Ni huduma gani nchini haijajaa malalamiko ambayo tunaweza kusema kwa 90% serikali imetenda?

Ni huduma gani nchini haijajaa malalamiko ambayo tunaweza kusema kwa 90% serikali imetenda?

Kwa hili naipongeza serikali na aliyekuja na ishu ya REA
Chanzo cha REA ni changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa Millennium Development Goals. Changamoto hizo zikapelekea kuanzisha mfuko wa Millennium Challenge Account. Zote ni akili za wazungu.
 
Lucas Mwashambwa akiulizwa hili swali kwanza atalia, yani machozi yatabubujika, kisha atayafuta na shati lake la kijani.... Halafu sasa ataanza kummwagia mama sifa zisizo na mwisho.
 
Goli la mama, hela hailali mzigo unakuwa uwanjani kabisa.
 
Hii ni kweli kabisa, tuko vizuri sana hapa kiasi kwamba hakuna fisadi anayedakwa hata mmoja😂😂😂🤣
Wadake ufisadi je chadema watadakwa na nani tuna maviongoz takataka kbs yan chadema ndo adui si ufisadi ujinga na umaskini
 
Wakuu,

Ni huduma gani ambayo tunaweza kusema kwa 90% na kuendelea kuwa serikali imetimiza? Yaani hata mtu akilalamika tutasema hapa ni roho mbaya tu ya watu kulalamika lakini huduma ni nzuri?

Si kwa huduma za 'bure' wala ambazo tunachangia ambazo zimefanywa kwa ufanisi. Kote kumejaa makando kando lukuki.

Na hii yote inatokana na rushwa, kila mradi 10% zinakatwa, bado hujahonga mpaka mlinzi kuhakikisha unapata tenda, na Rais Samia ulishabariki hili ulipowaambia wale kwa urefu wa kamba zao. Ndio maana hata hawajali wananchi wanapata huduma gani.

Halafu mnataka tuwaonee huruma watu kama Chalamila ambao wote ni mnyororo huo huo unafanya huduma ziko mbaya kila sehemu?

Ni huduma gani ya bure inatolewa kwa ufanisi tuseme hapa wananchi tupunguzie mzigo serikali kwa kuchangia kiasi fulani cha pesa tupate huduma nzuri?

Kuna watu wanapiga billions of money na hawachukuliwi hatua halafu mnakuja kushupaza shingo na kusema wajawazito wanatakiwa kulipia huduma, shame kabisa nyinyi.

GePG
 
Back
Top Bottom