa wenyew huu..hii ni hela ya kulisha familia siku tatu..
 
Back
Top Bottom