Mbona wengine tunarudishwa kirahisirahisi?Nina Ndugu Yangu Alijiandikisha December 2024,Mwaka Huu January 2025 Kapata Number Ya NIDA
April Kuna Family Friend Alikwenda NIDA
Akakuta Kimeshatengenezwa
Hakuwa Na SMS, Mlengwa Alipojulishwa Na Jirani Kuwa NIDA Kuna Kitambulisho Chako
Akaenda Bila SMS ya Kuitwa Lakini Wakampa Chap
Ndio nashangaa yaani wengine tunarudishwa kirahisi na mikwala ya kishambahao wafanyakazi wa nida unaweza kusema wameyapatia maisha kumbe mafukara tuMbona wengine tunarudishwa kirahisirahisi?
Hawawezi kutoa hao mbwaMimi maoni yangu NIDA itoke siku Ile Ile kama ilivyo KADI ya mpiga kura
Kweli kabisa na inawezekana, kwani muhusika anakuwa ameshamaliza mchakato mzima wa kupata hiyo Nida.Mimi maoni yangu NIDA itoke siku Ile Ile kama ilivyo KADI ya mpiga kura
Nami nilikubwa na tatizo kama lako uzuri ni kwamba wakati wa kuandikisha na kupigwa picha nilipewa kabisa namba yangu, ila baada ya miaka 7 au 8 mwaka jana mwezi wa tisa vitambulisho vyote vya zamani vilipelekwa kwenye kata husika ya mwenye nacho na tukataarifiwa kuvifuata na tukapewa.Kosa tulilolifanya hasa kwa sisi tulioandikisha vitambulisho 2017 na 2018 ni kutokuweka ushahidi wa ufuatiliaji wa vitambulisho.Nadhani kulitakiwa kuwepo na sehemu ya kusaini kila ukienda ofisi zao kuwa ulifika ila kitambulisho bado.Mfano mimi toka 2017 nilijiandikishia Nyamagana Mwanza nikaambiwa nitachukua kitambulisho NYABULOGOYA,nimeenda mwanza kila mwaka toka 2017 hadi 2023,mwaka 2024/25 ndio sijaenda likizo Mwanza.Muda wote nilipoenda Ofisi za kata Nyabulogoya naambiwaA vitambulisho bado,nilikuwa nawambia ninaishi mbali nawaachia namba za simu lkn huu ni mwaka wa 9 sijawahi kupigiwa simu wala kutumiwa sms,sasa hapo makosa ya kutopata kitambulisho mpk sasa ni yangu au ya serikali?Inamaana mimi kila mara niende mwanza tu bila sababu kila mwaka kwa ajili ya kitambulisho?Anyway mwaka huu nikipata likizo naenda kujaribu mara ya mwisho,nikikuta bado itabidi kusubiri utaratibu mwingine wa serikali juu ya wahanga wa vitambulisho NIDA kwa uzembe wao