Ni hatari sana kwa maskini na taifa matajiri wanapokuwa karibu sana na watawala

Ni hatari sana kwa maskini na taifa matajiri wanapokuwa karibu sana na watawala

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
2,471
Reaction score
3,768
Nimesthushwa sana humu jukwaani wanaoshabikia michango inayoitwa ya matajiri kukifadhili chama cha mapinduzi.

Ukweli ni kwamba tajiri hata mara moja hata kwa bahati mbaya hajawahi kuwa na mapenzi mema kwa maskini

Siku zote huwaza namna ya kumtumikisha na kumakuma huyu maskini hadi tone lake la mwisho la jasho.

Mara zote akili ya matajiri ni kuiteka serikali na kuiweka mifukoni mwao halafu wao hufanya kila litakalowanufaisha bila kujali nani kaumia.

Kwa kuona tu lile zoezi malofa wa nchi hii walipaswa kujihurumia na kujihakikishia kwamba tutalia sana kipindi kijacho.

Siku zote ilitakiwa serikali isimame katkati ili kuweka mizania pale ambapo maskini wanaonewa.
Sasa pale tumeshuhudia jitihada za kuwauzia matajiri madaraka.
 
Baada ya Polepole kuwachokonoa, naona Wahuni wameamua kujitokeza hadharani na kuonesha jeuri yao ya pesa za ufisadi na upigaji dili.
 
Back
Top Bottom