Ni ipi nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sasa?

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Anapoapishwa Rais, nafasi ya kwanza kuteuliwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Walioweka utaratibu huu hawakuwa wajinga kwa sababu kila jambo analofanya Rais linatakiwa kuwa sawa kisheria hivyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sahihi katika jicho la Sheria. Kazi ya mwanasheria Mkuu ni kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sawa kisheria.

Tangu awamu ya 5 , nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanza kuonekana kama kivuli tu na sio nafasi ya mshauri ya Rais kuhusu mambo ya kisheria ili maamuzi na matendo ya Rais na Serikali yawe sahihi kisheria.

Alianza marehemu magufuli kwa kutompa Prof Assad kipindi cha pili kinyume na matakwa ya katiba. Juzi mahakama ikatoa uamuzi kusema Rais alivunja katiba.

Sasa kafanya Samia kwa kutompa Prof Luoga kipindi cha pili cha miaka mitano kinyume na matakwa ya Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006. Hapa Rais wangu kipenzi nae kavunja Sheria

Ikumbukwe moja ya sababu za Rais kuondolewa madarakani ni kuvunja Katiba au Sheria hivyo haipaswi Rais kuonekana anavunja Katiba au Sheria waziwazi namna hii.

Ifike kipindi Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ionekane na kutumika inavyopaswa!

UPDATES
Sasa limetokea hili lingine
 
Sio lazima Gavana wa Benki kuu au CAG wamalize miaka 10, suala ni utaratibu na sababu zinazotumika kuwaondoa.
 
Waliotunga hizo sheria hawakuwa wajinga. Kitaalamu wanasema hizo nafasi zimewekewa security of tenure.

Kutokana na unyeti wake hizo nafasi, zimewekewa ulinzi wa kisheria, hivyo wanaposhika hizo nafasi wanalindwa na sheria hizo hadi inapotokewa wanatoka kwa taratibu zilizowekwa na sheria zenyewe.

Rais anapofanyia kazi jambo lolote lililowekewa utaratibu kisheria lazima apate ushauri wa kisheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ushauri huu ndo final kwa sababu endapo Rais akikiuka basi anavunja sheria na kuweka nafasi yake ya Urais matatani.
 
Assad aliondolewa akiwa hajafikisha umri wa kustaafu, huyu ameondolewa akiwa kafikisha umri wa kustaafu.

Prof Luoga ana miaka mingapi? Weka uthibitisho hapa
 
Anapoapishwa Rais, nafasi ya kwanza kuteuliwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Walioweka utaratibu huu hawakuwa wajinga kwa sababu kila jambo analofanya Rais linatakiwa kuwa sawa kisheria hivyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sahihi katika jicho la Sheria. Kazi ya mwanasheria Mkuu ni kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sawa kisheria.

Tangu awamu ya 5 , nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanza kuonekana kama kivuli tu na sio nafasi ya mshauri ya Rais kuhusu mambo ya kisheria ili maamuzi na matendo ya Rais na Serikali yawe sahihi kisheria.

Alianza marehemu magufuli kwa kutompa Prof Assad kipindi cha pili kinyume na matakwa ya katiba. Juzi mahakama ikatoa uamuzi kusema Rais alivunja katiba.

Sasa kafanya Samia kwa kutompa Prof Luoga kipindi cha pili cha miaka mitano kinyume na matakwa ya Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2008. Hapa Rais wangu kipenzi nae kavunja Sheria

Ikumbukwe moja ya sababu za Rais kuondolewa madarakani ni kuvunja Katiba au Sheria hivyo haipaswi Rais kuonekana anavunja Katiba au Sheria waziwazi namna hii.

Ifike kipindi Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ionekane na kutumika inavyopaswa!
 
Anapoapishwa Rais, nafasi ya kwanza kuteuliwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Walioweka utaratibu huu hawakuwa wajinga kwa sababu kila jambo analofanya Rais linatakiwa kuwa sawa kisheria hivyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sahihi katika jicho la Sheria. Kazi ya mwanasheria Mkuu ni kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sawa kisheria.

Tangu awamu ya 5 , nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanza kuonekana kama kivuli tu na sio nafasi ya mshauri ya Rais kuhusu mambo ya kisheria ili maamuzi na matendo ya Rais na Serikali yawe sahihi kisheria.

Alianza marehemu magufuli kwa kutompa Prof Assad kipindi cha pili kinyume na matakwa ya katiba. Juzi mahakama ikatoa uamuzi kusema Rais alivunja katiba.

Sasa kafanya Samia kwa kutompa Prof Luoga kipindi cha pili cha miaka mitano kinyume na matakwa ya Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2008. Hapa Rais wangu kipenzi nae kavunja Sheria

Ikumbukwe moja ya sababu za Rais kuondolewa madarakani ni kuvunja Katiba au Sheria hivyo haipaswi Rais kuonekana anavunja Katiba au Sheria waziwazi namna hii.

