Ni ipi mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kutatua tatizo la ajira nchini Tanzania?

Ni ipi mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kutatua tatizo la ajira nchini Tanzania?

Umetoa majibu ya kisiasa.

Bado hujataja mipango ya serikali kutatua changamoto ya ajira.

Mfano kijana ana kipaji cha ubunifu au wazo la ajira, serikali inamsaidia vipi? Au kazi ya serikali ni kukusanya mapato tu?
Chief!!

Ukiwa unaishi nchi za dunia ya tatu, jifunze jinsi ya kupambana na Hali yako.

Usiwategemee wanasiasa

Mbona kuna mashirika kibao ya mabeberu yanatoa mitaji kwa vijana wanaotoka nchi maskini?

Jifunze kujiongeza na kamwe usiwategemee wanasiasa hasa hasa hawa dizaini ya awamu tano.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mbona kuna mashirika kibao ya mabeberu yanatoa mitaji kwa vijana wanaotoka nchi maskini?
Hiyo ni mada nyingine. Wewe unaniambia mabeberu wanatoa mitaji, hivi swali langu umelielewa Kweli?

Nataka kujua serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ina mipango gani kutatua changamoto ya ajira!
 
Kitu ambacho wengi hatujagundua degree ya bongo inq expire date.
ukishafika miaka 35-45 hauajiriki tena😂😂😂😂
 
Kuna kitu watu wa HR wanaita ADEA (Age Discrimination Employment Acts) hapa mtu anabaguliwa hapati ajira kutokana na umri ,angalia nafasi nyingi za kazi zikitangazwa utaona wanaweka age limit utasikia not above 35 au not above 45 ss sidhani km Tz tuna hii kitu inayoitwa ADEA labda watu wa HR na au Sheria watusaidie ufafanuzi maana mm ni mhandisi sina uelewa mpana nyanja hii.

Hapa inamaana kama una umri kuanzia 35-45 ni ngumu sana kuajriwa serikalini au taasisi binafsi na kufanya bachelor yako hiwe kama ime expire.
😂😂
 
Umenichanganya Sana. Watoto wa masikini hata pesa ya kununua ndoano hawana. Dadeki
 
Nikisikia hizi kelele za wanasiasa kwamba vijana waende wakajiajiri,nakumbuka maneno ya Dr mmoja wa uchumi Kenya,DR David Ndii,wakati anachambua uchumi wa Kenya,anasema "there is no private solution for a public problem"Swala la ajira ni public problem,uwezi kulitatua kwa vijana kufanya uchuuzi,ambao Wala haukidhi mahitaji yao ya kila siku,
 
Back
Top Bottom