Ni halali kwenda kutubu dhambi kwa binadamu mwenzako, yaani kuungama?

Mathayo 16:18
Nami nakuambia, wewe ndiye Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

Kanisa limepewa Mamlaka ya kufunga na kufungua!

KWANINI WAKATOLIKI TUNAUNGAMA DHAMBI ZETU KWA PADRE?

Pengine umewahi kuulizwa swali hili au umewahi kujiuliza: hapa ni maelezo yatayokusaidia kuelewa sababu na uhalali wa jambo hilo.
Hapa tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipotoa amri hiyo kwa mitume wake akisema;
"Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungiwa dhambi wamefungiwa"(Yohane 20:22-23).
Na huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa kanisa wa mitume.
"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa"(Yakobo 5:16a)
Ni miongoni mwa maagizo msingi kabisa ambayo hatuna mamlaka kuyabadili labda Yesu mwenyewe aliyeagiza hivyo aje mwenyewe kuyabadilisha.
Mungu anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa msamaha huo,sisi tu nani tumpangie njia ya kutoa msamaha huo na kujipangia njia zetu?je tunamfundisha Mungu kazi?
Inashangaza siku hizi kusikia kwamba hata baadhi ya wakatoliki wameanguka katika mtego huu wa kutaka kubadilisha agizo hili la Yesu na inashangaza ni kwanini wanataka kurahisisha mambo kiasi hicho.
Mungu hafanyi kazi zake hewani bali huzifanya kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba msamaha tunategemea kusikia maneno kama vile "nimekusamehe",hutaka kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi amekusamehe.
Yesu kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo,alilitumia yeye mwenyewe akiwa binadamu(Luka 7:48).
Luka 7:48
"Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako"
na alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya kibinadamu,ndio maana aliwaachia binadamu baada ya kifo chake ili waendeleze kazi hiyo.
Kuondolea watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu(Marko 2:10),ni pamoja na kazi hiyo aliwaachia mitume wake(Yohane 20:23).
Tukilinganisha na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana,tunaweza kujifunza kwamba tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali ya toba na majuto(Luka 22:61-62).
Luka 22:61-62
"Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana 'leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu' hapo akatoka nje,akalia sana."
Hivyo bado tunadaiwa kuungama iki kuondolewa dhambi zetu(Yohane 21:15-17)
Chakushangaza ni kwamba,Wakristo wote tunaamini kwamba Sakramenti ya ubatizo inatuondolea kabisa dhambi ya asili na dhambi zote zikizowahi kutendwa na yule anayebatizwa na kwa kawaida huwa hatujibatizi wenyewe wala hatubatizwi moja kwa moja na Mungu moja bali hubatizwa na wanadamu wenzetu.
Sasa kama huyu mwanadamu mwenzetu anatubatiza na anatuondolea dhambi ya asili na wote tunasadiki hivyo iweje tukija kwenye kitubio tunapinga ushiriki wa binadamu mwenzetu na wakati matokeo yanayotarajiwa katika sakramenti hizo ni yaleyale kama ya ubatizo.
Iweje aliyekubatiza na kukuondolea dhambi ya asili na ukaamini kwamba amekuondolea ashindwe au ushindwe kusadiki ushiriki wake katika kitubio?
Iweje akisema "Nakubatiza kwa JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU" hiyo iwe sahihi lakini akisema "Nakuondolea dhambi zako KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU" iwe sio sahihi?
Sasa huoni kama unajipinga na kujichanganya mwenyewe hapo?
Wapendwa,tuache kutafuta visingizio visivyo na ukweli kwaajili ya kutaka kupindisha ukweli.
Anayekuondolea dhambi ni Mungu mwenyewe kupitia kwa wapakwa mafuta wake yaani mapadre ambao amewaweka mwenyewe kwaajili ya huduma ya kanisa lake.
Wengine hudai pia kwamba ni watu wote waliopewa jukumu hilo na sio mapadre pekee,lakini ni vizuri kwanza kabla hujajitetea kwa msimamo huo dhaifu uchunguze tofauti iliyopo kati ya "Wanafunzi" na "wafuasi" kisha usome Biblia yako na kuona je jukumu hilo Yesu aliwatamkia wanafunzi wake au aliwatamkia wafuasi wake.
Wanafunzi wa Yesu ni wale kumi na wawili walioandamana naye.
Wafuasi ni wale makutano wengi waliokuwa wakimfuata kwaajili ya kusikiliza mafundisho yake.
Ikumbukwe kwamba Yesu hakusema mambo yote hadharani mbele ya makutano,baadhi ya maagizo msingi kama haya aliwachagua watu maalum kwaajili ya kuwapa kazi hizo na Biblia inasema aliwaita faragha peke yao na kuwapa maagizo hayo.
Mungu awabariki.

