Ni halali kwenda kutubu dhambi kwa binadamu mwenzako, yaani kuungama?

Akili za kitoto hizi..

Niambie watumwa walioenda uarabuni karne hiyo walipotelea wapi??.

Mbona mataifa mengine, black color wapo hadi sasa...
 
Akili za kitoto hizi..

Niambie watumwa walioenda uarabuni karne hiyo walipotelea wapi??.

Mbona mataifa mengine, black color wapo hadi sasa...
Hakuna mtumwa aliepelekwa nchi za waarabu, waende huko walime nini kwenye jangwa?

Waraabu walikuwa mbele ya muda kama "Mawinga" kwasababu wanaiweza shuruba ya kuishi jangwani, ndio waliokuwa wanawasaka mababu zenu kwa msaada wa wale waafrika waliikuwa wamejipata na kujielewa kama Mtemi Mirambo na jeshi lake la kukamata mababu zenu misituni wakiwakuta wanaishi kama wanyama kwa kula mbegu na mizizi, wanawakamata kama mifugo na kubadilisha na waarabu kwa silaha kama bunduki.

Waarabu wanawaswaga mpaka maeneo ya pwani yaliyokuwa yameendelea miaka hiyo kama Kilwa na Bagamoyo ambapo meli za Wagalatia wenzenu wa Kireno na Kispanyola ndio walikuwa wakileta meli za kupakia watumwa na kuwasafirisha mpaka kwa wagalatia wenzenu huko Marekani ya Kusini na Kaskazini wenye uhitaji mkubwa nguvukazi kwenye mashamba ya pamba.
 

Mungu husamehe dhambi kupitia sakramenti ya ungamo.
Ni ibada kabisa.
Ina process zake.

Biblia inasema
Yakobo 5:16
"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."

Yohana 20:22-23
"Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa."

Kwahiyo sio unaenda kuungama kwa kila mtu. Hapana. Lazima awe kiongozi wa Dini.

Agano la kale.
Wana wa Israel walikuwa wanaenda mbele ya makuhani. Madhabahuni. Wakiwa na sadaka.
Either mnyama (damu -kwa kuchinja) au mazao. Na wanakiri kutenda dhambi na Kuhani anaweka mkono juu ya ile sadaka na kukuombea ondoleo la dhambi.

Baada ya Yesu. Hatumwag damu tena ili kuondoa dhambi maana Damu ya Yesu imetosha pale msalabani.

Mathayo 26:28
“Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”

Pia unaweza kukiri makosa . Kimoyo moyo au kwa saut mbele ya kiongozi wa dini, na kiongozi anakuongoza ungamo la toba. Na kukutakasa.

Yesu anawaambia wanafunz wake
Mathayo 18:18
“Amin, nawaambieni, chochote mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na chochote mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni.”

Mathayo 10:1
“Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwatoa, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu.”
 
Hii ungamo la kikristo ni gumu.
Linafanya mtu kabla ya kukata roho aitiwe Kiongozi wa Dini ili amuongoze kwenye ibada ya ungamo la dhambi.

Kwa waislam ni tofauti.
Unaweza kufanya madhambi ila kabla ya kukata roho ukiomba toba (ukiwa mwenyewe,sehem yoyote) unasamehewa na kuingia peponi.
 
Duuh Maajabu hayo.
Utaendaje kutubu kwa Binadamu mwenzio ambaye yamkini nayeye ana madhambi yake? Tena ati wamtajia hayo madhambi🤣, Dini ya ajabu hiyo
 
Wewe mbona unapeleka kuku kwa mganga na kufata masharti yake. Ina maana yule ni Mungu wako au?
 
Duuh Maajabu hayo.
Utaendaje kutubu kwa Binadamu mwenzio ambaye yamkini nayeye ana madhambi yake? Tena ati wamtajia hayo madhambi🤣, Dini ya ajabu hiyo

Viongozi wa Dini ni chombo tu. Na sio wao ndio wanaosamehe dhambi.
Ila anakuongoza kwenye ibada ya ungamo la dhambi.

Kwa wakatoliki , mtu anakiri dhambi, anapata ushauri wa kiroho, na anapokea tamko la msamaha kutoka kwa Mungu kupitia padri.

Viongozi wa Dini hawasamei dhambi.

Ila wanasema "kama ungamo hili ni la kweli na umetaka kwa moyo mmoja msamaha wa dhambi, Mungu kwa rehema yake ametusamehe dhambi zetu".

Pia ukikiri dhambi .kujutia. kuziacha na ukiungama kwa roho na kweli hata ukiwa mwenyewe Mungu anakusamehe dhambi.
 
kwenda kufanya kitubio yaani ukamwambia Padiri makosa yako yote uliyomkosea Mungu kama kuzini,kuiba halafu baadaye akakwambia nimekusamehe
acha upotoshaji mkuu, unaiwasilisha hoja yako kwa kuifanya ionekane ni dhaifu. una uhakika padre anakwambia nimekusamehe?
 
Nawakilisha jamani tumeona watu wakiungama mfano Kanisa katoliki yaani mtu anaenda kuungama kwa padri na kusamehewa dhambi zake hivi hii imeakaje?
Hata rafiki kipenzi changu Tundu Lissu simba wa yuda naye huwa anaungama samahani lakini
Toka lini padri akasamehe dhambi za mtu!?
 
Hapana hiki ni kizazi cha kuhoji hakiwezi kuyaacha mambo yapite tunaitaji kulijadili hili
Wewe ni mpagani, ni mkristo au muislam? Kama ni mkristo huwezi kuuliza maana utakuwa unajua Yesu alisema nini kuhusu kuondolewa dhambi. Kama ni mpagani au muislam, haikusaidii chochote hata ukiimbiwa, kwa sababu siyo imani yako, hilo halikuhusu.
 
Kwakuwa dini na Mungu/ Miunggu ililetwa na binadamu, basi ni halali kabisa kwenda kutibu dhambi Kwa Binadamu mwenzio.
 
Akili za MTU mweusi,watu wanatengeneza, AI, EV,(gari za umeme), bslistic missile, Magari, ndege, wewe unawaza dini! Basi nenda kazungukd jiwe Mecca, na kulipiga mawe,
🤣🤣 watu wanatengeneza, AI, EV,(gari za umeme), bslistic missile, Magari, ndege, wewe unawaza dini!
🤣🤣 Kunywa bia nakuja kulipa mkuu
Mtu anakesha nyumba ya ibada wenzetu wako bize nwanafanya mambo ya kuonekana
 
Sometimes huwa najiuliza, kwa nini mnapenda kufuatilia dini ambayo siyo yenu... Au ndo dalili zenyewe za kutokuwa na akili kichwani?? 🤔 🤔 🤔
🤣🤣 Usitufokee Sasa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…