Kuondoa mapema mawazo ya kuajiriwa serikalini kwenye kichwa cha mtoto ni ukombozi muhimu utakaosaidia asipoteze muda hapo baadae. Natamani mimi wakati nasoma ningeandaliwa kwa kujiajiri au kuajiriwa. Lakini hayo mawazo ya " lazima niajiriwe serikalini"yalinifunga kichwa changu na kunichelewesha. Nimekuja kujitoa kwenye hayo mawazo ya kitumwa muda umeenda. Nashukuru Mungu lakini baadae mambo yalienda vizuri na sasahivi mimi sio mwajiriwa wa mtu yoyote .
Wazazi wa sasa tubadilike,tumeona dunia inavyoenda,tusiwalee watoto wetu na mawazo ya kuajiriwa serikalini, tusirudie makosa ya wazazi wetu.