TUMSIFU YESU KRISTO!
 
Duuh Maajabu hayo.
Utaendaje kutubu kwa Binadamu mwenzio ambaye yamkini nayeye ana madhambi yake? Tena ati wamtajia hayo madhambi🤣, Dini ya ajabu hiyo
Mbona haushangai kuna mwanadamu mwenzako anaitwa 'Sheikh' anasimama na kuhubiri mbele ya wanafamu wenzake kana kwamba yeye ni Mungu? 😀
 
Hakuna mtumwa aliepelekwa nchi za waarabu, waende huko walime nini kwenye jangwa?

Waraabu walikuwa mbele ya muda kama "Mawinga" kwasababu wanaiweza shuruba ya kuishi jangwani, ndio waliokuwa wanawasaka mababu zenu kwa msaada wa wale waafrika waliikuwa wamejipata na kujielewa kama Mtemi Mirambo na jeshi lake la kukamata mababu zenu misituni wakiwakuta wanaishi kama wanyama kwa kula mbegu na mizizi, wanawakamata kama mifugo na kubadilisha na waarabu kwa silaha kama bunduki.

Waarabu wanawaswaga mpaka maeneo ya pwani yaliyokuwa yameendelea miaka hiyo kama Kilwa na Bagamoyo ambapo meli za Wagalatia wenzenu wa Kireno na Kispanyola ndio walikuwa wakileta meli za kupakia watumwa na kuwasafirisha mpaka kwa wagalatia wenzenu huko Marekani ya Kusini na Kaskazini wenye uhitaji mkubwa nguvukazi kwenye mashamba ya pamba.
Ujio wa Sultan Seyyid Said kutoka Muscat Oman katika kisiwa cha Zanzibar mwaka 1840 unaelezwa kuwa ulichochea kukua kwa biashara ya utumwa kutokana na ongezeko la uhitaji wa nguvu kazi ya mwanadamu katika kilimo cha karafuu ambacho aliakianzisha kisiwani humo.

Waafrika (hasa kutoka Afrika magharibi na Mashariki na Kati) walipelekwa kuuzwa:​

🔹 Mashariki ya Kati ya Asia:
  • Arabia (Saudi, Yemen, Oman)
  • Iraq, Syria, Jordan
  • Iran
  • Asia:
  • India
  • Pakistan
  • Persia (Iran ya kale)
👉 Hii ilijulikana kama Arab/Indian Ocean Slave Trade.

1. Watumwa hasa Wanaume wote waliotoka Africa walihasiwa (castration)🫢😓
2. Wanaume wengi walihasiwa
Walifanywa:
  • Walinzi wa majumba (eunuchs)
  • Watumishi wa kifalme
  • Wengi walikufa wakati wa kuhasiwa (hakukuwa na tiba)
👉 Hakukuwa na kizazi cha wanaume weusi kuendelea kuishi Uarabuni

👱 Wanawake:​

Wake wa ziada (concubines)
Watumishi wa ndani
Baadhi waliingizwa kwenye ndoa
Watoto nao walifanywa:
  • Watumishi
  • Askari
  • Wengine walichukuliwa mapema wakapoteza kabisa utambulisho

Kwa nini Uarabuni hakuna weusi hadi leo​

  • Hakukuwa na kizazi​
  • Wanaume wengi walihasiwa → hakuna kuzaa​
  • Tofauti na Amerika ambako watumwa waliweza kuzaa​
  • Kuchanganywa na kufutwa utambulisho​

Wanawake weusi:​

Walizaa na Waarabu
Watoto walihesabika kama Waarabu, si Waafrika

Hivyo Rangi ikapotea kizazi baada ya kizazi Kwa miongo mingi, ndio maana Hadi Leo rangi ya chotara haipo kabisa uarabuni

Uarabuni:​

Hakukuwa na uhuru wa kujenga jamii za kujitambua

Nchi nyingi za Kiarabu, Hazifundishi historia hii
Hakuna makumbusho makubwa ya utumwa wa Kiafrika
Maana wakifundisha waarabu wengi wataanza kufatilia nasabu zao na Koo zao mwisho wakute Wana damu za kiafrika

Mfano:​

Afro-Arabs (Oman, Saudi, Iraq)
Zanzibar.
Waarabu walikua makatili sana. Hata hapo mji wa bagamoyo walikua wanauwa wale watumwa ambao wamekosa wanunuzi kwa kigezo kwamba wakibaki pale watachafua mji.
 
🤣🤣 Usitufokee Sasa mkuu
Yani utakuta sheikh yupo mbele na 🎤, anakashfu kuhusu ukristo, sasa unajiuliza lengo ni kupinga dini za wengine au kufundisha mambo ya munyazi-mungu.

Akizungumza kuhusu dini yake namna itakavyo saidia waumini wake kwenda mbinguni kuna shida gani? 😁 😄 😄.
 
