Danisamweswa
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 453
- 154
Ni halali kwa asilimia 100..askali akikuthibitishia Kuwa umefanya kosa, akakuandikia notification, anaruhusiwa kisheria kukamata Gari hadi pale utakapolipa faini. Ni uamuzi wake kuchukua leseni au kitu chochote hata blue card ili kuenforce payment...
Asante kwa maelezo. Mimi ni dereva mgeni. Nimeingia barabarani si muda mrefu. Endapo polisi ataniandikia notification, ninamlipa hapo hapo yeye mwenyewe au kuna mahali naenda lipia ili kupata risiti?
Sheria ya usalama barabarani,inampa nguvu askari kuchukua "valid driving licence" pindi akisimamisha gari.
Hiyo ndiyo kitu ya kwanza anadai kabla ya yote
Tanzania hakuna utawala wa sheria. PERIOD
akikuandikia notification unaenda kulipa kituo cha polis kwa muhasibu hairusiwi kumpa yy pesa ya faini kabisaaa
hlf leseni haruhusiwi kuchukua ile ni mali yko ww
mi juzi nilitanua wakati naenda home pale karibia buzuruga plaza hamadi hawa hapa..
sikuwa na pesa mfukoni wakataka kuniandika faini wakati huo walikuwa wameshaniomba leseni..
nikawaomba niende home kufuata pesa sikurudi hadi kesho yake asubuhi nikawapigia na kuwapa ten wakarudisha lesieni yangu na mchezo ukaishia hapo
Kama polisi wamekagua gari na kukuta kuna kosa na akaandika notification kisha dereva akashindwa kulipa hela iliyoandikwa kwenye notification. Je ni halali kwa polisi kuchukua leseni ya dereva na kubaki nayo hadi atakapolipa fine aliyotozwa? Jambo kama hilo la kuchukua leseni ya dereva likitokea huyo polisi anapaswa kumpa nini dereva kama anayo safari ya kwenda mbali? Naombeni msaada wa kisheria