Ifike kipindi Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ionekane na kutumika inavyopaswa!
Uko sahihi mkuu!
Tatizo nchi yetu kwa sasa,ingawa tunajinasibu kuwa na amani.

Kiuhalisia bado ni "Divided State"
Kwa maana atatetewa yule ambaye tu ametoka kundi la wateule washika mpini kwa muda husika.

Hapa hutamsikia Zitto kabwe akijitokeza kulisemea hili.

"Menejimenti ya Benki Kuu inaundwa na Gavana, Manaibu Gavana, Wakurugenzi, Mameneja na Mameneja Wasaidizi. Gavana na Manaibu Gavana huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa mujibu wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, na hutumikia nyadhifa hizo kwa muda wa miaka mitano. Aidha, huweza kuteuliwa tena kutumikia nyadhifa hizo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Wakurugenzi, Mameneja na Mameneja Wasaidizi huteuliwa na Gavana kwa kuzingatia vigezo vya utendaji bora. Gavana ni Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu na pia ni mwenyekiti wa Bodi ambaye anawajibika katika maamuzi yote ya kisera yanayotolewa na Bodi. Vilevile, Gavana anawajibika katika Menejimenti kuteua au kumuachisha kazi mfanyakazi kutokana na sababu mbalimbali na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa."
 
Haipaswi Rais kuonekana anafanya makosa ya wazi namna hii

Kuna shida mahala. Hata press release za Ikulu lazima ziwe na vifungu vya Sheria vinavyompa mamlaka Rais kufanya maamuzi husika ila hili halifanyiki.

Tunaishi kama wanyama
 
Uko sahihi mkuu!
Tatizo nchi yetu kwa sasa,ingawa tunajinasibu kuwa na amani.

Kiuhalisia bado ni "Divided State"
Kwa maana atatetewa yule ambaye tu ametoka kundi la wateule washika mpini kwa muda husika.

Hapa hutamsikia Zitto kabwe akijitokeza kulisemea hili.

"Menejimenti ya Benki Kuu inaundwa na Gavana, Manaibu Gavana, Wakurugenzi, Mameneja na Mameneja Wasaidizi. Gavana na Manaibu Gavana huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa mujibu wa Kifungu cha 8 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, na hutumikia nyadhifa hizo kwa muda wa miaka mitano. Aidha, huweza kuteuliwa tena kutumikia nyadhifa hizo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Wakurugenzi, Mameneja na Mameneja Wasaidizi huteuliwa na Gavana kwa kuzingatia vigezo vya utendaji bora. Gavana ni Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu na pia ni mwenyekiti wa Bodi ambaye anawajibika katika maamuzi yote ya kisera yanayotolewa na Bodi. Vilevile, Gavana anawajibika katika Menejimenti kuteua au kumuachisha kazi mfanyakazi kutokana na sababu mbalimbali na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa."
Kifungu cha 8 kinasema Governor " SHALL BE " eligible for re appointment

Kwa manaibu gavana kinasema " Be elligible" for re appointment

Kwa tafsiri sahihi ya Kisheria Shall kwa gavana inamaanisha lazima apewe kipindi cha pili na kwa manaibu gavana be eligible inamaanisha sio lazima apewe kipindi cha pili kwa sababu manaibu gavana wamewekewa tu "Be" na sio "Shall"
 
Huyu alitimiza hiki kifungu?

(b) has not less than fifteen years experience in the fields of economics,
banking, accountancy or finance or law;
Kifungu cha 8 kinasema Governor " SHALL BE " eligible for re appointment

Kwa manaibu gavana kinasema " Be elligible" for re appointment

Kwa tafsiri sahihi ya Kisheria Shall kwa gavana inamaanisha lazima apewe kipindi cha pili na kwa manaibu gavana be eligible inamaanisha sio lazima apewe kipindi cha pili kwa sababu manaibu gavana wanewekewa tu "Be" na sio "Shall"
 
Huyu alitimiza hiki kifungu?

(b) has not less than fifteen years experience in the fields of economics,
banking, accountancy or finance or law;
Prof Luoga amefanya kazi za kisheria kwa zaidi ya miaka 15 kwahiyo uteuzi wake kuwa gavana ulikidhi vigezo
 
Anapoapishwa Rais, nafasi ya kwanza kuteuliwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Walioweka utaratibu huu hawakuwa wajinga kwa sababu kila jambo analofanya Rais linatakiwa kuwa sawa kisheria hivyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sahihi katika jicho la Sheria. Kazi ya mwanasheria Mkuu ni kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sawa kisheria.

Tangu awamu ya 5 , nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanza kuonekana kama kivuli tu na sio nafasi ya mshauri ya Rais kuhusu mambo ya kisheria ili maamuzi na matendo ya Rais na Serikali yawe sahihi kisheria.

Alianza marehemu magufuli kwa kutompa Prof Assad kipindi cha pili kinyume na matakwa ya katiba. Juzi mahakama ikatoa uamuzi kusema Rais alivunja katiba.