Mathayo 16:18
Nami nakuambia, wewe ndiye Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

Kanisa limepewa Mamlaka ya kufunga na kufungua!

KWANINI WAKATOLIKI TUNAUNGAMA DHAMBI ZETU KWA PADRE?

Pengine umewahi kuulizwa swali hili au umewahi kujiuliza: hapa ni maelezo yatayokusaidia kuelewa sababu na uhalali wa jambo hilo.
Hapa tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipotoa amri hiyo kwa mitume wake akisema;
"Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungiwa dhambi wamefungiwa"(Yohane 20:22-23).
Na huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa kanisa wa mitume.
"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa"(Yakobo 5:16a)
Ni miongoni mwa maagizo msingi kabisa ambayo hatuna mamlaka kuyabadili labda Yesu mwenyewe aliyeagiza hivyo aje mwenyewe kuyabadilisha.
Mungu anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa msamaha huo,sisi tu nani tumpangie njia ya kutoa msamaha huo na kujipangia njia zetu?je tunamfundisha Mungu kazi?
Inashangaza siku hizi kusikia kwamba hata baadhi ya wakatoliki wameanguka katika mtego huu wa kutaka kubadilisha agizo hili la Yesu na inashangaza ni kwanini wanataka kurahisisha mambo kiasi hicho.
Mungu hafanyi kazi zake hewani bali huzifanya kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba msamaha tunategemea kusikia maneno kama vile "nimekusamehe",hutaka kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi amekusamehe.
Yesu kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo,alilitumia yeye mwenyewe akiwa binadamu(Luka 7:48).
Luka 7:48
"Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako"
na alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya kibinadamu,ndio maana aliwaachia binadamu baada ya kifo chake ili waendeleze kazi hiyo.
Kuondolea watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu(Marko 2:10),ni pamoja na kazi hiyo aliwaachia mitume wake(Yohane 20:23).
Tukilinganisha na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana,tunaweza kujifunza kwamba tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali ya toba na majuto(Luka 22:61-62).
Luka 22:61-62
"Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana 'leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu' hapo akatoka nje,akalia sana."
Hivyo bado tunadaiwa kuungama iki kuondolewa dhambi zetu(Yohane 21:15-17)
Chakushangaza ni kwamba,Wakristo wote tunaamini kwamba Sakramenti ya ubatizo inatuondolea kabisa dhambi ya asili na dhambi zote zikizowahi kutendwa na yule anayebatizwa na kwa kawaida huwa hatujibatizi wenyewe wala hatubatizwi moja kwa moja na Mungu moja bali hubatizwa na wanadamu wenzetu.
Sasa kama huyu mwanadamu mwenzetu anatubatiza na anatuondolea dhambi ya asili na wote tunasadiki hivyo iweje tukija kwenye kitubio tunapinga ushiriki wa binadamu mwenzetu na wakati matokeo yanayotarajiwa katika sakramenti hizo ni yaleyale kama ya ubatizo.
Iweje aliyekubatiza na kukuondolea dhambi ya asili na ukaamini kwamba amekuondolea ashindwe au ushindwe kusadiki ushiriki wake katika kitubio?
Iweje akisema "Nakubatiza kwa JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU" hiyo iwe sahihi lakini akisema "Nakuondolea dhambi zako KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU" iwe sio sahihi?
Sasa huoni kama unajipinga na kujichanganya mwenyewe hapo?
Wapendwa,tuache kutafuta visingizio visivyo na ukweli kwaajili ya kutaka kupindisha ukweli.
Anayekuondolea dhambi ni Mungu mwenyewe kupitia kwa wapakwa mafuta wake yaani mapadre ambao amewaweka mwenyewe kwaajili ya huduma ya kanisa lake.
Wengine hudai pia kwamba ni watu wote waliopewa jukumu hilo na sio mapadre pekee,lakini ni vizuri kwanza kabla hujajitetea kwa msimamo huo dhaifu uchunguze tofauti iliyopo kati ya "Wanafunzi" na "wafuasi" kisha usome Biblia yako na kuona je jukumu hilo Yesu aliwatamkia wanafunzi wake au aliwatamkia wafuasi wake.
Wanafunzi wa Yesu ni wale kumi na wawili walioandamana naye.
Wafuasi ni wale makutano wengi waliokuwa wakimfuata kwaajili ya kusikiliza mafundisho yake.
Ikumbukwe kwamba Yesu hakusema mambo yote hadharani mbele ya makutano,baadhi ya maagizo msingi kama haya aliwachagua watu maalum kwaajili ya kuwapa kazi hizo na Biblia inasema aliwaita faragha peke yao na kuwapa maagizo hayo.
Mungu awabariki.

TUMSIFU YESU KRISTO!
milele amina
 
Back
Top Bottom