Ni ipi Logic ya kumpeleka mtoto wa miaka 5 Bording School?

Ni ipi Logic ya kumpeleka mtoto wa miaka 5 Bording School?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Leo kama kawaida ndio wanafunzi wanajiandaa kurudi shule kwa ajili ya kesho kuanza Masomo.

Sasa kwenye pitapita zangu nikakutana na vitoto nadhani vina miaka Minne hadi Mitano viko na wazazi wao na vimevalishwa uniform. Nadhani ile ndo point ya wao kukutania ili watoto wabebwe kwenda shule.

Wale watoto ni wadogo mno mno muda kama ule na baridi la Arusha walitakiwa wawe wamelala.

Sijajua tunakwama wapi aisee, mbona hata kuku au hata Wanyama wanatuzidi akili inapokuja swala la kutunza watoto?

Ni ubize wa kiwango kipi unaofanya mzazi kupeleka mtoto wake wa miaka minne Bording?

Hivi linapokuja swala la mtoto kweli kuna Optional? Kwamba watu wanachagua pesa badala ya watoto?

Kwa sababu kupeleka mtoto mdogo Bording ni kwamba Mzazi yeye pesa ndo kila kitu na sio mtoto.

Then utasikia Mzazi anasifia shule kwamba ile shule ina Matron mzuri sana ina Mazingira mazuri sana, wanakula chakula kizuri sana, wana Vitanda vizuri na kadhalika, Huu ni ujinga wa kiwango cha kutisha.

Mimi nililelewa kijijini nilikuwa nakunywa uji bila sukari make hakukuwa na pesa ya sukari lakini nilitunzwa na wazazi na nilikuwa na furaha.Tulikuwa tunalalia ngozi za Ng'ombe ila tulikuwa na furaha na amani.

Swala sio mazingira sijui mandhari bali malezi.

Malezi na Mandhari ni vitu viwili tofauti kabisa.

Mnaweza ishi kwenye nyumba ya maturubai na bado mtoto akapata malezi bora kabisa, hata wakimbizi wanaishi kwenye mahema ila wanawapatia watoto wao malezi bora.
 
Madness and Stupidity

Nadhani kwakuwa wazazi wengi wakosa ufahamu wa elimu ya Post and Prenatal stages.

0-8 years hakikisha mwanao umekaa nae wewe ili kuimarisha bond kati yenu pia ili kumshape vile unavyotaka kwa kuzingatia misingi ya ulimwengu na Imani yako.
 
Madness and Stupidity
Nadhani kwakua wazazi wengi wakosa ufahamu wa elimu ya Post and Prenatal stages.
0-8 years hakikisha mwanao umekaa nae wewe ili kuimarisha bond kati yenu pia ili kumshape vile unavyotaka kwa kuzingatia misingi ya ulimwengu na Imani yako.
Sasa Wazazi wengi hilo hawalijui na mbaya zaidi kuna wanaowapeleka ili wapate muda hata wa kula bata. Tena kuna wanaoona ni sifa kupeleka mtoto bording
 
Kupeleka mtoto wako boarding ni ujinga wa hali ya juu na roho mbaya. Kuna siku nilikuwa nachat na mzungu mmoja, akasema ile tabia ya wazungu ya roho mbaya mpaka kufikia kuwageuza race zingine watumwa ni mfumo ulitengenezwa mahsusi.

Mfumo huo ni kuwapeleka watoto wakiwa wadogo boarding ili wasiwe na mapenzi na mtu yeyote (emotional detachment). Hivyo kwasababu huyo mtoto anaenda kuishi na watu ambao sio damu yake, analelewa na watu ambao sio damu yake, inamfanya awe kauzu na akose utu.

Hivyo mimi naamini hata mzazi kama anampenda kweli mtoto wake hawezi mpeleka boarding. Kwasababu siku hizi boarding schools ndio imekuwa viwanda vya kuzalisha mashoga.

Wale watoto wakubwa kwa umri wanawalaghai wadogo na kuwaingilia kinyume na maumbile. Mimi nilishasema mtoto wangu ataenda boarding akimaliza form 4.

Period! Wakati huo atakuwa na akili zake timamu na tumeishi kama familia na anajua values za familia
 
Kupeleka mtoto wako boarding ni ujinga wa hali ya juu na roho mbaya. Kuna siku nilikuwa nachat na mzungu mmoja, akasema ile tabia ya wazungu ya roho mbaya mpaka kufikia kuwageuza race zingine watumwa ni mfumo ulitengenezwa mahsusi.

