Ni halali kwa Polisi kuchukua leseni ya dereva?

Sheria ya usalama barabarani,inampa nguvu askari kuchukua "valid driving licence" pindi akisimamisha gari.
Hiyo ndiyo kitu ya kwanza anadai kabla ya yote

Mkuu anapaswa kuikagua na kukurudishia, sio kubaki nayo kama dhamana. Akibali nayo ina maana amekupa kibali cha kuvunja sheria ya barabarani - kuendesha gari bila leseni. Nadhani siku moja nitakapofanyiwa hivyo nitachukua details za huyo askari na kwenda kumfungulia mashataka, yeye, OCD wake, RPC na Waziri wa mambo ya ndani.
 
Inategemea na kosa ulilofanya, ikiwa askari wana kitabu cha notification unaweza kulipa fine hapo hapo, kama hawana kitabu basi malipo ni hadi kituoni, sisitiza kupewa risiti
 
Hawana ruhusa au katika sheria yoyote askari kuchukuaa leseni yako....na endapoo ukikamatwaa ukapigwa faini ndani ya 30dayz inabidi uwee umelipaa hiyooo faini#ndo navojuaa
 
Kuichukua kwa maana gani labda?
Polisi anayo mamlaka kisheria kuomba leseni yako na kuikagua at anytime broda unapokuwa una drive

Ila kuichukua kama dhamana haikubaliki
 
Lakini hapa inabidi tukubaliane jambo moja if at first wewe ndio avunja sheria makusudi kabisaaa basi inabidi uendane na matakwa yake ili wewe upate unafuu.......huu ndio ukweli kwa kila dereva anajua hilo

Mfano umetanua makusudi akakushika hapo ni ama umpe sh elf5 hadi elf10 na kama huna basi atakwambia nachukua leseni ukipata pesa njoo ntakupa leseni
You have a choice komaa akupe leseni akuandikie notification ya elf30 kwa kila kosa atakalolikuta au kumuachia leseni......mind that umetanua mwenye kwa makusudi ukijua ni kosa

Tatizo hapa sio Trafiki tu, tatizo hata sisi madereva
Unafanya makosa makusudi halafu unajifanya kuhoji uhalali, kama hutaki shida ukidakwa kubali immediately unaandikiwa notification kama anakkitabu unalipa cash anakupa lisiti unasepa ukitanua tena unalipa elf30
Na sikuhizi wajuaji wengi kila trafiki ana notification mfukoni hakuna longo longo
 
Kuichukua kwa maana gani labda?
Polisi anayo mamlaka kisheria kuomba leseni yako na kuikagua at anytime broda unapokuwa una drive

Ila kuichukua kama dhamana haikubaliki

Tofautisha KUICHUKUA na KUIKAGUA!

Au kiswahili kwako kigeni?
Manake wahutu pia wamo humu.

Askari HARUHUSIWI KISHERIA KUCHUKUA LESENI YAKO NA KUBAKI NAYO.
Anacho ruhusiwa ni KUKAGUA na Akimaliza HATA KM UNA MAKOSA basi NI LAZIMA AKUTUDISHIE LESENI YAKO.
Akikataa chukua namba yake halafu KAMRIPOTI TAKUKURU kuwa Amechukua leseni yako ILI UKATOE RUSHWA.
Manake HIO NDIO SABABU PEKEE Ya Askari KUCHUKUA LESENI YAKO.
NA Hakuna jingine.
Manake anajua Utaifuata tu. Na ukienda lzm akuombe RUSHWA.
 

Nashukuru sana kwa ufafanuzi huu, kuanzia leo kabla sijaongea na askari bara barani kwanza nitajitambulisha na nitamwomba ajitambulishe kwa jina na namba yake ya kazi nami nitaandika. Akikataa nitajua hana nia njema, hivyo sitampa leseni yangu
 
Maelezo yako yana utata kidogo,sio elfu 30 kwa kila kosa huu ni udhaifu wa watanzania kutokujua sheria ya barabarani ambao hutumiwa na trafiki haijalishi una makosa mangapi faini ni elfu 30 tu.
 

Bill acha kupotosha watu ukiwa na kosa police wanachukua leseni na kumbuka wana hadi mamulaka ya kuifungia hiyo leseni yako kwa kipindi watakachoona inafaa. Nchi nyingine wana utaratibu wa point kila kosa point sijui ngapi na ikifika point fulani wanachukua leseni kwa muda au kama ni makosa makubwa wanachukua jumla inamaana wewe ndo basi tena kuendesha au uanze upya. Tatizo wenye magari tanzania mnajiona mpo juu ya sheria wakati hata sheria hamzijui
 

Mtu asaidie kuweka hiyo document kama picha. Iliandikwa na Saidi Mwema. Mimi natumia simu.
 

Attachments

Ninavyofahamu mimi kwa haya machache mfano.
1) Ukiandikiwa notification unaweza lipia kituo chochote na ukapewa risiti, kingine wengi hawapewi risiti maana wanaotembea barabarani hawana risiti zile sio risiti, risiti zipo kwa mhasibu wao. Cha maana anatakiwa akupe copy ya ile notification ya rangi ya blue(light blue), ile ndio sahihi kupewa kama hana uwezo wa kukupa risiti. Angalizo wale traffic unakuta wapo na gari mf la ocd huwa wanazo risiti halali kwa sababu wengi wanakuwa nje ya mji (barabara za kwenda mikoani).

