Kosa tulilolifanya hasa kwa sisi tulioandikisha vitambulisho 2017 na 2018 ni kutokuweka ushahidi wa ufuatiliaji wa vitambulisho.Nadhani kulitakiwa kuwepo na sehemu ya kusaini kila ukienda ofisi zao kuwa ulifika ila kitambulisho bado.Mfano mimi toka 2017 nilijiandikishia Nyamagana Mwanza nikaambiwa nitachukua kitambulisho NYABULOGOYA,nimeenda mwanza kila mwaka toka 2017 hadi 2023,mwaka 2024/25 ndio sijaenda likizo Mwanza.Muda wote nilipoenda Ofisi za kata Nyabulogoya naambiwaA vitambulisho bado,nilikuwa nawambia ninaishi mbali nawaachia namba za simu lkn huu ni mwaka wa 9 sijawahi kupigiwa simu wala kutumiwa sms,sasa hapo makosa ya kutopata kitambulisho mpk sasa ni yangu au ya serikali?Inamaana mimi kila mara niende mwanza tu bila sababu kila mwaka kwa ajili ya kitambulisho?Anyway mwaka huu nikipata likizo naenda kujaribu mara ya mwisho,nikikuta bado itabidi kusubiri utaratibu mwingine wa serikali juu ya wahanga wa vitambulisho NIDA kwa uzembe wao