hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
Ni huzuni kuu kwa Hamas na washirika wake na ni furaha kwa Israeli na washirika wake
Siku 5 zilozipita Netanyahu alitangaza mauaji (assasination) ya viongozi wa Hamas na Hezbollah.
Leo IDF wamemuua kiongozi mkuu wa Hamas pamoja na majenerali kadha wa kadha wa Hamas. Yahya Sanwar ameongoza Hamas kwa miezi miwili na siku 17 tu baada ya kuuliwa aliyekuwa kiongozi wa Hamas, Ismail Haeney katika jiji la Tehran.
Herzi Halevi ndio ameongoza operation ya kumuua kiongozi mkuu wa Hamas
Herzi Halevi mkuu wa majeshi wa Israeli kushoto pichani akitoa maelekezo akiwa kwenye eneo la tukio alipouliwa Yahya Sinwar huko Rafah-Gaza. Hivyo madai kwamba aliuliwa na Hezbollah kwa drone ni ya uongo, yalienezwa na mwandishi wa kipropoganda katika mtandao wa X.
Netanyahu
Amewapongeza wanajeshi wake kwa kumuua kiongozi wa Hamas. Vilevile kasema bado makusudi yao hayajakamilika, mchakato unaendelea. Akaongeza kwamba hii ni hatua ya kuelekea amani kwa mashariki ya kati kwa kuondoa mihimili ya uovu na kwamba mihimili ya waovu (axis of evils) wategemee mapigo zaidi. Akiendelea kusema, kwamba Hamas haitatawala Gaza tena, hivyo wana Gaza wajifungue mikononi mwa Hamas.
Marekani
Imeunga mkono mauaji ya Yahya Sinwar. Na kupitia Kamara Harris, makamu wa rais wa Marekani, imetangaza kwamba kifo cha Sinwar ni hatua muhimu ya kukomesha vita vya Gaza. Na Biden amesema hii ni fursa kwa Gaza pasipo uwepo wa nguvu ya Hamas.
Kuhusu viongozi wa Hezbollah
Kwasasa Mossad na IDF wapo bize kumwinda Naim Qassem, kaimu kiongozi wa Hezbollah na majemedari wake wawili waliobakia ambao ni: Talal Hamieh na Abu Al Reda. Hivyo hadi sasa Hezbollah imebakiwa na viongozi watatu wakuu. Juu ya Hashem Safieddine ambaye alitegemewa kuchukua kiti cha Hassan Nasrallah, toka october 3 mawasiliano yake yalipotea baada ya shambulio zito katika ngome ya Hezbollah kusini mwa mji wa Beirut. Israeli inasema walimuua kwa shambulio hilo. Na Hezbollah nao walikiri kupoteza mawasiliano na kiongozi wao. Ila kuna nyepesi nyepesi kwamba alihamishwa na kupelekwa Tehran haraka baada ya majasusi wa Iran kuwakamata wavujishaji siri kwa Mossad ambao ni viongozi wakubwa wa Iran ambao walikuwa wanaipa taarifa Mossad walipo viongozi wa Hezbollah na mambo mengine ndani ya Iran. Hivyo muda ni majibu.
Israeli dhidi ya Iran
Israeli muda wowote kuanzia sasa itaishambulia Iran kulipiza kisasi cha october 1 iliposhambuliwa kwa zaidi ya makombora 200 toka Iran. Inasemekana wanaweza kufanya moja wapo ya mambo haya:
1) Kumuua Esmail Qaani, mkuu wa majeshi ya Iran na baadhi ya waandamizi wake. Qaani amekuwa mstari wa mbele kwa kuitishia Israeli na kuionya. Akiiahidi Israeli mabaya na kichapo ama kuifuta kabisa.
2) Kulipua vinu vya nyuklia vya Iran, ingawa Marekani imeonya lakini Israeli wamesema wataamua kulingana na maslahi ya taifa lao.
3) Kuharibu kambi za kijeshi na miundo mbinu ya kitaifa.
Tusubiri tuone, lakini mpango uliopo ni kuiangusha serikali ya Ayattollah baada ya kuvunja Hezbollah na Hamas (Iran proxy armies). Hivyo wanaivuta taratibu ili ijae kwenye 18 zao. Iran ametambua hilo na ametangaza hayupo tayari kwa vita labda kama atachokozwa. Pia wametuma ujumbe katika umoja wa Ulaya na UN kuonesha kwamba wamechagua njia ya amani na si vita. Iran wameilaumu Marekani kuisapoti Israeli dhidi yake, hivyo imejitoa kwenye mazungumzo ya nyuklia na Marekani. Kwa hapa nasimama na Iran, maana njia ya amani ni bora kuliko vita.
Hii vita usiiombee
Na Jeff Massawe