2) Kama huna leseni na umeisahau kwa bahati mbaya basi kisheria traffic anachukuwa details zako kupitia kadi ya gari na unatakiwa ndani ya masaa 72 (siku 3) uipeleke kwenye kituo chochote cha polisi.

Angalizo, ukiwa unaongea nae ongea kiustarabu na usioneshe kupanic na ukimpatia maelezo hayo atafahamu kuwa unazijua sheria, utaambuliwa kuambiwa mkuu hamna shida ila fanya fanya mpango, hapo hata ukimwambia sina kitu atakuacha. Ukivunja sheria kubali yaishe, kosa kama la kutokuwa na fire extinguisher usikubali kuhonga haswa kama unasafari ndefu maana huwezi kutoa rushwa njia nzima itazd ile elfu 30, andikiwa notification lipia tena hakikisha makosa yanaandikwa yote ili ukikutana na mwingine unamuonyesha then anakuacha maana tayari ushalipia makosa yako.
 
SHERIA inaruhusu polisi kuchukua leseni yako ila nilazima ajaze form itakayo onyesha kuwa kachukua leseni yako form huyo itaonyesha jina lake na cheo chake nasababu yakuichukua pia kupewa notification sheria inasema unatakiwa kuilipa ndani ya siku Saba
Pia tukumbuke kuwa kulipa fine iwe barabarani au kituo cha polisi nikufupisha mlolongo sheria inamruhusu polisi kukushitaki mahakamani.
SHERIA inakataza kuendesha gari bila leseni ndiyo maana anapoichukua leseni yako lazima ajaze form hiyo ndicho kibali chako chakukuruhusu kuendesha gari
 
Msijali sana nimeskia kuna mchakato unataka kuanzishwa wa kulipia makosa barabarani kupitia mobile money kama m-pesa, yani ukishikwa anakuandikia notification then wewe unaingia kwenye menu yako ya mobile money unachagua Traffic (mfano) unathibitisha unakatwa hela (30,000/=) unapokea text yenye confirmation code unampa traffic then ndio inaandikwa kwenye risiti, onyo ikijulikana umefanya udanganyifu inakula kwako maana details za gari wanazo, kingine zinakuwa (IP camera) za barabarani (thanks lord) maana kosa lolote wanaliona kwenye screen zao huko control room na pia foleni zitapungua maana kama kuna gari bovu basi break down watafika haraka zaidi au kama kuna ajali, kikubwa daladala zitakuwa zinaingia kituoni na sio kupakia njiani tena pembeni ya kituo na kuleta foleni za ajabu. Dawa yao inakuja, na traffic wala rushwa pia, bodaboda itakayokatiza kwenye camera za mjini itakula kwake maana hawakukimbizi ila wanachukua namba then wanakutrace mpaka unaporudi kupaki sehemu halali unashangaa hao wamekuja kukukamata.
 
Mbona kama tunapeana mbinu za kupambana na dola tukiwa tumevunja sheria!!!! Maana hayo yote humpata aliyevunja sheria,la ni bahati mbaya.

Tusivunje sheria za barabarani na haya yote hayatatukuta.
 
Mbona kama tunapeana mbinu za kupambana na dola tukiwa tumevunja sheria!!!! Maana hayo yote humpata aliyevunja sheria,la ni bahati mbaya.

Tusivunje sheria za barabarani na haya yote hayatatukuta.

Sio kila wakati tunakuwa tumevunja sheria ndugu. Kuna wakati traffic police anapaswa kukuelimisha, yeye anawaza kukubambikia kosa ili apewe rushwa. Halafu sio kila kosa fine yake elfu 30, sometimes anatakiwa kukupa onyo ila kwa tamaa ya rushwa atakutisha
 
Mbona kama tunapeana mbinu za kupambana na dola tukiwa tumevunja sheria!!!! Maana hayo yote humpata aliyevunja sheria,la ni bahati mbaya.

Tusivunje sheria za barabarani na haya yote hayatatukuta.

We lzm utakuwa muendesha basikeli tu!

Madereva wote wa magari wanatambua kuwa Saa yyt unaweza kusimamishwa na Afande yyt yule na akakagua gari kila kona na akakuta kisheria HUNA KOSA LLT lkn akabumba kosa la kubumba tu akakuchomekea halafu anakwambia kata posho au mikuandikie fain ya elfu 30!

Lkn Askari akifahamu kuwa WEWE unazijua HAKI ZAKO na ukasimama kidedea bila ku panic au kutoa matusi yeye mwenyewe anashika adabu yake.
We ukiona maneno meengi Mwambie tu Twende makao makuu.
Halafu panda mpaka kwa BOSS MKUU WA KITUO umueleze manyanyaso anayokupa huyo paka mwizi! Na umfahamishe kuwa hii kesi isipo tatuliwa unaipeleka kwenye magazeti na TAKUKURU.

Lzm Atie adabu.

Waulize madereva wote mjini watakwambia.
Sio mpaka uwe na kosa ndio wakudake.
Wizi sana hao.
 

Ni kweli kabisa na ikiwa watakuomba hio leseni bado sheria inakuruhusu kuwapatia au kuwaonyesha waione tu sio kuichukia kwa kipindi cha masaa 24, yaani kwa maneno mengine si lazima uendeshe ukiwa Umebeba leseni maana risk ya kuipoteza ni kubwa kuliko kuihifadhi nyumbani na kuiwasilisha siku ikihitajika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…