Ni halali kwa Polisi kuchukua leseni ya dereva?

Danisamweswa

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
453
Reaction score
154
Kama polisi wamekagua gari na kukuta kuna kosa na akaandika notification kisha dereva akashindwa kulipa hela iliyoandikwa kwenye notification. Je ni halali kwa polisi kuchukua leseni ya dereva na kubaki nayo hadi atakapolipa fine aliyotozwa? Jambo kama hilo la kuchukua leseni ya dereva likitokea huyo polisi anapaswa kumpa nini dereva kama anayo safari ya kwenda mbali? Naombeni msaada wa kisheria
 
mi juzi nilitanua wakati naenda home pale karibia buzuruga plaza hamadi hawa hapa..
sikuwa na pesa mfukoni wakataka kuniandika faini wakati huo walikuwa wameshaniomba leseni..
nikawaomba niende home kufuata pesa sikurudi hadi kesho yake asubuhi nikawapigia na kuwapa ten wakarudisha lesieni yangu na mchezo ukaishia hapo
 
Tanzania hakuna utawala wa sheria. PERIOD
 
Wamezoea. Ungewaletea hela ya moto. Wamezoea kutesa watu.
 
Ata mimi nahitaji jibu mkuu, wanaojua tafadhali
 
Sheria inasemaje kuhusu hilo?wanasheria wasomi tunawaomba mpitie humu
 
Ni halali kwa asilimia 100..askali akikuthibitishia Kuwa umefanya kosa, akakuandikia notification, anaruhusiwa kisheria kukamata Gari hadi pale utakapolipa faini. Ni uamuzi wake kuchukua leseni au kitu chochote hata blue card ili kuenforce payment...
 
Asante kwa maelezo. Mimi ni dereva mgeni. Nimeingia barabarani si muda mrefu. Endapo polisi ataniandikia notification, ninamlipa hapo hapo yeye mwenyewe au kuna mahali naenda lipia ili kupata risiti?
 
Wanalazimisha makosa, yaan wanaboa aisee. Eti kuna crack ya sentimeter 10 kwenye windscreen tena upande wa abilia wanangania ni kosa, nikamuuliza crack inazuia au kusababisha hatari gani? Mara oh ulilinua hivyo, mara usinifundishe kazi.mBAF kabisa
 
Asante kwa maelezo. Mimi ni dereva mgeni. Nimeingia barabarani si muda mrefu. Endapo polisi ataniandikia notification, ninamlipa hapo hapo yeye mwenyewe au kuna mahali naenda lipia ili kupata risiti?

akikuandikia notification unaenda kulipa kituo cha polis kwa muhasibu hairusiwi kumpa yy pesa ya faini kabisaaa
hlf leseni haruhusiwi kuchukua ile ni mali yko ww
 
Sheria ya usalama barabarani,inampa nguvu askari kuchukua "valid driving licence" pindi akisimamisha gari.
Hiyo ndiyo kitu ya kwanza anadai kabla ya yote
 
akikuandikia notification unaenda kulipa kituo cha polis kwa muhasibu hairusiwi kumpa yy pesa ya faini kabisaaa
hlf leseni haruhusiwi kuchukua ile ni mali yko ww

Asante. Kwa hiyo ni kitu gani atachukua toka kwangu kama security ya yeye kunifanya mimi nikalipe hiyo faini?
 
mi juzi nilitanua wakati naenda home pale karibia buzuruga plaza hamadi hawa hapa..
sikuwa na pesa mfukoni wakataka kuniandika faini wakati huo walikuwa wameshaniomba leseni..
nikawaomba niende home kufuata pesa sikurudi hadi kesho yake asubuhi nikawapigia na kuwapa ten wakarudisha lesieni yangu na mchezo ukaishia hapo

Mnawalisha hawa jamaaa kweli nyie wadanganyika aisee
 
Kama polisi wamekagua gari na kukuta kuna kosa na akaandika notification kisha dereva akashindwa kulipa hela iliyoandikwa kwenye notification. Je ni halali kwa polisi kuchukua leseni ya dereva na kubaki nayo hadi atakapolipa fine aliyotozwa? Jambo kama hilo la kuchukua leseni ya dereva likitokea huyo polisi anapaswa kumpa nini dereva kama anayo safari ya kwenda mbali? Naombeni msaada wa kisheria

Hakuna Sheria yyt inayomruhusu POLISI KUCHUKUA LICENSE YA RAIA BILA RUKSA YA MAHAKAMA.

Wakifanyacho hawa askari ni kinyume Cha Sheria ya mamlaka ya Licence Tanzania.
Wananchi LZM watambue kuwa ASKARI SIO MAHAKAMA. na kama kuna Dispute baina ya Askari na Raia basi Ni MAHKAMA PEKEE NDIO YENYE KUTOA MAAMUZI YA MWISHO.

Siku Askari akichukua Leseni yako bila Hukumu ya MAHKAMA Chukua namba yake Ilete humu JF Tumfahamishe Waziri wa mambo ya Ndani na Wizara yake ili Wawatambue hao WAVUNJA SHERIA YA NCHI.
NA KM Hatua kama hizi hazichukuliwi hawa Askari watazidi KUONEA WANANCHI.
 
Je halali askari yeyote wa barabarani kushika leseni ya dereva au ni vehicle traffick anayerusiwa tu?
 
Back
Top Bottom