Mfumo huo ni kuwapeleka watoto wakiwa wadogo boarding ili wasiwe na mapenzi na mtu yeyote (emotional detachment). Hivyo kwasababu huyo mtoto anaenda kuishi na watu ambao sio damu yake,analelewa na watu ambao sio damu yake, inamfanya awe kauzu na akose utu.

Hivyo mimi naamini hata mzazi kama anampenda kweli mtoto wake hawezi mpeleka boarding. Kwasababu siku hizi boarding schools ndo imekuwa viwanda vya kuzalisha mashoga.

Wale watoto wakubwa kwa umri wanawalaghai wadogo na kuwaingilia kinyume na maumbile. Mimi nilishasema mtoto wangu ataenda boarding akimaliza form 4.

Period! Wakati huo atakuwa na akili zake timamu na tumeishi kama familia na anajua values za familia
Wazazi wa mwendo kasi hawajui hili
 
Mimi boarding nilienda nikiwa form 5 ila daah shida niliyokuwa naiona ingawa boarding yenyewe ilikuwa na mazingira mazuri pamoja na chakula kilikuwa kizuri sana lakini nilikuwa naona kero tu, sasa umpeleke mtoto wa miaka mitano
 
Leo kama kawaida ndo wanafunzi wanajiandaa kurudi shule kwa ajili ya kesho kuanza Masomo.

Sasa kwenye pitapita zangu nikakutana na vitoto nazani vina miaka Minne hadi Mitano viko na wazazi wao na vimevalishwa uniform. Nazani ile ndo point ya wao kukutania ili watoto wabebwe kwenda shule.

Wale watoto ni wadogo mno mno muda kama ule na baridi la Arusha walitakiwa wawe wamelala.

Sijajua tunakwama wapi aisee, mbona hata kuku au hata Wanayama wanatuzidi akili inapokuja swala la kutunza watoto?

Ni ubize wa kiwango kipi unao fanya mzazi kupeleka mtoto wake wa miaka minne Bording?

Hivi linapo kuja swala la mtoto kweli kuna Optional? Kwamba watu wanachagua pesa badala ya watoto?

Kwa sababu kupeleka mtoto mdogo Bording ni kwamba Mzazi yeye pesa ndo kila kitu na sio mtoto.

Then utasikia Mazazi anasifia shule kwamba ile shule ina Matron mzuri sana ina Mazingira mazuri sana, wanakula chakula kizuri sana, wana Vitanda vizuri na kadhalika, Huu ni ujinga wa kiwango cha kutisha.

Mimi nililelewa kijijini nilikuwa nakunywa uji bila sukari make hakukuwa na pesa ya sukari lakini nilitunzwa na wazazi na nilikuwa na furaha.Tulikuwa tunalalia ngozi za Ng'ombe ila tulikuwa na furaha na amani.

Swala sio mazingira sijui madhari bali malezi.

Malezi na Mandhari ni vitu viwili tofauti kabisa.

Mnaweza ishi kwenye nyumba ya maturubai na bado mtoto akapata malezibora kabisa, hata wakimbizi wanaishi kwenye mahema ila wana wapatia watoto wao malezi bora.
Uvivu wa kulea. Ijapokuwa ni vyema pale unapoona hupendi mtoto wenu arithi tabia zenu kwa sababu ni za hovyo. Unaweza ukampeleka huko akapate tabia ya hovyo improved
 
Hawa wazazi wanaofanya hivi wanahitaji kufanyiwa brain checkup.

Mtoto wa miaka 5 bado ni mdogo sana kiasi cha yeye kuweza kuelewa mambo mengi ya dunia hii chafu na ndio maana kunakuwepo wazazi ili mtoto afuate njia sahihi na asipotee.

Sasa kama mzazi unapeleka mtoto wa miaka 5 mbali na wewe kwa kisingizio cha kusoma au shule nzuri conclusion ni huyo mzazi hajitambui.

Na kama mtu hujitambui ni bora usizae kabisa, matokeo yake taifa linapata watu wenye tabia za ajabu na wasiojitambua kwa kukosa malezi bora ya baba na mama sababu ya wazazi wasiojitambua.

Serikali ndio solution ya hili tatizo sababu wazazi wasiojitambua hawawezi kuisha leo na ni wengi mno.
Mtu anayejipiga picha nusu uchi na kuirusha mtandaoni huyo kamwe hawezi kuwa mzazi anayejitambua.

Serikali ipige marufuku mtoto chini ya miaka 16 kwenda boarding schools. problem solved.

Hapo ndio njia pekee ya kuokoa kizazi kijacho na kujenga taifa la watu wenye maadili na wanaojitambua.
 
Back
Top Bottom