Sasa kafanya Samia kwa kutompa Prof Luoga kipindi cha pili cha miaka mitano kinyume na matakwa ya Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006. Hapa Rais wangu kipenzi nae kavunja Sheria

Ikumbukwe moja ya sababu za Rais kuondolewa madarakani ni kuvunja Katiba au Sheria hivyo haipaswi Rais kuonekana anavunja Katiba au Sheria waziwazi namna hii.

Ifike kipindi Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ionekane na kutumika inavyopaswa!
KUMBUKA MAGUFULI na NDUGAI walipitisha Sheria ya KINGA Hata wakikiuka KATIBA
 
Halima Mdee na Wahuni wenzake 18 Walifukuzwa na Chadema lakini Wakaendelea kuwa Wabunge MBONA MWANASHERIA MKUU wa Serikali ALIKAA KIMYA ILA MNATAKA ASHAURI LA GAVANA?
 
Kufundisha sheria chuo sio kufanya kazi za kisheria. Hata Kilangi ilikuwa ndio hivyo hivyo.
Katiba mpya ni muhimu sana kuweka haya mambo sawa.
Ni wakili wake zaidi ya miaka 20 pia kupitia kampuni yake ya uwakili ya FK yenye ofisi Upanga sea view
 
Halima Mdee na Wahuni wenzake 18 Walifukuzwa na Chadema lakini Wakaendelea kuwa Wabunge MBONA MWANASHERIA MKUU wa Serikali ALIKAA KIMYA ILA MNATAKA ASHAURI LA GAVANA?
Hili ndo tatizo. Kuanzia awamu ya 5 nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali imekuwa ikipwaya sana jambo ambalo lisipoangaliwa vizuri linaweza kuiweka hata nafasi ya Rais rehani
 
Halima Mdee na Wahuni wenzake 18 Walifukuzwa na Chadema lakini Wakaendelea kuwa Wabunge MBONA MWANASHERIA MKUU wa Serikali ALIKAA KIMYA ILA MNATAKA ASHAURI LA GAVANA?
Kama tungekuwa na mwanasheria mkuu wa serikali imara hawa wabunge hawakupaswa kuwa bungeni kwa sababu ni kinyume na sheria na wangeshauri na kusimamia ushauri wao.

Kama maspika hawa wangetaa ushauri wa mwanasheria mkuu basi wangepaswa kuondolewa katika nafasi zao za uspika
 
KUMBUKA MAGUFULI na NDUGAI walipitisha Sheria ya KINGA Hata wakikiuka KATIBA
Hakuna kinga kwenye kuvunja katiba au sheria
Screenshot_20230108-120653_Adobe Acrobat.jpg
 
Anapoapishwa Rais, nafasi ya kwanza kuteuliwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Walioweka utaratibu huu hawakuwa wajinga kwa sababu kila jambo analofanya Rais linatakiwa kuwa sawa kisheria hivyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sahihi katika jicho la Sheria. Kazi ya mwanasheria Mkuu ni kumshauri Rais kuhusu maamuzi yake yote ili yawe sawa kisheria.

Tangu awamu ya 5 , nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanza kuonekana kama kivuli tu na sio nafasi ya mshauri ya Rais kuhusu mambo ya kisheria ili maamuzi na matendo ya Rais na Serikali yawe sahihi kisheria.

Alianza marehemu magufuli kwa kutompa Prof Assad kipindi cha pili kinyume na matakwa ya katiba. Juzi mahakama ikatoa uamuzi kusema Rais alivunja katiba.

Sasa kafanya Samia kwa kutompa Prof Luoga kipindi cha pili cha miaka mitano kinyume na matakwa ya Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006. Hapa Rais wangu kipenzi nae kavunja Sheria

Ikumbukwe moja ya sababu za Rais kuondolewa madarakani ni kuvunja Katiba au Sheria hivyo haipaswi Rais kuonekana anavunja Katiba au Sheria waziwazi namna hii.

Ifike kipindi Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ionekane na kutumika inavyopaswa!
Mfupa uliowashinda wengi ! Ni Katiba ndio inayoleta Conflict of interest nyingi !! Upande mmoja sheria inasema hivi na kisha wakati huo huo Mkuu wa Nchi anakuwa halazimiki kufuata maana anakuwa ana choice ya kufuata au kuacha !! Hapo huwezi kumlaumu !!
 
Rais asipofanya jambo kwa mujibu wa katiba au Sheria matokeo yake anajiweka kwenye hatari ya kuondolewa madarakani na Bunge.

Ni most serious offence kwa Rais. Kukiuka Katiba au Sheria

Kwa suala la CAG kwa sababu Katiba ndo sheria kuu ilipaswa magufuli afuate Katiba

Kwa suala la Luoga katiba haisemi kitu ila Sheria ya Benki Kuu inasema lazima gavana ateuliwa kwa kipindi cha pili cha miaka 5 hivyo ni lazima sheria ifuatwe
 
Back
Top Bottom