lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Mahusiano Ni kitu kizuri
Mapenzi Ni kitu kizuri na
Urafiki ni kitu kizuri.
Sio mbaya kwa kijana kujipatia mahusiano,mpenzi au rafiki hapa JF au mitandao mingine kama JF isiyo ya kujiuza. Kwa mfano mtu anaweza kupata mchumba na baadae mke hapahapa JF. Kwani Kuna ubaya jamani?
Nahisi Me na Ke wengi wa jukwaa hili wamekua wakipata shida jinsi ya kutongozana kwa kuogopa yafuatayo:
Baada ya mawasiliano ya DM, na kupeana namba za simu,Sasa kimbembe Ni namna ya kukutana. Maswali yanakuja.
Je siku ya kwenda kuonana akimkuta haendani nae kwa 100%,atafanyaje.
Kutokuendana namaanisha
-Umri
-Mwonekano(haiba)
-Imani
-Jamii
-N.k
Hali hii imepelekea vijana wengi kutafuta kuonana kwa kuviziana.Mfano wakikubaliana kukutana mahala fulani saa fulani,mmojawapo au wote bila kuambizana huwahi kufika muda mrefu nyuma kabla ya muda wa makubaliano ili kuvizia kumuona huyo mpenzi mtarajiwa ili kuona mwonekano wake,na atakae wahi kumtambua mwenza kutokana na password walizowekeana na akaona sivyo alivyokuwa akimtegemea Basi mtu huyo humtoroka bila kuonana na akishakua mafichoni hupiga siku kwa kutoa udhuru wa uongo.
Ama ikitokea wakakutana na kukuta hayuko kama alivyokuwa akimfikiria,akimuwazia ama akimtarajia.basi hufedheheka Sana Tena mbele ya mgeni wake.
Njia isiyo na fedheha Ni:
Ukipendezwa na mtu yeyote kwa michango yake,maana hatujuani kwa sura na ukataka kukutana naye na mkawasiliana akakubali kuja ili mfahamiane zaidi kwa kuonana,fanya hivi:
Mwambie jinsi ambavyo unatamani kukutana nae uso kwa uso ili mfahamiane kwa Nia njema tu.Mhakikishie kuwa unapendezwa Sana na michango yake hivyo anaweza kuwa msaada kwako. Hapa namaanisha usioneshe shauku yoyote ya kumtongoza au mambo ya mapenzi.
Ikitokea akakubali kuja eneo la miadi,jiweke Tayari kisaikolojia kumpokea mtarajiwa wa aina yeyote. Kwa maana aweza kuja ndugu yako, bosi wako, kiongozi au mshirika wako kidini, jirani yako, mke au mume wako au mtu mwenye muonekano ambao haukuutarajia.
Basi akitokea mtu wa namna hiyo na kwa sababu hukuwa umemtongoza au hukua umemtamkia neno lolote baya,Basi mnaweza kufurahia kufahamiana na mazungumzo ya kawaida baina yenu.
1. Kama mlikua mnafahamiana pongezaneni na Kama mlikutana hoteli au mgahawani au Bar,Basi mnaweza agiza vinywaji mkaendelea na mazungumzo huku ukionesha kuwa umefurhi Sana kufahamu kuwa kumbe Ni yy mlikua mkiwasiliana nae kwa fake ID.
2. Kama mlikua hamfahamiani lakini umekuta Ni mtu ambae Yuko kinyume kabisa na matarajio yako,Hana kabisa sifa unazozitaka fanya Kama hapo namba1 juu.
Namaanisha kuwa Kama mlikutana hoteli,bar au mgahawani huduma zote ziendelee kama kawaida,huku ukionesha kufurahi kukutana nae bila kumuonesha kuwa hujaridhishwa nae,na Wala usimtongoze.
Unaweza kuleta mada nyingine kabisa mfano"Kama kumuomba akusaidie kupata kazi"n.k.
3. Ukikuta Ana sifa na vigezo vyote unavyovitaka wewe, MTONGOZE, yaani Mweleze yako yote ya moyoni.
Njia hi inaepusha kumdhalilisha,kumfedhehesha na kumvunjia mtu heahima.
Hakikisha unapopanga kukutana nae,uwe na hesabu ya kutosha mfukoni.