Ni ipi ligi bora kati ya La Liga na EPL?

Mkuu ukitoa barcelona na madrid na kwa mbali Atletico kuna Timu gani spain ambayo ni Ya kutisha? Ubora wa madrid na Barcelona haufanyi la Liga iwe bora, ni kama vile sababu Bayern ama Psg wanasumbua ulaya basi na ligi zao ni bora.

Nakupa sababu za ubora wa ligi ya uingereza.

1. Inakubalika duniani zaidi
Ligi ya uingereza ndio inayoingiza hela nyingi zaidi, na inaingiza hela nyingi sababu tv nyingi zinanunua licence kuonesha, na wananunua sana sababu waangaliaji ni wengi. Siamini kama duniani tumekuwa wapuuzi kiasi hichi kwamba tunaangalia ligi isio bora na kuacha bora.

2. Timu nyingi zaidi kufika uefa hatua muhimu.
Kwa miaka ya karibuni kama 15 iliopita timu za spain kuingia fainali uefa ni Madrid, barcelona na Atletico tu hutasikia sevila, sijui real sociedad ama granada kafika fainal uefa. Valencia aliwahi ila zamani kidogo.

Njoo uingereza sasa, man U, Arsenal, chelsea, liverpool, totenham wote wamefika fainali Na wapo kina Man city japo hawafanyi vizuri kufika huko fainali lakini robo na nusu wanafika. Even timu ngeni kama leicester ilioingia mara 1 ikafika hadi robo.

Hivyo kuwa wigo wa timu nyingi zinazofanya vizuri uingereza ( timu 6) compare na 3 za la liga kunaonesha ubora wa hii ligi.

3. Uwepo wa top 6.
Ligi ya uingereza ikianza ni ngumu kutabiri nani anachukua kombe kuna timu 6 sometime hadi 7 ukimhesabu na leicester zenye uwezo wa kubeba kombe, ila kule spain ni madrid ama barcelona ili timu nyingine ichukue kombe spain inabidi hao mabwana wakubwa wawe vibaya, yani wao kufikisha point zaidi ya 100 ni kitu cha kawaida.

4. Uwezo wa kifedha.
Mpira ni hela, ili uwe na timu bora unahitaji uwe na uwezo wa kusajili. Hivyo timu ndogo ama za kati ligi ya uingereza zina uwezo wa kugombania wachezaji wakubwa na timu kubwa za ligi nyengine.

Chukulia mfano wolves watu kama moutinho, neves, patricio etc wote wametolewa timu kubwa. Same kwa timu kama Everton na westham zenye uwezo wa ku attract kina Anceloti, Pelegrini, ama wachezaji kama Gomez toka barcelona, Felipe Anderson lazio, Kean toka juve etc.

Hivyo unaona timu za kati uingereza sasa hivi zina uwezo kirahisi kuwa top 4 ligi nyengine.
 
..maana yake hata Seria A ni bora zaidi kuliko EPL maana Cr7 ana wastani mdogo sana wa Magoli kuliko ilivyokuwa EPL.
Msimu mmoja tu ndio Ronaldo alifunga magoli mengi ila kikawaida ligi hakuwa akifikisha 20.
 
Mkuu kuingiza pesa nyingi au kuangaliwa sana hapa bongo sio kigezo cha ligi kuwa bora. Je kwa miaka kumi iliyopita timu za EPL zimechukua UCL mara ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuingiza pesa nyingi au kuangaliwa sana hapa bongo sio kigezo cha ligi kuwa bora. Je kwa miaka kumi iliyopita timu za EPL zimechukua UCL mara ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Timu moja kuchukua ubingwa si kigezo kwamba ligi fulani ni bora ila timu nyingi za ligi moja kinaweza. Mfano

Fainali 2005 liva na Ac milan
Fainali 2006 arsenal barca
Fainali 2007 liva na Ac
Fainali 2008 man u na chelsea
Fainali 2009 man u na barca
Fainali 2010 inter na bayern
Fainali 2011 man u barca
Fainali 2012 chelsea bayern

Hivyo unaona miaka 8 timu nne za ligi ya uingereza kasoro mwaka 1 tu hazijawa fainali ila miaka 7 ni uingereza mfululizo.

Ikaja domination ya madrid na ligi ya uingereza ikaja tena msimu wa juzi liver na madrid na msimu uliopita uingereza tupu liver na spurs.
 
Wewe nae sijui umetokea wapi? Unalinganisha EPL na vitu vya kijinga. EPL Watford anayeshuka daraja anamfunga bingwa mtetezi Man City, hiyo ndio maana ya ligi bora. Hata watu wa betting wanajua kaangalie ODDS utajua namaanisha nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…