Ni ipi njia isiyo na fedheha ya kutongoza mwanamke mtandaoni ambaye hamjawahi onana?

Njia rahisi na halisi, eleza ukweli. Achana na mambo ya kuchangia mada kama bill gates au elon musk wa tesla. Kingine acha kuonesha tabia za kuigiza sana. Kifupi, jiweke vile ulivyo. Kama hauendani na vigezo vyake ataamua mapema na kukupa jibu sahihi ambalo halitakufedhehesha na pia ikitokea mkaingia kwenye mahusiano mkiwa mnafahamiana (kiuchumi, kitabia, kimuonekano n.k) siku mnaonana kwa mara ya kwanza haitawapa shida sana kufurahia mtoko wenu. Ukiigiza lazima kuna mahali utapwaya. Waweza kumuomba muonane halafu mwenzako akakwambia anatamani mkutane mlimani city au palm village, wakati mwenznagu na mimi hizo sehemu kwako ni ndoto mwisho wa siku unaenda kuaibika bure.

Au Darlin unasemaje kuhusu hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…