Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 31,559
- 42,179
Mkuu ukitoa barcelona na madrid na kwa mbali Atletico kuna Timu gani spain ambayo ni Ya kutisha? Ubora wa madrid na Barcelona haufanyi la Liga iwe bora, ni kama vile sababu Bayern ama Psg wanasumbua ulaya basi na ligi zao ni bora.Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu ipi ni ligi bora kati ya la liga na EPL. Niseme kitu kimoja ambacho kinawachanganya watu ni vitu viwili: ushindani na ubora, watu wameshindwa kutofautisha both things.
Ligi ya Uingereza ni ligi ya ushindani lakini si bora, ukiangalia team kama Man U na Arsenal zina wachezaji baadhi ni wa kawaida ambao hata wakienda Leicester City number hawapati. Ndo maana wakicheza na team ndogo wanapata shida.
Ukiangalia team ya Man City ambayo ndio team bora kwa sasa EPL, ukimpeleka UEFA kajitahidi sana ni robo fainali. Kiufupi hawafanyi vizuri sana UEFA; mwaka jana kidogo ndo wamefanya vizuri lakini miaka 10 iliyopita mfululizo vilabu vya Hispania vime-dominate.
Ligi ya Hispania imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ubora wa wachezaji walionayo pamoja na soka wanaocheza ndo maana vilabu vya uingereza vikikutana na vilabu vya hispain wanapata shida Sana.
Hitimisho: ingawa me ni mshabiki wa epl lakini kuhusu ubora wa ligi naona upo hispania but tukisema ligi ya ushindani naona upo epl.
Nakupa sababu za ubora wa ligi ya uingereza.
1. Inakubalika duniani zaidi
Ligi ya uingereza ndio inayoingiza hela nyingi zaidi, na inaingiza hela nyingi sababu tv nyingi zinanunua licence kuonesha, na wananunua sana sababu waangaliaji ni wengi. Siamini kama duniani tumekuwa wapuuzi kiasi hichi kwamba tunaangalia ligi isio bora na kuacha bora.
2. Timu nyingi zaidi kufika uefa hatua muhimu.
Kwa miaka ya karibuni kama 15 iliopita timu za spain kuingia fainali uefa ni Madrid, barcelona na Atletico tu hutasikia sevila, sijui real sociedad ama granada kafika fainal uefa. Valencia aliwahi ila zamani kidogo.
Njoo uingereza sasa, man U, Arsenal, chelsea, liverpool, totenham wote wamefika fainali Na wapo kina Man city japo hawafanyi vizuri kufika huko fainali lakini robo na nusu wanafika. Even timu ngeni kama leicester ilioingia mara 1 ikafika hadi robo.
Hivyo kuwa wigo wa timu nyingi zinazofanya vizuri uingereza ( timu 6) compare na 3 za la liga kunaonesha ubora wa hii ligi.
3. Uwepo wa top 6.
Ligi ya uingereza ikianza ni ngumu kutabiri nani anachukua kombe kuna timu 6 sometime hadi 7 ukimhesabu na leicester zenye uwezo wa kubeba kombe, ila kule spain ni madrid ama barcelona ili timu nyingine ichukue kombe spain inabidi hao mabwana wakubwa wawe vibaya, yani wao kufikisha point zaidi ya 100 ni kitu cha kawaida.
4. Uwezo wa kifedha.
Mpira ni hela, ili uwe na timu bora unahitaji uwe na uwezo wa kusajili. Hivyo timu ndogo ama za kati ligi ya uingereza zina uwezo wa kugombania wachezaji wakubwa na timu kubwa za ligi nyengine.
Chukulia mfano wolves watu kama moutinho, neves, patricio etc wote wametolewa timu kubwa. Same kwa timu kama Everton na westham zenye uwezo wa ku attract kina Anceloti, Pelegrini, ama wachezaji kama Gomez toka barcelona, Felipe Anderson lazio, Kean toka juve etc.
Hivyo unaona timu za kati uingereza sasa hivi zina uwezo kirahisi kuwa top 4 ligi nyengine.