Ninavyofahamu mimi kwa haya machache mfano.
1) Ukiandikiwa notification unaweza lipia kituo chochote na ukapewa risiti, kingine wengi hawapewi risiti maana wanaotembea barabarani hawana risiti zile sio risiti, risiti zipo kwa mhasibu wao. Cha maana anatakiwa akupe copy ya ile notification ya rangi ya blue(light blue), ile ndio sahihi kupewa kama hana uwezo wa kukupa risiti. Angalizo wale traffic unakuta wapo na gari mf la ocd huwa wanazo risiti halali kwa sababu wengi wanakuwa nje ya mji (barabara za kwenda mikoani).
2) Kama huna leseni na umeisahau kwa bahati mbaya basi kisheria traffic anachukuwa details zako kupitia kadi ya gari na unatakiwa ndani ya masaa 72 (siku 3) uipeleke kwenye kituo chochote cha polisi.
Angalizo, ukiwa unaongea nae ongea kiustarabu na usioneshe kupanic na ukimpatia maelezo hayo atafahamu kuwa unazijua sheria, utaambuliwa kuambiwa mkuu hamna shida ila fanya fanya mpango, hapo hata ukimwambia sina kitu atakuacha. Ukivunja sheria kubali yaishe, kosa kama la kutokuwa na fire extinguisher usikubali kuhonga haswa kama unasafari ndefu maana huwezi kutoa rushwa njia nzima itazd ile elfu 30, andikiwa notification lipia tena hakikisha makosa yanaandikwa yote ili ukikutana na mwingine unamuonyesha then anakuacha maana tayari ushalipia makosa yako.