Kutokana na mapenzi ya mtu ikiwa wampendaye akihama chama,akifa au kushindwa uchaguzi chama kitatetereka kutokana na kusujudu mtu na si katiba,misingi na itikadi. Hii ni kwa vyama vya upinzani lakini Ccm wao baadhi kujifanya wafuasi wa mtu ni kujipendekeza ili wapate teuzi na chakula na Ccm inanufaika na dola kwahiyo si rahisi kutatereka.Mf baada ya kupita uchaguzi wa mwenyekiti taifa Chadema waliyokuwa wafuasi wa mtu na waandikaji na wakosoaji wakubwa wa serikali wamepowa sana mfano Martin Maranja Masese,Boni yai.
Hawa ni Watafuta Fursa .
Yaani ni kama Wakoloni .Leo mtu anaweza anadhani kuwa wakoloni walikua ni Waarabu na Wajerumani na Waingereza peke yao kumbe Kuna Wabelgiji,Wareno ,Wautaliano na Wafaransa.
Hao ni binadamu wenye hulka ya kutafuta mali kwa namna yoyote bila kujali haki na utu.
Ni wazi kabisa sasa kuwa Sio wapinzani wote wanania ya dhati ya kuwakomboa watanzania bali wengi ni wafanyabiashara waliojipenyeza kwenye siasa kwaalengo ya kujilimbikizia mali kwa Haraka.
CCM kilikua ni chama cha wakulima na wafanyakazi .
Leo CCM ni Chama cha Matajiri na machawa .
Yaani matajiri wanaweka mtu wao halafu wanatoa pesa kuwapa machawa ili wampatie mafuta yanayonukiaam ili kuondoa harufu ya ufisadi .
Hali kadhali Chadema kuna watu walikua wanaona fursa ya kuwa wapinzani kwa gharama za maisha ya watu . Yaani kakikundi kadogo kadiko na huruma na watu kamikua kanafanya shughuli zao kwa mgongo wa chama .
Sasa kushindwa kwao ni tatizo kwao na sio chama kwa sababu kwa sasa chama kinatakiwa kijipange na uchaguzi ujao japo Chadema limekua kikifanya makosa makubwa wana ya kiufundi bila kuangalia mambo kwa jicho la mabili zaidi . Mfano leo ni siku ya Mwisho ya kujiandikisha kupiga kura na kuhakiki . Cha ajabu Chadema hakikuhamasisha wananchi na wanachama na wapenzi wa Chadema kujiandikisha.
Athari yake ni kuwa Hata Ikiundwa katiba mpya na tume huru kesho CCM itashinda maana wanachama wake wengi wanajiandikisha kwa sababu wengi ni watu wazima wenye makazi parmanent.Chadema ilitakiwa iwakumbushe vijana kujiandikisha kwa wingi ili wajiandae kwa miaka au mwaka ambao watamua kugombea .